Ghana wapo mbali sana kwenye mambo ya demokrasia. Hata Malawi hapo karibu tu. Uchaguzi uliopita, Rais alikuwa akigombea tena huku Makamu wake akiwa anamchallenge urais kupitia chama kingine?
Tanzania bado safari ni ndefu
Hata hapa mbona tunajichanganya kidogo tu na hivi vyama bado havijajipanga sawasawa. Mbona hata hapa Waziri wa Mambo ya nje wa Zamani na kachero mbobezi BC Membe alimchallenge rais aliyekuwa Madarakani kupitia Chama pinzani.
Yaani ipo hivi, hivi vyama havijajipanga kufanya siasa za ushindani na chama tawala zaidi ya kuigeuza siasa kuwa ni kitega uchumi chao. Wanasubiri CCM ikosee na wao wawe ndio wanenaji wa kuwapelekea taarifa wananchi na kutia chumvi. Wanasubiri CCM wagombane na kufarakana wao wapate mwanya wa kushinda. CCM imara ina maana upinzani hauna cha kuwaeleza wananchi na ndicho kilitokea kipindi hiki cha kampeni.
Upinzani unatakiwa kujua matatizo yanayokabili wananchi na kuyatafsiri katika sera, sera zinazotatua kero za wananchi. Kipindi cha Slaa alifanikiwa sana katika hili. Angalia ujenzi wa miundo mbinu kama SGR na Elimu bure. Vyote viliasisiwa na Chadema ya katibu mkuu Slaa. Hebu niambie, toka Slaa ameondoka Chadema kuna nini kipya katika sera. Uchaguzi huu tumemsikia mgombea akidai UHURU, HAKI NA MAENDELEO. Hivi kweli mwananchi aliyepo mashambani huko Katurukila au Mbingu nabTanganyika Masagati atakuelewa unapomwambia mambo hayo? Yeye akiamka asubuhi ana uhuru wa kufanya mambo yake yote na haki ya kufanya lolote hata kuoa wake 20. Hii sio issue kwa mTanzania mpiga wa kawaida. Lakini wenzenu wanapeleka Zahanati kila kata na madawa tele, Elimu bure, maji, na barabara wananchi wanaona mafuso yanaingia maeneo yao kubeba ndizi na machungwa wanapata pesa, leo wewe unawagubiria Haki, uhuru na maendeleo, Umerukwa na akili???
Hivi vyama vijitafakari. Vimepotea na vimepoteza mwelekeo.
Wanabaki kulalamika wamenyimwa ruhusa ya mikutano. Hivi....
1. Nani kakataza mikutano ya ndani?
2. Kwanini havifanyi mikutano ya ndani
3. Mikutano ya hadhara ni ya watekeleza sera waliochaguliwa na wananchi
4. Kila mtu akiruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara nchi bado itakuwa kama vile ipo kwenye kampeni, mtekeleza sera aliyehaguliwa anaelekeza hili, mpinzani naye anapinga anataka lifanyike analowaza yeye. Huu ni ujinga na kama nchi huru maendeleo hayatafikiwa.
5. Kuimarisha chama na mikakati ya chama mikutano ya ndani ya kimkakati ikifanyila hakuna shida.
Kwa ujumla upinzania umepotea toka enzi za Slaa sijaona ten mwelekeo wa chama chenye utashi wa kutwaa dola. Kilichopo ni sanaa tu.