Elections 2010 Kinana aanza kuhaha kunusuru ccm kwa kutumia marais wastaafu

Negotiator

JF-Expert Member
Aug 9, 2010
303
44
Upinzani ukituzidi tutawatumia Mwinyi, Mkapa-Kinana












Mwiyi1(3).jpg

Mwenyekiti wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi



Mwenyekiti wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema marais wastaafu, Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa watashiriki kampeni za Rais Jakaya Kikwete iwapo kitazidiwa na upinzani.
Taarifa ya Kinana ilitolewa jana kwa niaba yake na mjumbe wa kamati ya kampeni za CCM, Dk. Raphael Chegeni alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kinana alisema hali ya kampeni ilivyo sasa inaashiria kuwa mambo yanakwenda vizuri.
"Sio kwamba mgombea wetu ametengwa na marais wastaafu, tunaona chama hakijazidiwa na wapinzani hivyo hakuna sababu ya kuwasumbua mzee Mwinyi na Mkapa," alisema.
Pia alisema CCM inamtambua mshindi wa kura za maoni kuwania ubunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, Hussein Bashe.
Bashe alishinda kura za maoni lakini Kamati Kuu (CC) ya CCM ilimuengua kwa kile kilichodaiwa kwamba si raia wa Tanzania.
Alisema CCM ipo tayari kumtumia Bashe katika shughuli mbalimbali za chama, ikiwemo kusaidia kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu.

SOURCE; NIPASHE http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=21247
 
Mwinyi alikwisha sema awamu ya nne rushwa imeshamili kuliko awamu zilizotangulia - kwanza naye itabidi ajibu swali la radar. Mkapa hakumpigia kampeni JK 2005, je mwaka huu atafanya hivyo? Naye itabidi ajibu maswali ya EPA, Kiwira, je yuko tayari kwa hayo?
 
Hawa wazee wanajua kusoma alama za nyakati hawawezi kujiingiza kwenye kikaango wakati wanajua wataungua wacha JK afe na tai shingoni asitegemee msaada kwa hawa wazee maana kila mtu ana skendo yake sasa wakitia mguu tu vitaibuka vya kuibuka hata vilivyo sahauliwa
 
Kama Mabere Marando aliweza kujibu kutetea mafisadi mahakamani, sioni vipi hao wengine wasiweze kujibu hayo unayoyauliza.
 
BWM hawezi thubutu kumpigia kampeni JK; yy mwenyewe ananuka rushwa na mkewe. Tutamuuliza ya Kiwira!
 
Kama Mabere Marando aliweza kujibu kutetea mafisadi mahakamani, sioni vipi hao wengine wasiweze kujibu hayo unayoyauliza.

Jiulize kwa nini hawataki Mdahalo, Wastaafu wote hao wana yao ambayo hawana majibu nayo
 
Thread inasema kwamba "Kinana aanza kuhaha kunusuru ccm kwa kutumia marais wastaafu" and the newspaper has quoted Kinana saying "Sio kwamba mgombea wetu ametengwa na marais wastaafu, tunaona chama hakijazidiwa na wapinzani hivyo hakuna sababu ya kuwasumbua mzee Mwinyi na Mkapa". Mbona unatupotosha sasa humu ndani kaka?

Yaani you had even to bend the truth ili basi uweke image kwamba CCM inazidiwa. Nyie Chadema hamko serious. Huyu mdau anapindisha hadi ukweli wa gazeti. This is pathetic.
 
Back
Top Bottom