Kimya kinachouma

Kimya kinachouma

Kwa sasa napitia kipindi kigumu sana, na afya nayo hainiruhusu kuwa sawa kabisa.

Shida kubwa afya maradhi ni mengi ila naomba iwe siri angu Kwanza...

Mengine nabaki nayo moyoni. Mwenyezi Mungu awabariki wote watakaogusa maisha yangu kwa wema. 🤲
 
Sijui kama ni uchovu, presha ya maisha au mambo yamezidi tu…

Kwa siku hizi najikuta niko kimya sana. Kuna mambo napitia ambayo si rahisi kuyaeleza kwa mtu, na ukweli ni kwamba nimefika sehemu najihisi nimeelemewa sana.

Sina nia ya kulalamika wala kutafuta huruma. Nimejaribu kujishikilia na kutafuta njia ya kutoka, lakini kuna wakati nguvu zinapungua.

Kuna jambo dogo tu nikilipata linaweza kunisaidia kuvuka hii hatua, lakini sitaki kulazimisha mtu. Mwenye kuona anaweza kunisogeza hatua moja mbele, nitathamini msaada wake sana.

Wakati mwingine mtu anayekaa kimya si kwamba hana shida… anaweza kuwa anapigana vita ambayo hakuna anayoiwona.

Mungu anipe nguvu nivuke kipindi hiki. 🤲
Usiogope Mungu amekuumbia nguvu ndani yako na utashinda vita uliyonayo tupo wenye hali pengine kama yako ila Mungu anatupigania ,ila kwa sasa wengi wetu hata usingizi tuu kuupata ni shida jamii yetu inakumbwa na janga lakukata tamaa pamoja na migogoro ya nafsi kikubwa tuzidi kumtumainia Mungu ,wakati mwingine kupata mwenye changamoto zinazoelekeana ni rahisi kuelewa unakopita.
Naamini kesho yako itakuwa bora zaidi ya leo Mungu aishiye milele akutie Nguvu
 
Ukimya mara nyingi huficha mambo mengi mazito, na maneno yako yana hekima kubwa inayofunua uhalisia wa maisha ya watu wengi.

Mara nyingi, mtu anayepitia changamoto kubwa za kisaikolojia, kihisia, au kimaisha huchagua kukaa kimya si kwa sababu hana shida, bali kwa sababu ya kutotaka kuwa mzigo kwa wengine, kukosa maneno sahihi ya kuelezea maumivu yake, au hata hofu ya kuhukumiwa na jamii.

Ujumbe huu ni ukumbusho mzuri sana kwetu sote kuwa wenye upendo, subira, na fadhili kwa kila mtu, kwani hatuwezi kujua ni vita vya namna gani mtu anapigana navyo kwa ndani nyuma ya tabasamu au ukimya wake.
 
NAOMBA MNISAIDIE TAFADHALI NIKIWAA SAWA NITAWAAMBIA TYU MARADHI YANAYONISUMBUA NAPITIA CHANGAMOTO JAMAN DAH....
 
Usiogope Mungu amekuumbia nguvu ndani yako na utashinda vita uliyonayo tupo wenye hali pengine kama yako ila Mungu anatupigania ,ila kwa sasa wengi wetu hata usingizi tuu kuupata ni shida jamii yetu inakumbwa na janga lakukata tamaa pamoja na migogoro ya nafsi kikubwa tuzidi kumtumainia Mungu ,wakati mwingine kupata mwenye changamoto zinazoelekeana ni rahisi kuelewa unakopita.
Naamini kesho yako itakuwa bora zaidi ya leo Mungu aishiye milele akutie Nguvu
Suffering today doesn't mean u will be fine tomorrow no...u may suffer until you die
 
Ukimya mara nyingi huficha mambo mengi mazito, na maneno yako yana hekima kubwa inayofunua uhalisia wa maisha ya watu wengi.

Mara nyingi, mtu anayepitia changamoto kubwa za kisaikolojia, kihisia, au kimaisha huchagua kukaa kimya si kwa sababu hana shida, bali kwa sababu ya kutotaka kuwa mzigo kwa wengine, kukosa maneno sahihi ya kuelezea maumivu yake, au hata hofu ya kuhukumiwa na jamii.

Ujumbe huu ni ukumbusho mzuri sana kwetu sote kuwa wenye upendo, subira, na fadhili kwa kila mtu, kwani hatuwezi kujua ni vita vya namna gani mtu anapigana navyo kwa ndani nyuma ya tabasamu au ukimya wake.

Sina La Zaidi Kaka MshanaJr 🙏🙏🤟
 
Back
Top Bottom