Kimenukaa Urusi vs Marekani

Kimenukaa Urusi vs Marekani

Trump anaendelea kufeli kisiasa

alisema atafanya kazi na Russia,sasa wanatushiana

alimcheka Obama kwa hatua alizokuwa anachukua dhidi ya Syria,naye anafanya hayo hayo
Utashi wa taifa(National Interest) Kimataifa kwa Marekani huwa haubadiliki hovyo ingawa marais wanabadilika! hivyo kusema Trump kafeli kwa kufanya alichokuwa anafanya Obama si sahihi..wenzetu linapokuja suala la kitaifa kwa maslahi ya taifa huwa hawabadiliki!
 
Israel aliingia syria akafanya anayotaka akaondoka zake, putin sio mueled km tumchukuliavyo sisi

Ile mifumo ni kwa sisi tu tunabishana hapa ila kiukweli hakuna inachoweza fanya
Juzi juzi tu Israel kaingia na ndege zake pale
Putin akaanza piga kelele

Leo kapigwa na hiyo mifumo yake anaanza leta bit za kupeleka aircraft carrier Med Sea
 
Hivi we unaejiita profesa Zina kutosha kweli

Hivi unaelewa maana ya vita kuu ya Dunia?

Nikwambie tu Anaweza asife raia hata moja wa marikani, ila ukafa we uliepo Lind

Ila nakuhurumia sana km kweli we ni professional profesa

Mleta thread unajua kuogopesha watu! habari ilivyokaa utafikiri vita ya tatu ya Dunia (WWIII) ndo tayari ilishaanza....ila kiukweli natamani kuwaona USA na Russia vitani...I mean serious war na harafu nione who will prevail! maana tumechoka sasa (In mizengo pinda's voice)...
 
Red line ipi we Mmakonde, Israel juz kaingia syria kafanya anayotaka kaondoka urus kaishia kulia tu

Hamfahamu tu namna vile Warusi walivyo, ile red line waloichora ikivukwa tu basi mtapata kuwafahamu na hapo ndiyo utajua ubora wa hiyo mifumo nk .
Unakumbuka kule Crimea kilichotokea? Pale red line ilivukwa polite people wakaingia uwanjani.
 
Utakuwa ni kichaa kutangaza idad ya wanajesh wanaokufa vitani wakat vita vinapiganwa
Hivi huwezi hata kujiongeza mkuu

Mkuu unaziamini taarifa toka BBC zinazo zungumzia nguvu au uwezo wa kivita na kiuchumi wa Urusi? Uingereza ni adui namba moja au mbili wa Urusi(Russia). Sehemu kubwa ya habari zao zinakuwa za propaganda au zinachaguliwa zile zenye kuonesha udhaifu wa Russia lakini wakati huo huo kuna habari nyingine nyingi ambazo za matukio ya ubora/uimara wa Russia lakini hawazirushi BBC makusudi. Kama kuna makombora au ndege za Uingereza na washirika wake zinaporomoshwa na silaha za warusi hawawezi kuzirusha au watarusha idadi ya uongo kukwepa mgogoro wa kisiasa na wananchi wao.
Unajua askari wangapi wa uingereza na washirika wao walikufa kule Irak na Afghanistan? Maiti zilikuwa zinashushwa na ndege kimya kimya, ni mara 2 hadi 5 zaidi ya ile idadi unayoipata toka ktk vyombo vyao vya habari.
 
WE UNADHANI URUSI WALIKUWA HA3ANA UWEZO WA K6ZUIA? WALIPEWA TAARIFA NA MAREKANIWAKAWAELEZA ZILIPO NDEGE ZAO NA MAJESHI YAO KTK UWANJA HUO AMBAO NDEGE NA VIFAA VYA ASSAD VILIMIMINIWA MAKOMBORA. SASA UELEWE KIDOGO WAKUBWA WALIVYO.ISRAEL YENYEWE WAKISHAMBULUA URUSI INAPEWA HABARI NA MAREKANI NA KUEPUSHA VIFAAA NA WATU WAKE WALIOKO KULE SYRIA NA HILO ULIJUE. WANAEND3LEA KUSIDIA WAARABU WAJIANGAMIZE WENYEWE WASIJE WAKASINGIZIA WARUSI AU WAMAREKANI.AKILI MUKICHWAAA. UNAELEWA HAWA WAKIWA SUPER POWER WATAFANYA NINI DUNIA HII
 
Utakuwa ni kichaa kutangaza idad ya wanajesh wanaokufa vitani wakat vita vinapiganwa
Hivi huwezi hata kujiongeza mkuu
Exactly that is what I'm talking, kwamba sio taarifa zote zinawekwa hadharani kwa sababu mbalimbali. Kwa hivyo sio kwamba silijui hilo isipokuwa hujanielewa, nilikuwa najaribu kuelezea sio taaarifa zote unazosikia ni sahihi.
 
WE UNADHANI URUSI WALIKUWA HA3ANA UWEZO WA K6ZUIA? WALIPEWA TAARIFA NA MAREKANIWAKAWAELEZA ZILIPO NDEGE ZAO NA MAJESHI YAO KTK UWANJA HUO AMBAO NDEGE NA VIFAA VYA ASSAD VILIMIMINIWA MAKOMBORA. SASA UELEWE KIDOGO WAKUBWA WALIVYO.ISRAEL YENYEWE WAKISHAMBULUA URUSI INAPEWA HABARI NA MAREKANI NA KUEPUSHA VIFAAA NA WATU WAKE WALIOKO KULE SYRIA NA HILO ULIJUE. WANAEND3LEA KUSIDIA WAARABU WAJIANGAMIZE WENYEWE WASIJE WAKASINGIZIA WARUSI AU WAMAREKANI.AKILI MUKICHWAAA. UNAELEWA HAWA WAKIWA SUPER POWER WATAFANYA NINI DUNIA HII
Hivi, mnafikiri dunia hii ikiwa na amani na utulivu, viwanda vya silaha vitafanya kazi gani?
Halafu, mkiwa na amani na utlivu, na mkastawi, viwanda vyao vya mahitaji ya wanadamu vitafanya kazi gani?
Nadhani hata sisi Watanzania, pale ambapo wanasiasa wetu wanapotupeleka, hmm! Sijui!
 
Sasa Unataka urus watangazwe Kwan wao hawawez kujitangaza? We unataka nchi kubwa km urus ipewe msaada wa media?

Ushawahi kuangalia RT Inayomolikiwa na Russia?

Tena wenyewe wanatangaza ujinga tu habari zao hazina hata mvuto


Exactly that is what I'm talking, kwamba sio taarifa zote zinawekwa hadharani kwa sababu mbalimbali. Kwa hivyo sio kwamba silijui hilo isipokuwa hujanielewa, nilikuwa najaribu kuelezea sio taaarifa zote unazosikia ni sahihi.
 
habari zao hazina hata mvuto
Hoja yako kama niliyo kunukuu ni very subjective... Kinachokuvutia wewe kinaweza kisinivutie mimi and vice versa is true. Kwa jinsi ulivyojenga hoja yako sasa nazidi kukubali ile faida ya kuwafundisha watu lugha yako ili waishi wakiongozwa/kulazimika kufuata mawazo yako na utamaduni wako. Sisi tungetawaliwa na Russia tungekuwa tunafuatilia sana mambo yao na kuyaona ndio bora. Kinachotuumiza na kutufanya tuishi katika ulimwengu usio na uhalisia kuwa wanataka tuamini kile wanachotaka tuamini sio kile tulichotakiwa tuamini bila kuwekewa nguvu ya msukumo toka kwao. Kwanini waingereza na wamarekani na wafaransa, wachina na warusi wanapigana sana kueneza lugha zao? Jibu: Tuishi watakavyo wao kwa utamaduni wao tuwe watumwa wa bidhaa zao(iwe vitu au taarifa).
 
dah ustadh ungepitia kwanza andiko lako kabla hujaileta hapa.. naona unachanganya destroyer na aircraft carrier.. destroyer inabeba makombora na kushambulia wakati aircraft carrier ndo inabeba ndege nyingi zikiwa za mashbulizi kwa ajili ya kusogeza mashambulizi karibu.. destroyer inabeba helicopter moja au mbili tu kwa ajili ya kufanya operation ndogo ndogo karibu na meli husika japo nyingi hua zinatumika kutrack nyambizi... na kwa suala la uwepo wa S-300 na S-400 ndani ya Syria na kua kwa kua zipo Syria haikutakiwa kua inashambuliwa na nchi kama Israel na jana Usa nadhan kuna ushabiki unatufanya kutofuatilia mambo kwa uhalisia wake.. ulinzi wa anga hua sio swala dogo hasa kama unajilinda dhidi ya adui mwenye uwezo kama Usa na Israel.. kujilinda dhidi ya nchi kama hizi unahitaji kua na mtandao ambao uko intergrated unaounda kitu kama mwamvuli juu ya anga la nchi husika.. mfano unahitaji SAM batteries atleast katika kila eneo ambalo ni strategic, kua na early warning radars, early warning satellites na centeres za kucontrol hizi assets zote.. hivyo kwa kesi ya Syria hii inakua ngumu kwa kua mitambo ya kisasa iliyopo ni minne tu tena nayo iko kwenye base za Russia tu za Tartus na Hynemym(sina uhakika na spelling).. mitambo yenyewe ni S-300V(special kwa kutungua makombora, S-400(special kwa kutungua ndege hasa fixed wing kama fighters), Pantsir S1 (special kwa helicopter, vifaru na drones) ila pia kuna mtambo wa Bastion anti ship(ulinzi wa pwani).. hii mitambo ni michache kwa ulinzi wa nchi nzima na isitoshe ilipelekwa Syria kwa ajili ya kulinda ndege na base za Urusi ndo maana karibu yote imepelekwa pale tu Uturuki walivotungua ndege ya Russia.. Syria ana mitambo yake kwa ajili ya ulinzi wake sema almost yote ni ya enzi za soviet na ni michache pia.. S-300 na S-400 zisingekua na chochote kama makanjanja wengi mnavodai leo China, India, Iran, Turkey na nchi nyingine nyingi zisingekua eager kutaka kuinunua hii mitambo pia Netanyahu asingehaha kwenda Moscow kumshawishi Putin asiruhusu uuzwaji wa S-300 kwa Iran.. Pia isingekua na chochote tungesikia base na ndege za Russia nchini Syria zinahujumiwa lakini hamna kitu kama hicho... Kwa hiyo sa nyingine ni vizuri kuongelea na kuchambua mambo ya bashite na gwajima, mange na diamond maana ndo tunayoyajua sio haya mengine
Kwaiyo Russia na USA nani zaidi kwa vifaa vya kisasa mkuu?
 
Duh aisee RUSSIA imepeleka Warship Mediterranean ocean kuzikabiri fighting jets za USA zinazorusha makombora sasa hivi Syria kutokea kwenye Destroyers ambazo zipo Pia mediterranean ocean.Hii ni hatar kwa usalama wa dunia.Wale watu wa mungu msali tu sasa huu ndo muda
Russian warship heads toward U.S. Navy after Syria strikes
Russian warship steams toward US destroyers that launched Syria strikes
waandishi nao kwa kupika story si haba!! Mrusi kasema meli yake kwenda Mediterranean ni routine ya kawaida sio kama waandishi wanavoipika story 😀
 
Kwaiyo Russia na USA nani zaidi kwa vifaa vya kisasa mkuu?
Me naona US.
Japo sipend kuiunderestimate Russia coz nao wapo vzr.
Ila ukilinganisha Air power,Navy,Land...mwnyw jibu utapata.
 
Hivi we unaejiita profesa Zina kutosha kweli

Hivi unaelewa maana ya vita kuu ya Dunia?

Nikwambie tu Anaweza asife raia hata moja wa marikani, ila ukafa we uliepo Lind

Ila nakuhurumia sana km kweli we ni professional profesa

😛😛mkuu punguza jazba.yaani anaweza asife raia wa marikani akafa yeye wa lindi.dah
 
Back
Top Bottom