A
Anonymous
Guest
Ningependa kuwasilisha masikitiko yangu kuhusu hali ya Kijiji cha Shabaha, Kata ya Mabogini, ni eneo linalokuwa kwa kasi, likiwa na idadi kubwa ya vijana na watoto, lakini linasahaulika katika mambo yafuatayo:
Miundombinu:
Barabara ya kutoka Manguzoni (mpaka wa TPC) kuelekea Shabaha hadi mjini ni mbovu sana na ina mashimo mengi. Ikiwa mvua zitaanza, mawasiliano yatakatika kabisa.
Elimu na Afya:
Licha ya ongezeko la watu, Shabaha haina Shule ya Serikali wala Kituo cha Afya. Hali hii inahatarisha maisha ya mama wajawazito na watoto wanaolazimika kufuata huduma mbali.
Wajibu wa TPC:
Sheria inaelekeza TPC kuchangia huduma za kijamii (CSR) kwenye maeneo yanayozunguka mashamba yao, lakini mchango wao hauonekani Shabaha.
Tunaiomba Serikali kupitia TARURA na uongozi wa Wilaya ya Moshi kuingilia kati. Wananchi wa Shabaha ni walipa kodi na wanastahili huduma bora za kijamii.