Kina dada kuweni makini na maamuzi

Anyisile Obheli

JF-Expert Member
Dec 13, 2009
3,398
319
Kuna dada mmoja ambaye alipata Mimba kabla ya kuolewa, na baada ya kujifungua akaamua kuchimba shimo na kumfukia mwanae hadi shingoni, lakini Mungu si juma wala george, wapita njia wakakikuta kitoto kimefukiwa hadi shingoni, wakaamua kukitoa, na kufanya msako wa nani alikuwa mjamzito katika eneo lao,

wakakumbuka kuwa ni yule dada X lakini mbona mimba hana tena? wakaazimia kumbana
mpaka alipokubali kuwa ni yeye na ameamua kufanya hivyo kwa vile mzazi mwenziye hamtunzi, akakabidhiwa kile kichanga akilee chini ya usalama,

mara baada ya miwili alipata bahati ya kuolewa lakini akawa hashiki mimba tena baada ya kuonana na ma Dr. akaambiwa hana uzazi tena, ikabidi aongeze mapenzi kwa yule mwanae
ambaye aliwahi kumfukia, lakini la Mungu halipingikia yule mtoto naye akafa kwa kansa ya damu

Sasa huyo dada amebaki na majuto,

*****kuweni makini kina dada na maamuzi ya ufahamu na akili zenu******
 
Inasikitisha sana kweli mtoto uliyemtoa tumboni mwako unaenda kumfukia looh mungu apishe mbali.
Thanks kaka Anyisile
 
kama una ukaribu naye mwambie asijali kuna watoto wengi kwenye vituo vya watoto yatima na wa mitaani; anaweza kumchukua mtoto mmoja au zaidi kwa kufuata taratibu za kisheria na kurejesha furaha katika ndoa yao.
 
Inasikitisha sana kweli mtoto uliyemtoa tumboni mwako unaenda kumfukia looh mungu apishe mbali.
Thanks kaka Anyisile
yaani we acha tu FL1, tatizo kuweka tumaini kwa mtu, tena unaweza ukute ni wachache waliolelewa kwa mapenzi ya wazazi wote wawili katika kila watoto mia ukute ni 30 tu,
 
Back
Top Bottom