JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 2,091
- 4,716
Hivi vituo vya mwendokasi ujenzi wake umekosewa tangu mwanzo kutokana na kukosekana ushirikishwaji wa mawazo ya wananchi, wenye akili wachache wamekaa wakaamua kujenga walichojenga mwisho wa siku foleni limekuwa balaa na janga kwa watumiaji wa barabara.
Hivi vituo vya mwendokasi vilitakiwa vijengwe na underground tunnels kwa wavuka kwa miguu ili mtu akiwa ndani ya kituo basi anashuka ngazi na kuingia underground na kuvuka upande anaoenda.
Mainjinia wangeweza kuweka miundombinu hii tena ni cheap kuliko madaraja kama ya Kimara ambayo ni expensive na yanapoteza muda sana kwa wavukaji.
Hizi underground tunnels zingetumia makaravati ya mita tatu ambayo ni gharama nafuu kuliko kujenga madaraja hivyo kuondoa kero ya foleni.
Hata huu ujenzi wa njia nane morogoro road ukikamilika uvukaji wa watembea kwa miguu utasababisha foleni zisizo za msingi kila kwenye mataaa.
Ingekuwa bora kama hawa wabunifu wangeweka underground pedestrian crossing ili wavukaji wasiingiliane na magari kwa sababu njia nane na mwendokasi katikati ni hatari mno kwa wavukaji kwa miguu pia ni kupoteza muda kuweka mataa kwa ajili ya wavuka kwa miguu wakati kungekuwa na underground tunnels za wavuka kwa miguu kusingekuwa na usumbufu wa maingiliano wa magari na wapita njia kwa miguu.
Pia hizi underground tunnels zingeweza kutumika kuingizia kipato cha jiji kwa kuweka mabango kwenye kuta za tunnels kwa matangazo ya biashara kwa kuwa wavukaji ni wengi ambazo pia zingeingiza pesa za kulipia bili za umeme kwa taa za ndani ya tunnels na hata air condition ingewezekana pia vingewekwa hata vibanda vya wafanya biashara pia kulingana na design ya tunnels.