Leo mchana nikijadiliana na mbunge mmoja wa CCM kutoka mkoa wa Dar, aliniambia wazi kwamba, Lowassa hawezi kufukuzwa chamani, kwani ndiye anayeunganisha chama. Kabla ya EL kungo'lewa gamba, mwenyekiti atakuwa wa kwanza kwani matatizo lukuki ndani ya chama na taifa yametokea katika utawala wake. Amesema udini, ufisadi, umasikini, siasa ya makundi yameendelezwa na mwenyekiti wa chama na siyo Lowassa, kwa maana hiyo gamba kubwa ni Rais mwenyewe na siyo EL.
EL akingo'lewa basi tutaelekea kwenye uchaguzi mara moja na CCM itakufa kwa maana 70% ya wabunge CCM wanamuunga mkono EL. JK hawezi kumgusa EL na anajua hilo