Kina Mama, Mmeajiri hausi geli au mke mbadala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kina Mama, Mmeajiri hausi geli au mke mbadala?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by muhosni, Feb 20, 2011.

 1. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kina Mama Mmeajiri hausi geli au Mke Mbadala?

  Ebo! Kwa masihara mliyoyaibua zama hizi akina mama naapa mmeliwa! Wapo mamaza mnaoonyoosha miguu juu kabisa mkishapata hausi geli. Mnawachukulia ni wakombozi wenu eti? Naapa mmepotea!

  Enyi wana wa nguo za kike! Kama mlidhani mmepata hesabuni mmepatikana! Nimegundua kuwa "my wife" wetu mnakoelekea ni kurejesha utumwa kwa mlango wa uani. Mkome! Mnalea tabia za Kisultani?

  Kwanza hampo makini kuhusu ni majukumu gani myakasimu kwa ma hausi geli na ni yapi myang'ang'anie. Kaeni chonjo, ma hausi geli wamewapiku kiulaini, japo kuwa si washindani wenu, mnawapapatikia hawa mabinti kana kwamba kuwa nao ni fasheni? Ninyi mtabakia kwenye kupika nywele, "panel beating" ya nyuso na kufuga kucha. Na hapa ma hausi geli watawafanyia mapinduzi bila kumwaga damu.

  Ewe mama huna hata soni! Hausi geli akutandikie kitanda, "master bedroom", bado upone? Ashonee vishikizo suruali za mumeo bado upo hai? Amnawishe maji na kumlisha, eti wewe uko bize na mitindo ya nywele zako.

  Lengo ni ili nywele hizo ziwe za kizungu, kihindi, au kigoha? Mapambano yako ni kuachana na nywele zako za upilipili na hii rangi nyeusi uliyojaliwa na Mungu? Hizo si ndo origino kwako? Utakula jeuri yako!

  Kwani kazi za hausi geli zinabadilika badilika kutokana na mudi ya maza? Mara amwandalie mumeo maji bafuni, amkamue jipu au kumkata kucha. Hapa unajisukia msiba wa kujitakia!

  Mumeo kaja baada ya usiku wa manane, binti ndani ya kanga yake moja ya India anaamka kwenda kumpakulia pilau. Yaishie huko tu, wakati kaanza kujua "make-up"?

  Eti wewe mwanamama, samahani mama Mudi. Eti cha mno umechoka kwani ulikuwa mwanakamati kwenye "kitchen party"? Iwe "Kitchen Party" au "Chichen Party" ndo mumeo uliyeampa kumtunza?

  Elezeni ni kazi ya hausi geli kumpakulia mumeo? Wewe mama, mipaka ya hausi geli ni ipi? Je mumeo anaijua? Una hakika mmeijadili pamoja? Wenzenu "Day one" tu huwa wameshakamilisha "job description".

  Nayo itasaidia nini hiyo, iwapo baada ya si9ku chache haiheshimiki tena? Kama tamaa yenu inawatuma hausi geli akuuzie vitumbua, au alime matuta ya matembele ndo mtegemee nini?

  Wengine huanzia na jukumu la kulea mtoto. Haijalishi hausi geli mwenyewe kamaliza shule, au anamlea mtoto mwenzake. Ni haki ma hausi geli wajue wao ni nani na hatima zao ndo zipi? Huko pa uyaya sipaelewi; ila ni pamoja na kumwogesha mtoto, kumbadili nepi, kumbembeleza, kumpikia na kumlisha. Aidha, ni pamoja na kuandamana na mamaye popote aendapo ziara binafsi.

  Wapo baadhi kwenye ujasiriamali kukuza kipato. Watauza karanga, maji, vitafunwa, mbogamboga, barafu, na kila ghasia. Pia, watatumwa kwa wifi kutwanga kisanvu. Si ni njaa yenu?

  Wapo wanaoajiriwa kwa kazi za jiko tu. Watawapikia watoto wa shule, milo ya familia. Kuosha vyombo, kupakua, kupanga meza, n.k. Hawa na kama paka si lazima wajue sokoni.

  Uhausi geli kijumla ni "general slavery". Anachukua majukumu yako, mkeo, wanao, na kadhalika? Ndiye anayeratibu hadi siku za kliniki kwa mtoto. Huna aibu! Hata mtoto wako akiota meno ni hausi geli ajuaye?

  Mama mzima waruhusu hausi geli awe "personal assistant" wenu wa kukumbusha hiki na kile. Toba! Mtoto wa watu ni mhasibu wa familia, mlinzi wa nyumba, dobi, na mtu wa itifaki kwa wageni wenu waingiao kwa makumi toka kijijini kwenu.

  My God! Si hayo tu! Hausi geli ndo wa kuwapangia mle nini leo, huku mliapa siku ya harusi kuwa mkeo atahusika na hayo ya huduma kwako. Wewe mama, wafanya nini hadi kukasimu madaraka kiasi hiki? Mmemfanya "mama mdogo".

  Yangeishia basi hapo, lakini muda wowote utakapo kuelekea kwenye kutafuta mkate hausi gel indo hukukabidhi mkoba na orodha ya mahitaji ya wiki. Haya nayo si ya mama mwenye nyumba?

  Nisisahau, ni hao hao ma hausi geli mnaowatumia kwenda kumpitia "baba" ofisini ili wapitie sokoni kununua mahitaji. Yangeishia basi hapo! Ni kazi ya hao mabinti kuyatunza na kufuatilia mahitaji kifupi "storekeeper".

  Pamoja na hilo, hawa ni "housekeeper" waliotukuka. Wamemkasimu "mama watoto" katika kadha wa kadhaa za nyumbani na mara nyingine hata kwenu. Mtume! Hata na bustani ndogondogo huhusika mpatapo bamia kidogo.

  Ewe mama! Kama yamefika huko na hujamkabidhi hausi geli uke wenza ni dhuluma ya wazi. Hiyo ndo pensheni pekee, ikichukuliwa wengi hulipwa elfu selasini kwa mwezi. Msingojee ya Tunisia!

  Je, haya mambo yangekuwa yanakwenda kwa zamu ungevumilia na bintiyo yamfike hayo?
  Acheni hizo!
  Chanzo: Papaa Mawani (Mwashangaa nini?)
  Gazeti la Mwananchi Jumapili 20 February 2011, ukurasa wa 11
   
 2. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Duh hapa kanena ukweli mtupu ila inapotokea wife kawahi kutoka kaniacha nimelala then anakuja house girl asubuh saa 12 na kanga 1 ya india kufanya usafi hafanyiwi kosa maana muda huo inakuwa na nguvu sana isitoshe tunakuwa hatuna akili vzuri tunaishia kupeana tamu!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kweli tupu
   
 4. LD

  LD JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi unapofanya hivo unamkomoa nani?? Huyo ubavu wako au huyo mtoto wa watu?? Mimi hapa nazishangaa tena akili za wanaume, sitaki sana kusema wote coz najua Mungu ana watu wake waadilifu wakiwemo wanaume.

  Fikiria huyo house girl ni binti yako anafanyiwa hivo na 'libaba' lenye nyumba fulani hivi?
  Unajua hii dunia ni tambara bovu, mshukuru Mungu kwa sababu uko hivyo ulivyo leo, lakini hujui kesho yako/yetu itakuwa je. Huyo binti yako anaweza akatokea akawa house girl mahali vile vile no matter what? Hii ni dunia, hebu chukulia tukio la Mbagala/G.Mboto. Kama kabinti fulani kalipona lakini baba/mama wakaondoka wote, hata kama walikuwa matajiri kiasi gani, je binti huyu anaweza akajua hata kama baba yake alikuwa na sh. Ngapi benk? Let say ni binti wa miaka kumi hivi. Kama Mungu hatafungua milango na kuinua watu kwa ajili yake hakuna uwezakano wa mtoto huyu kupoteza mtiririko wa maisha aliyokuwa analelewa na wazazi wake na hata kupelekea siku moja awe housegirl kwa mtu??

  Kina baba wapendwa fikirieni kabla ya kutenda, kumharibu mtoto wa watu kisaikologia na kumfanya awe mtumwa wa kazi na ngono sio fimbo ya kumchapia ubavu wako ulio na kasoro. Waoneeni huruma hawa mabinti jamani, wanafanya mengi kwa ajili yetu, jalini utu wao. Wakati mwingine maisha ya watoto wetu na sisi wenyewe yanakuaga mikononi mwao, kwa sababu wanaweza kufanya lolote wawapo majumbani mwetu. Jamani wapo mabinti wanaofanya vizuri sana mpaka unamuoenea huruma unatamani angekuwa mahali fulani. Wapendeni upendo wa kimungu jamani. Daaa hebu fikirieni unamlipa huyu binti labda elfu 30 au 20 kwa kazi ngumu kwa mwenzi mmoja. Lakini wewe matumizi yako ya siku moja tu na hapo ni starehe ni zaidi hata ya laki moja. Kwa nini tunawabebesha na adhabu nyingine wasiostahili!!

  Daa Eeee Mungu walinde binti zetu!!!
   
 5. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa hapo ina maana mama asiwe anakuacha peke yako ndani ya nyu
  nyumba au itakuwaje. Au akutengenezee kufuli afunge kila akikuacha home
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  POint zimejaa kwenye mada..ila najaribu kwenda mbali zaidi kifikra.... siyo kila mtu anaweka hausgeli...
  je wenye kuwa na mijibaba kuangalia nyumba na kufanya kazi inakuwaje..maana majukumu hayatofautiani!
  Je inabidi baba mwenye nyumba ajisikie kuna upinzani na hivyo awe mwema zaidi kwa mkewe au inakuwaje?
   
 7. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  LD, pole mama. Narudia kusema tena, not even God is ripe enough!
   
 8. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Haya tupanue wigo pia. Wadogo wa kike wa wake zetu nao wako salama kwenye kila nyumba wanazoishi na shemeji zao?
   
 9. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tamaa tu za kina baba hawa. Kama nafanya kazi atakuwepo tu na atafanya majukumu yake kama kawaida alale nae au asilale nae. Kwani sie tunawauliza wanapotuacha home na walinzi na mashamba boy wao wanarudi saa nane za usiku na sie tunaruhusiwa kuwaza kama wao na kutembea na walinzi? Na nyumba zingine zina mahouseboy pia wanawake nao wakifikiri the other way???
  Huyo mwandishi ameongea utafikiri wale makungwi wa kitchen party bila kufikiria upande wa pili wa shilingi penye housegirl panaweza kuwa na houseboy vilevile na mambo yakawa vilevile.Na hiyo ni adha tu ya wanaume wengine kujihalalishia umalaya wao.
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ukiangalia kwa makini basiutasema kila mwanamke yuko hatarini kwa mwanaume! umezungumzia wadogo wa kike.... hata dada na mabinti! sasa hii dunia inaelekea wapi? Nyie wanaume hivyo vitu mnavykula huko... punguzeni maana vinawapeleka pabaya.Kwani ni lazima humo ndani? Si mtafute nje ya nyumbani au ndo mambo ya ku keep it within the family???
   
 11. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gaga, nadhani mwandishi alihitaji kwa focussed bila kuchambua kila mtu. Hata hivyo hausi geli ndo popular phenomenon zaidi kuliko hausi boi
   
 12. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mama gaude wangu umesikia mistari hii sio tuoane uanze ooh huku osdorp baridi ngoja tulete house girl wa kimatumbi utamkamatia delft shauri zako.mi ngoja nkapige box
   
 13. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sikuwezi,siku ukikamatwa,sijui....l.o.l:rain:
   
 14. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Watu wametoka nje ya mada tatizo kwa nn wakina mama mnawaachia mahouse girl majukumu yenu?
   
 15. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kwanza kuna change ya lifesytle jamani,si rahisi sisi kufanya majukumu yote kwa asilimia 100%,japokuwa nakubali kuwa kina mama sasa wamekuwa wazembe mno,yaani A-Z afanye housegal,ambacho haruhusiwi labda ni kulala na mumeo.....its not right,najua sasa wengi wetu tuko busy makazini,na hayo mafoleni tunashindwa kutimiza baadhi ya wajibu lakini tujitahidi.....la sivyo tutakuwa tunaajiri wake wenza in the shadow of house gals.......wanaume nanyi mjitahidi kutusaidia majukumu si kukaa tu kama miungu watu......
   
 16. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu nyie mmewaachia wakina mama majukumu yenu hadi yakawazidia..nao wanawaachia mahausglz! Mkichukua yale yenu basi na siye tutabeba yale yetu.

  Akina baba mnajidekeza sana ..mlioa mke au mliajiri mfanyakazi? Kama ni mke basi kazi zake sizo hizo mnazotaka wafanye. Mke ni mwenza na siyo mjakazi. Ukiweza na wewe kusaidia hata na huyo masichana wa kazi atakuwa na kazi kidogo. Unataka nitafute kipato hapohapo unataka nifanya kazi zote kama vile meiye ni mtumwa wako? Nilikuja kuolewa babu ehhhh.. sikuja kukutumikia!
   
 17. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Na aliyekwambia kutandika kitanda ni jukumu la mke tu ni nani? wewe umeamka wa mwisho kwa nini usitandike kitanda, umeoga wa mwisho kwa nini usikaushe maji bafuni? wenzetu nchi za magharibi wameweza kukaa bila mahg sababu wanasaidiana majukumu ya kazi za ndani na waume zao sio hapa baba kakaa sebuleni anasubiri kila kitu hata ukitenga chakula bila pilipili atakusimamisha ukalete kwenye fridge na hapo umefanya kazi zote na ukizingatia mmerudi wote kutoka kazini. mnafikiri sie marobot? halafu hapo bado umefika kitandani umechoka anaanza kukuchomachoma na dudu lake eti limesimama
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Hakuna kosa baya linaloweza kudhalilisha familia kama baba mwenye nyumba kulala na housegirl... DHARAU NA DHIHAKA ZA HUMO NDANI HAZIISHII KWENYE NYUMBA TU

  NI AIBU SANA WAKUU
   
 19. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mie nashangaa kwa nini housegirl akilemewa na majukumu ya kazi lawama zinatupiwa kwa mama tu???wababa hawahusiki katika kusaidia kupika,kuosha vyombo etc???? sio lazima housegirl asaidiwe na mama tu hata baba anaweza kusaidia akiona kazi ni nyingi........
  halafu mpk utembee na mtu,ni awe amekuvutia kiumbo nk,sioni HOW mtu anavyofanya kazi za nyumbani zaidi ndio wewe unahamasika kutenda naye ngono?! utakuwa na matatizo ya akili......
  by the way yeyote anayetembea na housegirl haheshimu hio institution ya ndoa...and he didnt deserve to get married in the first place!!!!:A S 13::A S 13:
   
 20. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waambiye wanaume wenzio kaka maana wamezidi sana.Post kama hii ni kithibitisho tosha cha uchafu unaoendelea kwenye nyumba za watu.

  Wakina mama wengi sana wanajua kinachoendelea na wengine hujikausha kama hawajui ili maisha yaende hasa pale familia ina watoto wadogo.Kuna mama mmoja yeye alikuwa anawaacha watoto na majirani anaenda kazini akirudi ndio anachukua wanaye. Akaulizwa mbona huweki msaidizi akuangalie wanao unadiriki kuwaacha kwa majirani - hadi lini? Alichojibu kilishangaza na kuwaacha watu midomo wazi.Ati mumewe alikuwa anabaka wafanyakazi. Alishabaka wafanyakazi watano! hapo wanaye walikuwa wana miaka 6 na 4 msichana na mvulana. Wenziwe walichomshauri ni kuwa, unahatarisha maisha ya wanao.Weka mfanyakazi na mwache aendelee kutembea nao mradi hakikisha siyo wasichana under age! LOH! PATENI PICHA!
  MBABA KAMA UNATAKA MWANAMKE TOKA NJE!UNADHALILISHA WANAO!
   
Loading...