katika vita haijalishi tu unasilaha kali na kubwa kiasi gani, vita inajali pia idadi ya silaha ulizo nazo, inawezekana Mapanki akawa na silaha nzuri lakini Je anazo za kutosha. Marekani anasilaha nyingi sana, akiamua kuziamisha zote katika wanja wa vita anauwezo wa kuondoa nchi kwenye ramani ya dunia, pia jua kuwa marekani inapigana huku inaangalia sheria za kimataifa au tuseme huku mkono mmoja umefungwa, kama ikiamua kujitoa ufahamu ikafunga macho, inaweza sababisha madhara makubwa sana, wala nchi kama korea isipate hata sekunde ya kutumia silaha zake, kisha ikajikaanga na silaha zake yenyewe.
CHAMUHIMU TUMUOMBE MUNGU AEPUSHE HII VITA, watanzania wengi tunashabikia kipuuzi tu hatujui madhara tutakayopata kwenye hii vita yatakuwa makubwa sana, kwa sasa bila vita lakini maisha yetu ni ya kuunga unga, mimi fani ninayofanyia kazi inahusiana moja kwa moja na dunia ya mbele, sasa patakapo kuwa na vita madhara nitayaona wazi. mfano rahisi ni kipindi hali ya amani ilipokuwa mbaya kenya kutokana na vishambulio vya alshabab, madhara yake yalichukua zaidi ya mwaka ku heal, sasa je hili la mabwana wakubwa je?
EEEE MUNGU USIKIE DUA ZETU, TUEPUSHE NA HILI BALAA. AMEN