KILIO CHAJA: Wafanyakazi na wamiliki wa mitandao ya kijamii kupoteza ajira

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Wakuu,

Hivi karibuni kama sikosei kumekuja tamko kuwa mitandao ya kijamii ( Blogs) kulipa kiasi fulani kwa mwaka.

Hapa kuna kilio kikubwa kwa wamiliki wa hiyo mitandao ya kijamii kutokana na kuwa (blogs) nyingi hazitaweza kulipa.

Hatujatema mate yakakauka tunasikia tena tamko mitandao ya kijamii kusajiliwa.

Kutokana na hivyo basi pia kuna kilio kwa wafanyakazi wa hizo blogs kwani blogs nyingi zitaondoa wafanyakazi.

Mbaya zaidi hata hizo blogs nyingi zitashindwa na kuamua kufunga.

Sasa hapa kuna kundi kubwa la watu ambalo linarudi nyumbani kwa kukosa ajira.

Nawaza tu; Hili kundi la hawa watu waliokuwa wamejiajiri na kuajiriwa wanakwenda wapi?

Nawasilisha.
 
maisha lazima yasonge na kutafuta fursa nyingine. sio kulialia
 
Kuna SHERIA ya ku control contents zinazotakiwa kupostiwa pia katika mtandao ya kijamii na blogs....

Ukivunja mtandao unapigwa lock mwaka mzima kama magazeti vile....
 
Itabidi zile domain tuzifanye za Kenya sio hii .go.tz bali iwe .ke.org maana huyu jiwe naye anahangaika sana maana mipango yake ikikwama yanakuja ya wasiojulikana
 
Si mbunge wala waziri yeyote mwanae atakaa anawinda dola 50 za adsense, hawajui kuna vijana tunalipa kodi kwakua hua tunawachukua shooting wanaoupload video youtube na kuna wengine blogs zinawaweka mjini.

Wana hamu ya kuhakikisha taifa linakua kimya juu ya mambo yao mpaka wanaharibu na vitega uchumi vya vijana.
 
Back
Top Bottom