Cavill
JF-Expert Member
- Nov 12, 2019
- 443
- 1,565
Matabaka hayajawahi kumuacha Binadamu Salama.. Sasa tukimalizana na Makafri Dunia nzima kumbe kuna uwezekano tukaliendeleza sisi kwa sisi eeeh..
Kabla hujamuona mwenzio sio mkamilifu ama kumkosoa kwa lolote lile hebu jihakikishe wewe kwanza kama umekamilika ipasavyo. Ila Nikutahadharishe tu kwamba ukiamua kujikosoa wewe kwanza hutakua na muda wa kuhangaika na wengine maana hakuna kilicho kikamilifu chini ya jua..
Kikubwa ni kuheshimu tofauti tulizonazo na kubadili mitazamo ya wengine kwa kugeuka kuwa mifano mizuri mbele ya macho yao na sio kutumia nguvu kubwa kuwaaminisha kuwa tunachokiamini ni sahihi kuliko chao wakati hata sisi hatuna uelewa mkubwa wa kile tunachokiishi. Uwe mkristo, muislam, msabato, muhindu au mpagani tambua kuwa unafki sio kitendo cha kiungwana.
Tutangulize upendo na utu kwa Kila Jambo.