Kimenuka jumuiya za kimataifa, Rais Magufuli hasomeki

Kimenuka jumuiya za kimataifa, Rais Magufuli hasomeki

SOURCE please!!!Kutokuhudhuria mikutano sio ujanja kwa kuwa unaipotezea nchi fursa nyingi.Utaja jua tu kwanini mkuu wa kaya anaipiga chenga mikutano ya kimataifa wakati muda utakapofika.Fikirisha akili kidogo kabla yakuleta uzi mheshimiwa.Ukinyamaza unaweza hesabiwa hekima zaidi.
Fursa ipi ya presida kuhutubia dakika kumi na kurudi gharama za nchi kazi kuuza sura tu baasi
 
Kabisa huyu ndo rais mwenye msimamo asiyeburuzwa na mabepari safi sana tukijitegemea tutaendelea haraka kuliko izo za kuburuzwa na mabepari nilikua naota sana tuwe na raisi kama huyu na wakija hapa sisi ndo tutawatungia sheria za kuishi na kufanya biashara apa
 
HII INAONYESHA WAZI JPM ALIINGIA MADARAKANI AKIJUA FIKA NINI ANAKWENDA KUFANYA,THATS WHY HATA WAPINZANI WAMESHINDWA KUMSOMA,LA MSINGI NA LA MAANA NI KUZIDI KUMUOMBEA RAIS WETU AFYA NJEMA,SABABU ANA DHAMIRA SAFI YA KUISAIDIA NCHI YETU,PIA NI MENGI USIYOYAJUA KAMA UYAJUAVYO.
Mi nadhani CCM ndio wameshindwa kumsoma kabisaaaaa! Wala si wapinzani.
 
Tena wasije na wakija Rais aongee kiswahili ili wajue na sisi sa hivi tutatoka wenyewe
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga
mambo ya msingi wewe unatoa comment za kitoto sana. Tangu line mwenye PHD ya Chemistry akashindwa kuongea kiingereza, usipende sana kuziamini habari za udaku, watu wanapojadili mambo ya msingi jitahidi kuweka utoto pembeni, mada nyingi zinahitaji fikra makini, sio kila sehemu mtu aandike kwa sababu anao uhuru wa kuandika.
 
father Magu,piga kazi kurudisha heshima ya nchi yetu,watanzania tupo nyuna yako.
 
Tatizo lugha kule hawaongei kiswahili,jk alipewa miaka kumi kuwa waziri wa mambo ya nje ili ajifunze lugha akaambulia kile anachoungaunga
Mbona rais wa China alipokuja hapa aliongea Kichina ? Ingawa JPM anajua kiingereza vzr lkn sii angeweza tu kuongea Kiswahili au hata kisukuma na kila kitu kingeenda sawa tu....
 
mambo ya msingi wewe unatoa comment za kitoto sana. Tangu mwenye PHD ya Chemistry akashindwa kuongea kiingereza, usipende sana kuziamini habari za udaku, watu wanapojadili mambo ya msingi jitahidi kuweka utoto pembeni, mada nyingi zinahitaji fikra makini, sio kila sehemu mtu aandike kwa sababu anao uhuru wa kuandika.
Wewe ulimuona wapi akiongea kingereza
 
Wewe hujui kwamba hakwenda kwa sababu hajui kingereza? Ataongea nao nini wakati anajitanabahisha kwamba yeye ni Dr na kasoma kwa kutumia lugha ya kiingereza? Kama kasoma kwa kutumia kiingereza maana yake anakijua kiingereza kwa kuwa alikuwa anakijua na ndiyo maana alielewe masomo an kufaulu. Sasa unataka aende akashindwe kuwasiliana naye atengeneze Headlines duniani kwamba ni kiongozi anayetiliwa kughushi elimu?

Ataongea nao nini?

Acha visingizio badala yake nyoosha maelezo. Tatizo si nii wala nini. NI LUGHA!.



Kuna wingu zito kati ya ushirika wa NATO na mshenga wao Marekani na ule mlengo wa kushoto wenye wakumunisti wa zamani China na Russia.

Issue iko hivi.

Mabepali wa Ulaya na Marekani hawamsomi JPM kabisa, kama unavyojua kila Rais mpya anapoingia hawa ndugu zetu hufanya juu chini ili kupata nafasi ya kumteka katika upande wao, ili maslahi yao na ya makampuni kutoka kwao yalindwe. Sasa kasheshe likaanzia hapa

Mabepari walimualika Mh JPM katika mkutano wa Jumuiya ya Madola in personal, kwanza ili ajitambulishe kwa wenzie lakini pia wapate nafasi ya kuteta nae kuhusu interest zao, na kumvutia kwao. Jamaa hakwenda akatuma wawakilishi.

Wakamualika tena kikao cha mazingira na hali ya hewa, Ufaransa, ikiwa ni mara ya pili, ili kupata nafasi tena ya kutimiza ile adhma yao, jamaa tena kakomaa, hakwenda instead akatuma wawakilishi. Hii haikumfurahisha Uingereza kabisa na za chinichini zinasema akamtonya mshenga wake Marekani watunyime zile za MCC ili Mkuu wa kaya afunge safari kwenda kuwabembeleza na wapate nafasi ya kutoa masharti.

Mshenga akafanya hivyo kwa visingizio vya kitoto. lakini mpaka leo JPM hajaenda wala kubembelezea hiyo kitu. Jamaa wakapanic na wakaanza kufikiri labda JPM anahamia ukomunistini

Wakuminist kuona hivi, wakatupa karata yao, kwanza wakamualika kwenya kikao muhimu cha SINO Africa, wakijua jamaa hachomoi hapo, na kwa za ndanindani ujumbe wa Russia pia ulikuwepo huko SA, to their surprise JPM hakutokea instead akaenda VP. China na mshirika wake Russia wamesikitika sana hasa ukizingatia Russia anaitolea macho Gas yetu kwa muda sasa.

Ikumbukwe Tanzania ina reserve kubwa sana ya Uranium, Gas, na Coal , hivi ni vitu muhimu sana kwa hii miamba ya milengo miwili na mpaka sasa wanashindwa kumuelewa JPM. Hawamsomi wala hasomeki kwao

Nasikia soon Tutapata ugeni mzito, wameamua kuja wenyewe

JPM hasomeki, Hongera JPM
 
Jifanye hujaona clip yake wakati anajitafuna tafuna na jasho kumtoka akiongea english
Huo ndio ukisikia umaskini wa mawazo na ujinga ndio ulio nao wewe. Wachina na wajapan na warusi kila sehemu wanatumia lugha zao tu na wamegundua vitu vingapi? na wanakwenda mikutano ya kimataifa na kuongea lugha zao je wamepungukiwa nini? mtumwa we, hata Magufuli akienda kuongea kiswahili wakalimani wapo na watamuelewa tu acha utumwa.
 
Mtu anasema rais hajui kiingereza, yeye anayejua hiyo lugha ya malkia ameifanyia nini nchi hii?,kuna watu wana akili za kitumwa sana. Kwao mtu kujua kiingereza tayari ameshaikaribia mbingu. Akili za kijinga sana, kwa bahati mbaya hii ni mmojawapo ya vitu vinavyotutambulisha watanzania. Watanzania wangapi ni madaktari waliosomea Russia na kufundishwa na maprofesa wasiojua kiingereza, Watanzania wangapi wamesomea uhandisi Ujerumani na wamefundishwa na maprofesa wasiojua wala kuithamini lugha ya kiingereza?. Huu ni ushamba ambao baadhi ya wachangiaji wa JF wanao.
 
I think President Magufuli is planning to move our country in the middle. If so then he will be playing to our strengths coz we need them both (west and communist world).
HIKI kizungu ni lazima! jisomee kwanza binafsi kabla hujakileta kwenye hadhira! ukitafsiri kiswahili kwenda kizungu ndio haya matokeo! 'is planning to move our country in a middle'
 
Wewe ulimuona wapi akiongea kingereza
Kuongea kiingereza sio ujanja, amekuwa waziri wa ujenzi kwa miaka mingapi?, unataka kuniambia mawasiliano yote aliyokuwa akiyafanya na wamiliki wa makampuni ya ujenzi yaliyojenga madaraja na barabara, alikuwa akiyafanya kwa kutumia lugha ya kiswahili?, vitu vingine sio lazima uambiwe jaribu kwa akili zako kujiuliza kabla hujajitia aibu kwa kuandika utumbo humu JF. Kwa wewe kutoiona mikanda ya video inayomuonyesha akiongea kiingereza haimaniishi kuwa hajui kiingereza, au ulitaka wakati anaongea na makandarasi wa kigeni akuite ili ujue kuwa kweli anao uwezo wa kuongea kiingereza?.
 
Hizo nchi au jumuiya zina wawakilishi wao hapa nchini.hawawezi kupanick kwa Magufuli kutokwenda kwenye mialiko yao! tunamikataba kibao yenye kujali maslahi yao tuliyoingia nao.hatuwezi kuivunja wanasheria wetu wanaingia mikataba inayotubana sisi kuliko hao business partners wetu.so uzi huu ni fikra binafsi.
 
Huwezi kumchenga mchina au mzungu eti ukajitegemea mwenyewe,haiwezekani,nchi zote zinategemeana isipokuwa inatakiwa mikataba ambayo iko fair.uwekezaji wote unategemea wageni,imports and exports zinategemea wageni,mtauza wati madini na mazao yenu kama mnajifungia ndani.economic diplomacy ni muhimu kwa sasa
Tanzania inao mabalozi wangapi huko nje? wanalipwa mishahara ili wafanye kazi gani?. Miaka 10 ya JK economic diplomacy imefanyika sana, huu ni wakati wa kuweka msisitizo kwenye uchumi wa ndani.
 
Usijifananishe na mchina.mchina yuko level ya USA kiuchumi na kitechnolojia so ana jeuri ya kukomalia lugha yake.si unajua jeuri ya pesa
Matumizi ya Lugha yake ndo yamewafikisha hapo, kuwa level inayokaribiana na USA> Kumbuka, Lugha sahii hufikisha ujumbe sahii
 
Russia anaitamani gesi yetu ili aifanyie nini? Kwa gas reserve au technology ya kusambaza gas tunamshinda Russia au?
 
Back
Top Bottom