Kilio chetu juu ya Ukimwi

Mwlmgomaji

Member
Joined
Aug 3, 2012
Posts
93
Reaction score
6
Nipo hospitalini kwa ajili ya Kuonana na Doctor. Kama dakika kumi hivi hazijapita, watoto zaidi ya kumi wamekuja kuchukua dawa za UKIMWI. Wengine hawajasindikizwa na wazazi wao kama watatu hivi miaka takriban 4-6, Yani hali inatisha jamani. Yani ni kilio jamani. Hawa watoto wadogo wakija kuwa wakubwa je, patakuwaje huko mtaani. Endapo serikali inajijali yenyewe. Sisi watoto wa maskini afya zetu atazijali nani?
Picha zimegoma wadau mngeona jamani...
 
Tafadhali sana, hata hizo picha usiweke. Huo utakuwa ni uvunjifu wa privace yao. Kwa nini uogope wakati ukimwi uko tangu 1983? Tangu hapo mpaka leo ni miaka 29, ko kuna watu wana umri huo na kushuka wako positive ila hawafahamiki. Naomba wala hata usihangaike kuweka picha hapa! Je madaktari ambao tunakutana nao kila siku tusemeje? Hao ni watoto bwana, waache. Inaumiza sana we unapotoa machozi kuwaonea huruma aafu mwingine anaona ni kitu cha kuweka picha jf. Nilidhani ungeshauri kwamba tuwe tunapima kabla ya kufanya maamuzi ya kuzaa ili kuwanusuru watoto we unataka kuweka picha!
 
kwanza wewe unahitaji elimu juu ya haya mambo.
kwanza wala usijaribu kuapload hizo picha unajua sisi tulio huku jamvini twatoka wapi,, yawezekana ukaapload picha za ndugu zetu, hivi unadhani hatujui haya,, ,,au unadhani sie madakitari hatuyaoni haya si tungeweka picha,,,
tunaita proffesional ethics,, usithubutu.

thanks for ya concern about this, ni kweli janga limekua kubwa
watoto ni wengi swala la kutokuja na wazazi miaka 4-6 linaweza likawa geni lakini wengi wao wa umri huu
hata hawajui wanaumwa nini bado hawajaambiwa, ila huwa wanaambiwa pale wanapokua na uwezo wa kuelewa,
either na dakitari, nesi au mzazi baada ya kufundishwa namna ya kudisclose hili swala kwa watoto
baada ya kuelewa huwa ni kawaida kwa wao kuja kuchukua dawa wenyewe kwanza inawatengenezea uamifu na kujijali wenyewe..... kama kweli una uchungu fanya upate semina na uwe unatoa elimu kwa jamii kuhusu haya mambo au tembelea vituo vya kulelea kwa kutoa msaaada
 
Inasikitisha, wape pole lakini kama walivyosema wadau usiweke hizo picha hapa.
 
Usiweke picha tafadhari,hao watakuwa wameupata kutoka kwa wazazi wao,kuna jamaa m1 mwanae yupo shule ya msingi anatumia dawa arv,hili tatzo ni kubwa sana,watu(wanaume) wanaambukiza virusi makusudi mabinti na wake za watu,nashangaa TISS wanafanya kazi gani? Utalindaje nchi bila kuwalinda na wananchi? Watu walioumia mitaani wanajulikana na 2nawaona wanavyoendeleza libeneke chapa ilale yani inasikitisha!! Inafaa kuwe na karanteeni au Eviction....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…