Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 617
Kuna taarifa kwamba, vikao vya awali vya CCM mjini Dodoma vimeanza kwa kuwahoji vijana kadhaa wa UVCCM wanaotajwa kuwa karibu na Watuhumiwa wa ufisadi walotakiwa kujivua gamba.
Haijafahamika kama vijana hao watakua kafara la baba zao ama ndio kipima joto cha maamuzi magumu yanayotarajiwa kufanywa wiki hii. Hakika mwandishi mahiri wa makala katika Raia Mwema alisema, "mbele giza nyuma kaburi" na sasa uamuzi wa kurudi nyuma ni CCM kuingia kaburini na kwenda mbele ni gizani maana magamba yana nguvu za ajabu na kila kukicha yanakua magumu.
Je, CCM itaamua kuingia gizani kuvua magamba ama kurudi nyuma na kuyaacha iwe ni kaburi la CCM?
Taarifa zaidi baadae.