Kimenuka: Baraza la Wakulima Tanzania lawajia juu ACT-Tanzania

Eti Pigo mbona kitu kidogo sana hicho. Sisi washabiki hatufuati jina tunafuata muelekeo wa chama uzalendo, uwazi ,na mdiliko! Hata jina lao likiwa . ( Yaani fullstop) litapata wanachama wengi tu. Hivyo sisi hilo kwetu ni dogo sana.
 
Kimenuka vipi sasa nani wa kupewa lawama kila mmoja yupo kisheria na anafanya kazi zake bila kuvunja sheria za nchi, hawa Baraza la Kilimo walikuwa wapi siku zote kupinga ilo jina.
Kwa mara ya kwanza nimekubaliana na ulichosema. Kwa nini hili Baraza la Kilimo halikuona ufanano huu wa jina hadi ZZK alipojiunga na ACT ndiyo waibuke kudai hayo???
 
ACT = Artemether Combination Therapy (Dawa Mseto ya kutibu Malaria). Nembo hii (ACT) imesajiriwa na shirika la Afya Duniani WHO!
 
Zikiwa ni dalili za bundi kuendelea kuandama jitihada za Mwenyekiti mtarajiwa wa ACT-Tanzania, BARAZA la Kilimo Tanzania (ACT), limekitaka chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), kuacha kutumia kifupisho (Nembo), cha jina la chama hicho kwa vile kinafanana na cha baraza hilo la wakulima.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Sinare Sinare, alisema Baraza hilo limefikia hatua hiyo baada ya kufanya majadilino na kukiandikia barua chama hicho cha siasa mwaka huu kubadili kifupisho hicho, lakini hadi sasa chama hicho kinaonekana kudharau matakwa ya baraza hilo.

Alisema dharau hizo za (ACT-Tanzania), zimesababisha kuleta mkanganyiko kwa wanachama wa baraza la kilimo kushindwa kutofautisha baadhi ya taarifa zinazotokana na vifupisho vya Baraza na chama hicho. Kinachotokea ni wanasiasa kutopenda kufuata sheria, wao walichotakiwa kwanza ni kufuatilia kwenye mitandao ambako wangegundua uwepo wa jina lenye kifupisho chetu, alisema Dk. Sinare.

Dk. Sinare, alisema baraza hilo, limefikia uamuzi wa kukitaka chama hicho kuacha kutumia kifupicho hicho kwa vile baraza limeanzishwa tangu mwaka 1999 na kupata setifiketi ya kumiliki nembo hiyo ya ACT ya mwaka 2014.

Haiwezekani katika nchi moja kuwa na taasisi mbili tofauti zinazotumia nembo moja inayofanana na kwa yeyote atakayekwenda kinyume kwa kutumia nembo hiyo kwa maslahi tofauti na baraza watambuwe kuwa upo uwezo wa kuburuzwa katika vyombo vya sheria, alisema Dk. Sinare.
Dr Sinare, Katokota!
 
Back
Top Bottom