Kinachosababisha foleni Kimara Korogwe ni wavuka barabara wanaoshuka mwendokasi

Hata wangeweka wabobgo wasingeitumia hilo daraja la juu kimara tuu watu wanapita kule chini nondo zilikochomoka
Daraja linamizunguko mingi mno tofauti na underground hiyo ni straight forward. Hebu fikiria njia nane zile na mwendokasi katikati toka kimara hadi kibaha balaa lake kwa wavuka kwa miguu. Alafu uweke mataa tena kwa ajili ya wavuka kwa miguu unasababisha foleni kubwa. Sasa kungekuwa na underground mtu akae kusubiri mataa wakati underground iko wazi masaa yote.
 
Kwanza pale abiria wengi wanaovuka Ni kutoka kwenye mwendokasi ambao wengi wao wanashuka ili kupanda bajaji na daladala za mbezi kwa urahisi wawahi kufika,pili wakazi wengi wanaoishi karibu na kimara mwisho wanashuka pale ili kuepuka panda shuka daraja la kimara mwisho....
Serikali miezi michache iliyopita ilikuwa inataka kuzivunja nyumba kuanzia bucha Hadi kimara mwisho na zimeshawekwa X sijajua kizunguzungu kinatoka wapi?
Pale serikali ikiamua hakuna foleni haitatokea ni suala la miundombinu tu.


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Pia unaweza kufanyika uamuzi mwingine mgumu wa kuvirudisha vituo vya dala dala vilipokuwa zamani maeneo ya "Resort" pande zote mbili na hapo Korogwe ikabaki kuwa kituo cha mwendo kasi tu. Lakini kikubwa kwanza kuondoa machinga kwenye njia za waenda kwa miguu kwani ndio tatizo kubwa linasababisha watu kupita barabarani hivyo kwa kiasi kikubwa kupunguza kasi ya magari kutembea.

Na kwa Kimara mwisho ni lazima vituo vya dala dala vijengwe vipya kabla au baada ya kituo cha mwendokasi yaani visiwe samba samba na kituo cha mwendokasi. Vile vituo vilivyopo sasa Kimara mwisho ni vidogo mno na vimejengwa kwa ajili ya kushushia na kupakia abiria tu lakini sasa hivi dala dala zinapiga kambi kabisa ndio matokeo yake haya foleni.
 
Back
Top Bottom