Kilio elimu ya juu

emrema

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
268
42
Wanajamii nimekutana asubuhi hii pale ubungo Bus terminal na kijana aliye chaguliwa kuanza masomo pale IFM Kozi ya Banking and Finance. Amenyimwa mkopo na loan board hata wa asilimia 0. Tuition fee peke yake ni Tshs.1,920,000 (Millioni moja na laki tisa na elfu ishirini).Hivi sasa kadiri ya maelezo yake anarudi nyumbani Arusha (Arumeru Magharibi) kwani hana namna ya kusoma tena na amesisitiza hana sababu ya kuendelea kuishi. Amenionyesha vyeti vyake ana Division 3 point 14. JAMANI NIMECHOKA NA KUDUWAA WANGAPI WAPO KAMA HUYU.
 
KAMA NI KWELI, HIO NI RASILIMALI YA TAIFA INAYOPOTEA.

ILA KUNA TATIZO PIA HESLB; WALIOKOPA MIAKA YA MWANZO HAWALIPI, HIVYO KUFANYA AVAILABLE FUNDS KUWA CHACHE MNO.

WADAU

MWAKA HUU HESLB CUTOFF POINT YAO ILIKUWA NGAPI? MAANA NI COMPETITIVE

tHANKS FOR THE POST
 
Sikutarajia kama leo roho itaniuma namna hii.
Nimeumia sana baada ya kusoma hii taarifa ya kusikitisha.
kijana kama huyo wakitokea akina 'osama' wakimtrain kulipua Tanzania, atakubali na bila kipingamizi.
 
Wanajamii nimekutana asubuhi hii pale ubungo Bus terminal na kijana aliye chaguliwa kuanza masomo pale IFM Kozi ya Banking and Finance. Amenyimwa mkopo na loan board hata wa asilimia 0. Tuition fee peke yake ni Tshs.1,920,000 (Millioni moja na laki tisa na elfu ishirini).Hivi sasa kadiri ya maelezo yake anarudi nyumbani Arusha (Arumeru Magharibi) kwani hana namna ya kusoma tena na amesisitiza hana sababu ya kuendelea kuishi. Amenionyesha vyeti vyake ana Division 3 point 14. JAMANI NIMECHOKA NA KUDUWAA WANGAPI WAPO KAMA HUYU.

Wako wengi sana matatizo mengi ya nchi hii huwa tuna tabia ya kudharau na kupuuzia mambo ya msingi.
Mfano mzuri wakati ule wanavyuo wanagomea haya mambo wakapigwa hadi mabomu wazazi/walezi hawakunga mkono wala kuafiki kwa kisingizio wanataka wapewe hela ili wakalewe au kula raha na haya ndo matokeo yake.
Kwa sistimu ya nchi huwezi kukopesha watu wakati hujawaandalia mazingira mazuri ya kurudisha na ndo maana hata wale waliokopeshwa ni ngumu kuwakamata......agrhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
Nina alama katika mwili wangu kwa lile tukio pale SURVEY.......Wazazi walikua wanasema sie hatuna haja na shule...tunaangalia pesa tu.....
 
Tunamsaidiaje huyu dogo? mana haya mafisadi yanaiba tu kijana kama huyu anakosa fursa ya kusoma.
 
dah,this is terrible na sijui tuendako itakuwaje!

Ila asife moyo asubiri next year,

au kama anaweza kiji-support kwa semester moja aende chuo then akiwa chuo anaanza mchakato wa mkopo kwa mara nyingine,

wengi wamefanya hivo hapa UDSM ila wao atleast walikua na kauwezo sijui kwa ndugu yangu kama ataweza na ada yenyewe kubwa balaa.
 
Wanajamii nimekutana asubuhi hii pale ubungo Bus terminal na kijana aliye chaguliwa kuanza masomo pale IFM Kozi ya Banking and Finance. Amenyimwa mkopo na loan board hata wa asilimia 0. Tuition fee peke yake ni Tshs.1,920,000 (Millioni moja na laki tisa na elfu ishirini).Hivi sasa kadiri ya maelezo yake anarudi nyumbani Arusha (Arumeru Magharibi) kwani hana namna ya kusoma tena na amesisitiza hana sababu ya kuendelea kuishi. Amenionyesha vyeti vyake ana Division 3 point 14. JAMANI NIMECHOKA NA KUDUWAA WANGAPI WAPO KAMA HUYU.

Hiyo ni sehemu ya sera ya CCM. Maisha bora kwa kila Mtz
 
Wanajamii nimekutana asubuhi hii pale ubungo Bus terminal na kijana aliye chaguliwa kuanza masomo pale IFM Kozi ya Banking and Finance. Amenyimwa mkopo na loan board hata wa asilimia 0. Tuition fee peke yake ni Tshs.1,920,000 (Millioni moja na laki tisa na elfu ishirini).Hivi sasa kadiri ya maelezo yake anarudi nyumbani Arusha (Arumeru Magharibi) kwani hana namna ya kusoma tena na amesisitiza hana sababu ya kuendelea kuishi. Amenionyesha vyeti vyake ana Division 3 point 14. JAMANI NIMECHOKA NA KUDUWAA WANGAPI WAPO KAMA HUYU.

Huu utaratibu kwa kweli haufai kabisa. Elimu inabidi iwe haki ya kila kijana wa kitanzania. Hiyo hela ni nyingi sana.. na ukweli ni kwamba mtanzania wa kawaida (na hata wa middle class ya kitanzania) hawezi kumudu kulipa hela hiyo kwa mwaka.
 
Kile HESLB kinafanya sio kitu kizuri, wala huwezi kiukitafakari, wala kutolea maamuzi ni sawa na usimamizi wa kura za uchaguzi chini ya NEC. Uliza wanachuo wote utakukuta 100% majority ni wale wanaotoka katika mtandao wa watu wenye uwezo. You cannot imagine!!!. Ndio maana mara baada ya Kikwete kuapishwa amepewa ushauri wa bure kuchukua mazuri ya CHADEMA!!!
 
Back
Top Bottom