Ufafanuzi wa kufutwa kwa VRF kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, waajiriwa tegemeeni kuongezeka kwa take home

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,035
6,907
Nawasalimu kwa jina la JMT

Kulikuwa na maswali kadhaa kwamba je Salary itaongezeka baada ya kufutwa kwa tozo ya VRF ya 6% kwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya Juu au hapana.

Jibu ni kwamba take home itaongezeka maana makato ya 15% kwenye mshahara wa mwajiliwa nayo yana mchanganuo wake kwa mujibu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Kwa mfano kama ana salary yaTsh. 1,000,000 kwa mwezi na alichelewa kuanza kulipa atakatwa 15%=Tshs.150,000/=

Sasa hii 150,000 iko kwenye mchanganuo uliogawanywa kama ifuatavyo;

i) 1% ya Loan admnistratio fee=1,500

ii)6% ya VRF=9,000

iii) TSH.15,000 ambayo ni ADHABU ya kuchelewa kuanza marejesho na

iv)TSHS.139,500/= ndio pesa inayopunguza deni halisi yaani Principal Amount

Kwa hiyo kanuni ndio hiyo hapo na iko applicable kwa kila mtu kulingana na kiwango chake cha mshahara

Kwa mantiki hiyo basi 6% iliyofutwa kwa kutumia mfano huo hapo juu ni TSH.9,000/= ambayo itaongezeka kwenye Take Home ya mhusika.

Kwa hiyo ndugu watumishi ukichukua hiyo VRF iliyofutwa na punguzo la 1% kwenye Kodi ya PAYE bila shaka kuna pesa ya kilo kadhaa za nyama zimeongezeka wengine watapata kiasi hadi cha kukopea.

Technically makato ya 15% ukitoa hiyo 6% na 1% inabaki asilimia 9% ambayo ndio makato halisi na hayo mengine ulikuwa wizi.

Note,Kwa mtu ambae ameanza malipo kwa wakati ile adhabu haimuhusu.
View attachment 1776150View attachment 1776151View attachment 1776152

IMG_20210507_100519_726.jpg
 
Sijaelewa vizuri. Mh. Rais kasema mnufaika ataendelea kukatwa 15%. Hiyo 6% nilitegemea ionekane upande mwingine ambao hawaonyeshi kwenye salary slip.
Kuna shida sehemu. Bodi wamebambikia sana watu madeni hewa. Sasa kama mgao uko hivyo kwanini waongeze deni baada ya kumaliza?
 
Haitaongeza chochote katika Net take home kwasababu, huo mchanganuo wa 15% unafanyikia bodi na sio kwa mwajiri.

IKO HIVI

1. Administration fee 1% huwa inalipwa kwa mkupuo unapoanza2 kukatwa/kulipa.
2. There after 6% Ya unachokatwa (15% of your basic salary) kinaenda kupunguza outstanding retention fee.
3. Finally, Kinachobaki ndicho kinaenda kupunguza Principle outstanding loan.

Hivyo basi, kwakufutwa VRF hakutaathiri Take home Bali kutaleta tija katika kupungua kwa as the result, repayment period itapungua.
 
Makato ni Yale Yale VRF ilikuwa inaongezwa kwenye principle ndio maana den lilikuwa haliiishi kwakuwa mwisho wa mwaka ukiongeza 6% Deni linarudi vile vile

Sent from my CPH1937 using JamiiForums mobile app
Hivi ndivyo hata mimi ninavyo ielewa. VRF haikatwi kwa mwezi ila ni increment ya 6% kwenye principal amount ya mkopo.

Mfano kama mkopo wako wote ni 5,000,000/=(milioni 5) basi kila mwaka deni lako litaongezeka kwa (6% × 5,000,000/=) i.e 300,000/=(laki 3).

Kwa hyo kwa mfano kama deni lako ukiligawa ile 15% unayokatwa likawa litaisha kwa miaka kumi basi kuna milioni 3 itaongezeka kwenye deni kama VRF, hivyo utakatwa miezi mingine 20 zaidi kukamilisha deni lako.

Sasa sijajua kama VRF imeondolewa tangu ile iliyokuwa ikiongezwa baada ya VRF kuanzishwa ama inaanza with effect from now.

Hivyo basi VRF haiathiri makato ya mshahara ya mwezi bali inaathiri principal amount ya mkopo na muda wa marejesho, kama ulikuwa ulipe kwa miaka kumi utajikuta kuna miaka almost miwili ya ziada.
 
Hata mm nilikua najiuliza hilo....inafaa watoe VRF iliyowekwa na deni libaki kama mwanzo
 
Mm deni langu lilikua 7.3m baada ya kuweka VRF admistration fee na Panalti likafika 13.6m..swali je
Deni langu litarudi kwenye 7.3m au ndo litabaki kwenye 13.6 na halitaongezeka?
Hapa kuna mchanganyiko sana. Hapa ufafanuzi wa maana unahitajika. Wakitoa hizo gharama zao za uonezi madeni yangekuwa yameisha.
 
Hadi tuone matokeo maana ufafanuzi wako unatuacha njia panda. Kwa nijuavyo mimi 6% ya VRF inajitegemea, 1% ya administration fee inajitegemea na 15% inayokatwa kama marejesho ya deni nayo inajitegemea kivyake.
Mimi nimeweka hapo maelezo yaliyotolewa na Bodi na nategemea ongezeko la aslimia 6 isome kwenye salary
 
Mm deni langu lilikua 7.3m baada ya kuweka VRF admistration fee na Panalti likafika 13.6m..swali je
Deni langu litarudi kwenye 7.3m au ndo litabaki kwenye 13.6 na halitaongezeka?
Tusubirie ufafanuzi wa Bodi walisema wanapitia upya madeni baada ya kufutwa VRF
 
Back
Top Bottom