Ngho
Senior Member
- Jun 2, 2015
- 121
- 189
Baada ya kifo cha mpendwa wetu takriban mwezi mmoja sasa kumetokea na sintomfahamu kubwa BUNGENI miongoni mwa MPs, hali ambayo sio AFYA kwa taifa letu. Tukumbuke kuwa hili ni Bunge la budget, lakini anasimama mbunge wa jimbo fulani kuchangia Hotuba ya wizara husika lakini hoja inajikita katika malumbano ya kifikra juu ya Marehemu.
Kuna ambao wanataka Marehemu aenziwe kama mwenyewe alivyotaka yaani 'Special Recognition'. Hawa wanataka Bunge liwe na azimio la pamoja katika kuenzi yote ambayo yameachwa na Marehemu, hawa mwalimu wangu anawaita Protagonist.
Na kuna wengine ambao wanakubali kuwa aenziwe ila Legacy ijipambanue kama ile ya watangulizi wake kuanzia kwa Mwl Nyerere katika harakati zake za ukombozi wa Nchi na Bara kwa ujumla na mengine mengi ambayo tunayasikia, Mzee mwinyi kama tulivyoishi katika nyakati zake mpaka akawa nominated kama Mzee Ruksa, Mr Ben ambaye Mzee wa msoga alimuelezea kama master plan wa malengo yanayotekelezwa kwa awamu hizi nne kuanzia na mzee wa Lupaso mwenyewe, pia tuna Mzee wa msoga mwenyewe ambaye kila mtu anamjua na anaelezwa vyovyot na yeyote KUTOKANA na aliyoyafanya, tena tuna Marehemu ambaye kwa bahati mbaya au kwa mapenzi ya Mungu ameshindwa kumaliza terms mbili za utawala wake. Hili kundi la pili linataka Legacy ya mtu isilazimishwe kwa watu KUAMINI kuwa the man was superb than his formers bali wanasisitiza waache mambo yajieleze na wanaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa Mzee wa Chato amefanya mambo mengi, yamo yanayofaa kuendelezwa, kuondolewa na vile vile Mama ambaye ni mrithi wake anaweza KUBUNI kadri anavyoona inafaa.
Mtazamo wangu, kwenye Bunge hili la 12 limebeba wabunge wa kila aina kama tutakuwa na kumbukumbu tunajua mchakato ulivyokuwa kuanzia kwenye chama mpaka kwenye Ballot box. Kuna WALE ambao walibebwa na mfumo moja kwa moja yaani UNEXPECTED to enter the house, na wale ambao wana uwezo pasipo kuwa na mfumo ambao ulitumika. Changamoto ambayo inalikumba kundi la kwanza ni kuwa mfumo uliwabeba hivyo wanamshawishi mama afuate nyayo za mtangulizi wake ili wanufaike moja kwa moja na aina ya siasa ambazo zilitumika,KUMBUKA katika hili kundi kuna watu waliokotwa majalalani na kuletwa kwenye siasa, na kundi la pili linaona wao kama wao wanaweza kujipambanua wao wenyewe kadri iwavyo KUTOKANA na uwezo wao, the FUTURE is on their own, hawa ni pure politicians.