Kinana aibiwa nyumbani kwake

Kinana aibiwa nyumbani kwake

Mi nilidhani unamaanisha watu wasiofahamika wamekuja nyumbani kwake wakambeba Kinana na kutokomea nae kusikojulikana

Neno IBIWA lina tafsiri tata
 
dogo hakulamba nyara? Yani nyaraka. Na huyo mchaga anayekataa kurudisha hela ajitazame vizuri
 
Aaaaaaaah! mi nilidhani majambazi yamevamia na hata kumjeruhi Kinana! Oyaa! mbona mnapenda kutuharibia mood wengine!!
 
Huyo kijana lazima atakuwa ni mwanachama wa CDM, kapandikizwa na Mch. Msigwa...teh..teh..teh. Ni bora wazirudishe maana Kinana akipandisha mori Tembo wote watatoweka kwa muda mfupi kufidia hela yake.
 
Huko kwake hakuna benki? Aliogopa nini kuweka benki. Huo ni mtindo wakizamani kuweka fedha nyumbani. Pole sana mzee kinana. Lakini msamehe huyo kijana kwa sababu alizitumia vizuri katika mambo ya kimaendeleo.
 
huyu kijana anarudisha mali na tembo wetu, vipi ajaiiba vipuri vya viwanda vya kusaga meno ya tembo?
 
Chini ya Masaa 48 tangu Mkurugenzi wa Ugaidi na kuhatarisha Usalama atoke Segerea tumeanza kuona cheche zake!
 
thread za uzushi na uwongo uliokithiri wenye kulenga kumchafua mtu na kuishusha hadhi yake zinaihribia JF na kuonekana na moja miongoni mwa medias zinazotumiwa kimkakati katika kuchafua viongozi wa Chama na serikali. Jambo hili ni baya na linaloleta tafsir mbaya mbele ya jamii, ni vibaya mno media kutumika kwa maslahi ya mtu au kikundi. Mods thread hizi za namna hii kwanini zipewe nafasi hapa JF..?

Nape, si Kinana ni boss wako? Tupe ukweli basi, kaibiwa hajaibiwa??

Umerudi lini toka Hong Kong ulikotumwa kwenda kusimamia upakuaji wa mzigo wa bosi wako??
 
Kwa Kinana dola 60 elfu ni change tu mbona!!!!!!!!!! Nahisi nyumba yake basemet ni hela tu!!! Unajua hela za dili wakati mwingine kuweka bank ni hatari!! Bora basement wakuu.Ha ha ha. Ila kijana boga sana, yaani unaiba halafu unafanya mambo ya kuonekana? Unatulia hata miaka 5 mpaka so limalizike halafu unatimka na kufanya mambo yako kimya kimya. Ulimbukeni huu hatari sana.
 
Habari za uhakika zilizonifikia ni kwamba, Kinana amepata balaa kubwa baada ya mfanyakazi wake wa ndani kumuibia kiasi cha dola elfu 60, taarifa zinasema kuwa kijana huyo mwenye asili ya mkoa wa iringa yuko sasa hivi ktk kituo cha polisi mabatini, na tayari alikuwa ameshanunua gari moja ain ya vitz na pikipiki 3 na nyumba maeneo ya mbagala, gari na pikipiki bado zinashikiliwa na polisi na nyumba bado muuzaji anatafutwa ili arudishe pesa.

Muuzaji wa nyumba ni kijana wa kichaga na ameapa hawezi kurudisha pesa. Kwanini mtu msomi kama yule aweke kiasi kikubwa cha pesa nyumbani kwake?

Kwa uhakika zaidi juu ya suala hili ampigie mkuu wa kituo cha Mabatini hapo Kijitonyama
Hizo ni fedha za pembe za ndovu ,haingii akilini mtu wa haiba ya kinana kuweka dola zote hizo ndani wakati bank yeye hapangi foleni
 
Tembo wetu nao wapumuweeee!!!! Wanang'olewa meno bila ganzi lol!
 
Kumbe hata majangili yanaibiwa! Jamaa ameona haiwezekani akawa anafaidi tembo peke yake!
 
"Tembo ni wetu na pesa ni zetu" by Baba V
 
Last edited by a moderator:
Mi nilidhani unamaanisha watu wasiofahamika wamekuja nyumbani kwake wakambeba Kinana na kutokomea nae kusikojulikana

Neno IBIWA lina tafsiri tata

teh teh teh teeeeeh niliwaza ki2 hichohicho...
 
Back
Top Bottom