Wanajamii nimekutana asubuhi hii pale ubungo Bus terminal na kijana aliye chaguliwa kuanza masomo pale IFM Kozi ya Banking and Finance. Amenyimwa mkopo na loan board hata wa asilimia 0. Tuition fee peke yake ni Tshs.1,920,000 (Millioni moja na laki tisa na elfu ishirini).Hivi sasa kadiri ya maelezo yake anarudi nyumbani Arusha (Arumeru Magharibi) kwani hana namna ya kusoma tena na amesisitiza hana sababu ya kuendelea kuishi. Amenionyesha vyeti vyake ana Division 3 point 14. JAMANI NIMECHOKA NA KUDUWAA WANGAPI WAPO KAMA HUYU.