Ndugu zanguni, sijui kama mnafuatilia sakata kati ya Apple Smartphones na Serikali ya Marekani. Serikali inashinikiza Apple wawatengenezee backdoor App. ili waweze kusoma encrypted messages za wale majangili (mke na mume) walioua watu huko California hivi karibuni. Inaelekea serikali itashinda.
Hii ni hali ya hatari sana. Hivi sasa wote katika mtandao, hasa wanaotumia Smartphones, hawana privacy yoyote ile. Apple ameifanya simu yao mpya kuwa na uwezo wa kutumia encryption ili mtu baki hawezi kukusoma. Najua Whatsup pia wanafanya hivi. Kama California wakishinda hii kesi basi ujue tumekwisha. Huwezi tena kutongoza mke wa mtu (mchepuko) na ukawa na uhakika hutakuja katwa mapanga na mwenye mali (hii nimechapia tu).
MFANO:
Wanachofanya hizi serikali zote duniani ni mfano wa Shirika la Nyumba kujenga nyumba za kisasa lakini kila chumba kikawekwa vinasa sauti na kamera (ili mwenyewe uweze kuiona unapokuwa safarini) lakini serikali pia inapoamua tu wanaweza nao kuangalia kinachoendelea kila chumba na wakati wowote ule. Sidhani kama kuna mmoja wetu atakaekubali kununua nyumba kama hiyo.
Kwa wale wenye Smartphones au wanaofikiria kuzinunua, tafakarini sana. Najua kuna faida nyingi sana za kutumia hizi Smartphone lakini hizi serikali wanachofanya ni kitu cha ajabu sana. Kama unaridhia upekuzi huu wa hali ya juu usiku na mchana pasi wewe kujua, haya endelea nayo. Mwenzenu machale yamenicheza.
Mimi niliamua siku nyingi sana kwa makusudi mazima kutumia kitochi (dumb phone) badala ya Smartphones. Zaidi ya hapo, ile kamera ilioko kwenye kompyuta yangu nimeiziba. Huifungua tu pale ninapoihitaji (kama kutumia Skype).
Nimeleta hii mada kwenye jukwaa hili kwa waliokubuhu kwenye hizi teknolojia. Haya, nijuzeni ushamba wangu uko wapi?