Kinana aivuruga Lumumba

Kinana aivuruga Lumumba

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Kuna sintofahamu katika Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba kuhusu ziara zinazoendelea za Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana. Patashika hiyo ya kichama ni kuhusu hasa timu inayoambatana na Kinana katika ziara za mikoani.Makada waandamizi wa Lumumba wanadai kuwa ziara za Kinana hazilengi kuimarisha chama kama zinavyoonekena ila ni kujitangaza na kuwatangaza anaoambatana nao ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Werevu tunajua.Katibu Mkuu na timu yake wako katika kujitangaza na kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Hakuna jipya ambalo wanalifanya. Ndiyo maana hata timu yake haibadiliki.Ni kwamba amechagua vijana wa kuwatangaza na wengine kuwatenga. Kwanini timu haibadiliki? Kwani nani hawezi kuhutubia na nani hataki posho?" aliuliza kwa kulalama kada mmoja maarufu aliyehamia CCM katika miaka ya karibuni.

"Ziara za Katibu Mkuu zitaleta ubaguzi chamani na mpasuko usio na maana. Chama hakiimarishwi na watu wale wale kila siku.Kila kada anaweza kwenda mikoani na kukitangaza chama. Kwanini wale wale hata kama wanaonekana kusema mambo ya kawaida sana? Tunajiandaa kuchukua hatua juu ya hili" alidakia kada mwingine wa Ofisi Ndogo Lumumba

Nionavyo,lengo kuu ni posho na umaarufu. Kumbe!??

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Angalia Mchele uliopikwa na Msomali na ule wa kwetu (Ubwabwa) Mmoja unaweza kiurahisi kuufinyanga kuwa lundo la lulitupia mdomoni huo mwingine Mmmm ni kazi...
 
Wasilalamike, ni wazi kuwa CCM ndiyo imeasisi, kubariki na kuachia utaratibu wa viongozi kujiamulia kufanya wanayotaka. Ni serikali ya CCM iliyotupa kando uwajibikaji na maadili ya viongozi wa umma. Ni CCM na viongozi wake waliofikia hatua ya kuzidharau sheria na kukiuka katiba ya nchi kwa manufaa yao.

CCM ni chama pekee ambapo watu wenye kashfa za ubakaji kama Prof. Kapuya wanaweza kupeta na vyeo vyao bila kubughudhiwa na yeyote. Ni katika CCM ambapo kiongozi anayetuhumiwa na umma anaweza kugombea uongozi wa umma huku akipigiwa kampeni na Mwenyekiti wa chama hicho bila aibu!

Tena ni katika CCM na serikali yake ambapo kiongozi anaweza kuwaamuru polisi au jeshi kuvunja sheria na kutoheshimu katiba, na asiulizwe na yeyoye. Ni katika serikali ya CCM ambapo wahalifu wateule kama Kamuhanda wanaweza kupandishwa vyeo, pamoja na mauaji waliyoyasimamia kuwa na ushahidi wa wazi!

Kwani wao walitegemea nini kutokana na chama chao? Tell them to sit tight. Katika CCM kila kisichowezekana kwingineko kinawezekana kwao. Kila kisichoruhusiwa kwingine ndani ya CCM ni ruksa!
 
Wasilalamike, ni wazi kuwa CCM ndiyo imeasisi, kubariki na kuachia utaratibu wa viongozi kujiamulia kufanya wanayotaka. Ni serikali ya CCM iliyotupa kando uwajibikaji na maadili ya viongozi wa umma. Ni CCM na viongozi wake waliofikia hatua ya kuzidharau sheria na kukiuka katiba ya nchi kwa manufaa yao.

CCM ni chama pekee ambapo watu wenye kashfa za ubakaji kama Prof. Kapuya wanaweza kupeta na vyeo vyao bila kubughudhiwa na yeyote. Ni katika CCM ambapo kiongozi anayetuhumiwa na umma anaweza kugombea uongozi wa umma huku akipigiwa kampeni na Mwenyekiti wa chama hicho bila aibu!

Tena ni katika CCM na serikali yake ambapo kiongozi anaweza kuwaamuru polisi au jeshi kuvunja sheria na kutoheshimu katiba, na asiulizwe na yeyoye. Ni katika serikali ya CCM ambapo wahalifu wateule kama Kamuhanda wanaweza kupandishwa vyeo, pamoja na mauaji waliyoyasimamia kuwa na ushahidi wa wazi!

Kwani wao walitegemea nini kutokana na chama chao? SAWA KABISAAAAAA
 
Kuna sintofahamu katika Ofisi Ndogo za CCM-Lumumba kuhusu ziara zinazoendelea za Katibu Mkuu wa CCM,Kanali Mstaafu Abdurahman Kinana. Patashika hiyo ya kichama ni kuhusu hasa timu inayoambatana na Kinana katika ziara za mikoani.Makada waandamizi wa Lumumba wanadai kuwa ziara za Kinana hazilengi kuimarisha chama kama zinavyoonekena ila ni kujitangaza na kuwatangaza anaoambatana nao ili kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwakani.

"Werevu tunajua.Katibu Mkuu na timu yake wako katika kujitangaza na kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Hakuna jipya ambalo wanalifanya. Ndiyo maana hata timu yake haibadiliki.Ni kwamba amechagua vijana wa kuwatangaza na wengine kuwatenga. Kwanini timu haibadiliki? Kwani nani hawezi kuhutubia na nani hataki posho?" aliuliza kwa kulalama kada mmoja maarufu aliyehamia CCM katika miaka ya karibuni.

"Ziara za Katibu Mkuu zitaleta ubaguzi chamani na mpasuko usio na maana. Chama hakiimarishwi na watu wale wale kila siku.Kila kada anaweza kwenda mikoani na kukitangaza chama. Kwanini wale wale hata kama wanaonekana kusema mambo ya kawaida sana? Tunajiandaa kuchukua hatua juu ya hili" alidakia kada mwingine wa Ofisi Ndogo Lumumba

Nionavyo,lengo kuu ni posho na umaarufu. Kumbe!??

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mzee tupakule, unaweza ukatumegea majina ya hao wateule ili nasiye tusiohudhuria mikutano ya 'kinana' tuwafahamu?
 
Kinana na kampeni za kugombea Urais wa Tanzania ... subirini muone
 
Back
Top Bottom