Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 123,252
- 98,255
Pasco
Ni lini hivyo vyombo ulivyovitaja vilitangaza wazi kuwa sehemu ya Vyama tajwa. Mathalani sijasikia wakati wowote StarTV and RFA wakisema wao ni sehemu ya CCM, ni kwa nini ITV, Radio one na magazeti yao watangaze hivyo? Binafsi ninafikiri katika vyombo vya habari vilivyotenda haki katika uchaguzi huu ni vyombo vya IPP. Pamoja na kwamba unaweza kuhisi kuwa wanapendelea upinzani (kwa sababu tu ni nadra hapa kwetu kuona chombo cha habari wakiwapa wapinzani nafasi kama chama tawala), lakini kiukweli walifanya kama inavyotakiwa katika nchi ya kidemokrasia!
Mkuu huyo alishapumbazwa kuwa ccm ni kila kitu na hajui kuwa sasa tupo ndani ya mfumo wa vyama vingi vya siasa