kina mama nawaulizeni.........

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Mara kwa mara nasikia mnasema 'kuolewa ni bahati',hivi mnamaanisha nini hasa?
 
Kwa miaka hii, kwa mtazamo wangu at least,
mitazamo yetu ya kujiweza, kutokuogopa maisha, kutikutishiwa na maneno ya maisha magumu ukiwa peke yako, mifano mingi ya wanawake wanaoshi kwa raha bila ndoa.
Msichana anapojaliwa wazo la kujinyenyekeza, kukubali kuitwa mke, kukubali kushare, kurisk personality yake,
anapopata kijana
anayeona maisha ya ndoa yalivyo ya kushangaza, mifano mibaya, matisho ya kuripoteza uhuru. Kazi nyingi hakuna muda wa kupumzika.
Inaweza kutokea wakakutana wawili hawa, katika umati wa watu, kumbe wanaweza kuongea na kumbe wanaweza kufikia maamuzi na kumbe eti, wasimama mbele ya wazazi na kuapa kuwa pamoja na yote, watakaa pamoja kama mke na mume.

Ni bahati kubwa sana, almost a miracle!!!
Ila muujiza mkubwa ni ule wa kuishi pamoja baada ya ndoa, inawezekanaje???
You can ask me that
 
My point is,huku kwetu uswazi mwanamke akipata mwenza halo halo zinakuwanyingi...'mlisema haolewi mbona kaolewa' na khanga zinaandaliwa zenye mafumbo,ndo nauliza swali hilo hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
...haswa kwa miaka hii kweli hawana budi kusema ivo. kwanza idadi ya wadada unaoweza kusema ni "wife material" imeshuka sana, pili umakini wa wanaume kutaka mke bora na wakusaidiana kimaisha umekua juu sana!...(kiufupi tumepanda bei gafla...lmao!)
 
Mimi nisiyekua na mpango wa kuolewa ntasemaje kuolewa ni bahati??maisha ya bahati nasibu waliyaweza babu na bibi yangu..
 
We Lizzy alokuleta kwenye uzi wangu nani?
Kwanza nasikia AR kuna baridi sana,embu rudi kwenye blanketi,ila niitie Kongosho na sweetlady waje hapa watoe maelezo maana kila kukicha wanapiga talalila humu kuwa kuolewa ni bahati,waseme kivipi.
Bishanga hapa nilipo nimefunikwa na mikono miwili ya ukweli kwahiyo ondoa shaka. Kweli kuolewa sio bahati, bahati kupata mwanaume wa maana.

Waja. . .
 
Last edited by a moderator:
Bishanga hapa nilipo nimefunikwa na mikono miwili ya ukweli kwahiyo ondoa shaka. Kweli kuolewa sio bahati, bahati kupata mwanaume wa maana.

Waja. . .

uko sawa kabisa Lizzy..
Kuolewa sio bahati jamani bahati ni kumpata atakayekupenda kwa dhati,kukuheshimu,kukuthamini na kukujali...
Watu wanaolewa daily lakini wanayokumbana nayo huko ndoani only God knows!
Ingekua kuolewa ni bahati ndoa zisingevunjika..
 
Last edited by a moderator:
Nilivyomuelewa muanzisha mada ni kuwa Kuolewa ni bahati kwani unakuwa umeweka historia kwamba once uliwahi kuolewa kwani ni wachache ambao hubahatika kufikia hiyo hatua katika maisha na swala la kuwa hakuna maana yoyote iwapo aliyekuoa ana kujali au la havina uhusiano na hiyo mada.
 
it's complicated I guess.

Kuolewa si bahati, bahati kumpata mwenza wa kaliba unayoitaka.
Unaweza jikuta umezungukwa na akina karum.ekenge tu.
 
...haswa kwa miaka hii kweli hawana budi kusema ivo. kwanza idadi ya wadada unaoweza kusema ni "wife material" imeshuka sana, pili umakini wa wanaume kutaka mke bora na wakusaidiana kimaisha umekua juu sana!...(kiufupi tumepanda bei gafla...lmao!)
subiri Rose1980 aje ndo utalijua jiji mi simo.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nisiyekua na mpango wa kuolewa ntasemaje kuolewa ni bahati??maisha ya bahati nasibu waliyaweza babu na bibi yangu..
sasa Purple utaishije bila mme mji huu,na ham ya kudo unaikabili vipi bila mwenza,au ndo yale ya Darlingtone na @serafina ?
 
Last edited by a moderator:
Bishanga hapa nilipo nimefunikwa na mikono miwili ya ukweli kwahiyo ondoa shaka. Kweli kuolewa sio bahati, bahati kupata mwanaume wa maana.

Waja. . .
kwa hiyo huyo mwanaume wa maana hata asipokuoa we poa tu?
 
Nilivyomuelewa muanzisha mada ni kuwa Kuolewa ni bahati kwani unakuwa umeweka historia kwamba once uliwahi kuolewa kwani ni wachache ambao hubahatika kufikia hiyo hatua katika maisha na swala la kuwa hakuna maana yoyote iwapo aliyekuoa ana kujali au la havina uhusiano na hiyo mada.
swadakta!
 
Back
Top Bottom