Kilio cha Madaktari wanaomaliza internship Awamu ya Tano

Wakati kKikwete ana ajiri hao wote alishindwa kusambaza dawa vizuri.
Alishindwa kutoa elimu bure hadi kidato cha nne.
Alishindwa kujenga maabara nchi nzima.
Alishindwa kusambaza maji safi kwa kiwango kikubwa hata hapa DSM. Huku maeneo ya Ubungo na Kimara tulikuwa hatupati maji ya bomba hata wiki 3 na zaidi.

Kwa mifano hiyo sio kusema Kikwete hakufanya kitu bali aligawa pesa kwa vipaumbele tofauti na Serikali hii.

Kuajiri waalimu bila vifaa vya kufundishia, bila madawati, bila maabara na kuajiri madaktari bila vifaa tiba na dawa kutosha ni kazi bure.

Watu wanaugua kipindupindu hovyo enzi zake kwa kukosa maji salama haina maana sana. Inabidi pesa chache zilizopo zisambazwe kidogokidogo kwenda kila sekta muhimu na sio kurundika daktari wanaokuja kugoma kazi sababu mishahara yao midogo na vifaa tiba hakuna wala dawa hakuna.

Umesikia sasa jiji la Dar likusumbuliwa na kipindupindu kama zamani kabla ya serikali ya Magufuli?

Acheni ubinafsi kuwaza muajiriwe ninyi na huku wengine wakifa kwa kukosa huduma sahihi za afya au vijana wengine wakishindwa kwenda shule tupate daktari na waalimu zaidi sababu ya kukosa pesa zilizorundikwa kwa ajira kwenye mzigo wa wage-bill.
We jamaa naona huna akili timamu!! Yaani ni vyema umuweke nyumban dokta ulimsomesha kwa mamilioni ya pesa ili utoe elimu bure? Hiyo elimu bure si ndio juzi watu walikua wanachangishwa baada ya wanafunzi kukosa chakula shuleni??

Je wazazi walishindwa kusomesha watoto primary au sekondary mpaka usiajiri madokta? Haya walimu nao vipi?? Mpaka leo wako nyumban na mashulen walimh wa sayansi hamna!!

Zahanati na hospitali hazina madokta alafu madokta wapo mtaani na kuajiri hutaki? Una akili wewe??
 
UDAKTARI, UHANDISI hizi kada zina tittle kubwa, masomo yake complicated.. ukija kwenye maslahi ndo hovyo kabisa, majina makubwa maslahi chini
Kweli kabisa,wiki jana nilienda Kijijini nyumbani sasa walitegemea Mhandisi naenda na MKOKO na Kumwaga mahela.Nikawaambia Hakuna mtakacho ambulia kutoka kwa Mhandisi Mimi ambaye ni Mzalendo(natumikia umma) Walicheeeka sana,eti bora uache hiyo fani
 
Kweli kabisa,wiki jana nilienda Kijijini nyumbani sasa walitegemea Mhandisi naenda na MKOKO na Kumwaga mahela.Nikawaambia Hakuna mtakacho ambulia kutoka kwa Mhandisi Mimi ambaye ni Mzalendo(natumikia umma) Walicheeeka sana,eti bora uache hiyo fani
Hii Inchi wote wanalalama sio mhandisi,daktari,Mwalimu,yaani wote haieleweki sijui ni nn kinatokea.Ni nani anakula keki ya Taifa hili kama ndio wasomi wetu wanalalamika namna hii?
Kuna shida sehemu hapa Kubwa sana .
 
We jamaa naona huna akili timamu!! Yaani ni vyema umuweke nyumban dokta ulimsomesha kwa mamilioni ya pesa ili utoe elimu bure? Hiyo elimu bure si ndio juzi watu walikua wanachangishwa baada ya wanafunzi kukosa chakula shuleni??

Je wazazi walishindwa kusomesha watoto primary au sekondary mpaka usiajiri madokta? Haya walimu nao vipi?? Mpaka leo wako nyumban na mashulen walimh wa sayansi hamna!!

Zahanati na hospitali hazina madokta alafu madokta wapo mtaani na kuajiri hutaki? Una akili wewe??
Kwa hivyo hapo ndio umemaliza kutoa ushauri nini kifanyike?
Hapo ndio mwisho wa kufikiri wa mtu mwenye akili timamu anaemkosoa asie kuwa na akili timamu?
Tuambie nini cha kufanya na tutatoa wapi pesa za kutekeleza hayo mawazo yako na hizo changamoto zingine tofauti na ajira kwa madaktari tunazitatuaje ili mambo yote muhimu yatekelezwe kwa wakati mmoja.
 
Fungua duka la dawa baridi utapinga mpunga tu, kwani lazima uajiriwe
Mtajiii?? Unajua mnavyosema fungua Duka la Dawa as if kuna mtaji.
Kukopa tu Bank mpaka uwe mfanyakazi au una kiwanja au Nyumba.
Yaani Ni Shiiiiiiidaaaaaaa!
 
Anaandika Daktari Mpya mtaani aliyemaliza mafunzo ya utaraji (internship) katika awamu ya Tano inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)

"Jina kubwa" kuliko wallet. Unakutana na classmate wako wa o level anakuita kiongozi, mkuu, kamanda na anaenda maili moja mbele anakuita " Daktari".

Meanwhile hauna kitu mfukoni zaidi ya nauli na maisha yako yamekuwa ya kuungaunga.
Hapo ndo unatamani kumziba mdomo. Unaanza kukumbuka jinsi ulivyokomaa miaka mingi sana shuleni ukijidanganya ukipata jina kubwa la "Daktari" pengine na pesa zingekuwa nyingi.

Ndipo unakumbuka hauna kitu zaidi ya ujuzi wa udaktari kichwani na mikononi na hauna sehemu ya angalau kuutumia huo ujuzi maana Serikali haiutambui uwepo wako. Unakumbuka jinsi wazee wa Muhimbili walivyokusotesha miaka 5+ kwa kile wanachokiita 'to satify the examiners' pamoja na kukuita 'The cream of The nation' huku wengine wakikuita 'mbuzi', 'mhuni' n.k

Unakumbuka ulivyovumilia matusi yote ukiamini ipo siku yatasahaulika.Naam sasa unaona matusi yale ya wazee wa MUHAS yalikuwa nafuu pale unapotafta angalau kijisehemu cha kujishikisha halafu mtu anakuambia atakuajiri na atakulipa bei sawa na mlinzi wa hospitali yake.

Unachukia sana ila hauna jinsi maana unakumbuka utokapo kwamba pengine usipofanya kitu kabisa wadogo na wazazi wako mambo hayaendi kabisa. Unaamua kutafuta kijiwe kingine na kingine ili angalau pamoja na kulipwa hela ya mlinzi majumlisho kwa hivyo vijiwe vitatu yaweze angalau kukidhi baadhi ya mahitaji yako ya msingi.

Masaa 24 daily uko kazini except siku ya ibada. Sehemu ya kulala ni kwenye daladala ukiwa unahama kijiwe kimoja kwenda kingine. Unakumbuka wimbo wa Kibaha School wa 'Struggle for success' unaamua kukomaa hadi itakavyothibitika vingine.

Pamoja na hayo...

Ndipo unakumbuka wenzio hawana vyeti na ni wakuu serikalini achilia mbali wenye vyeti feki. Tena wanapiga pesa na masaa yao ya kazi ni mawili kwa siku wanapata na muda wa kwenda gym. Wanalala kwenye mahekalu tena wakilindwa huku wewe unaegesha kwenye nyumba ya kupanga. Unaambiwa wanaishi hivyo maana ni waunga mkono juhudi za mamlaka toka juu!

Ndipo unaposema kwa ujasiri kama alivyosema mtu wa Mungu Musa "Ni heri kuteseka na watu wa Mungu/ Watanzania walio wengi kuliko kuitwa Mwana wa Binti Farao"

Eee Mwenyezi tusaidie.

Na Dr. Baraka Marco Nkondo.


My Take:
Serikali imeendelea kujificha kwenye kivuli cha uhakiki, kuwa kigezo cha kutoajiri wahitimu wapya.
Mleta maada muingo
 
Tuambie nini cha kufanya na tutatoa wapi pesa za kutekeleza hayo mawazo yako .

Hayo uliyoandika yote hayana maana, hoja iko hapa!!

Leo mnauliza mtapata wapi pesa kwani jk alipata wapi pesa? Nyie si ndio mnabana matumizi, sasa kama mnabana matumizi na kudhibiti ufisadi pesa zinaenda wapi?

Enzi za jk mnasema kulikua na wizi lakin enzi hizo ajira zilitolewa na watu walipandishwa madaraja, lakin enzi hizi mnasema hamna wizi je pesa mnapeleka wapi?? Maana ajira hamtoi, hamboreshi hali za watumishi yaani mpo mpo tu kila siku kuja na uhakiki uchwara!!

Ukipata majibu ya hayo maswali basi utakua umepata jibu lako!!
 
Mkubwa gani anaishi vijijini hata ndugu zao wakiumwa wanaletwa mjini. Hospitali nyingi za vijijini matabibu wao ni Nurse axillary wale wenye nguo za rangi ya kaki. Hao AMO utawakuta mjini au hospitali za dini (missionary hospital). Huku madaktari wenye degree wako mitaani, wamama wanakufa wakati wa kujifungua vijijini kwa kukosa huduma bora!! Shame!!
 
Wewe ndo huna info ndo maana nimekuuliza hiyo topic inafundishwa katika somo gani ili nielewe. Najua sylabus ya madaktari haina masomo ya hayo halafu wewe unauliza huko chuo hawakusoma. Jibu ni hawajasoma.
Entrepreneurship tunaisoma kwenye ds in second year ila haimpi ujuz wa kutosha kiasi cha mhitimu kujiajiri
 
Chuoni mlifundishwa ENTERPRENEURSHIP, kwahiyo usilalamike hapa.....SERIKALI Inapunguza Wage-Bill na sio kila Muhitimu lazima aajiriwe na serikali....OVa
Umeandika kama vile kichwani kumejaa vapour. Huyo anayepunguza wengine yeye mbona ameajiriwa?
 
Kuna AMO, CO ni ma cheap labors......serikali inapunguza Wage-Bill...Mshahara wa kumlipa Daktari wa Degree Serikali haina, kwahiyo Mvumilie tu.
Kwasasa tumejikita kwenye ununuzi wa ndege endeleeni kutuvumilia tukimaliza kununua ndege tunaanza kununua meli mwanza na kwengineko vumilieni tu ndio maisha tulioyachagua kwasasa
 
Mkipata muda sikilizeni hata wimbo Nash mc.

"Maisha baada ya chuo-Nash Mc"


Nchi sasa inakwenda kama kuku aliyekatwa kichwa.
 
Hayo uliyoandika yote hayana maana, hoja iko hapa!!

Leo mnauliza mtapata wapi pesa kwani jk alipata wapi pesa? Nyie si ndio mnabana matumizi, sasa kama mnabana matumizi na kudhibiti ufisadi pesa zinaenda wapi?

Enzi za jk mnasema kulikua na wizi lakin enzi hizo ajira zilitolewa na watu walipandishwa madaraja, lakin enzi hizi mnasema hamna wizi je pesa mnapeleka wapi?? Maana ajira hamtoi, hamboreshi hali za watumishi yaani mpo mpo tu kila siku kuja na uhakiki uchwara!!

Ukipata majibu ya hayo maswali basi utakua umepata jibu lako!!
Hata kichaa anaetembea bila nguo anaona uvaaji wa nguo hauna maana yoyote.
Mtoto mdogo anaekwepa kwenda shule haoni maana yoyote ya kwenda kusoma shule.

Lakini wewe kama una akili timamu huwezi kusema uvaaji nguo na kwenda kupata elimu shuleni havina maana yeyote. Wewe nakufananisha na huyo mtoto ambae hajui kitu lakini anahisi anajua kuliko wakubwa wake (eg. wazazi au walezi).

Sasa hoja yangu kama ulinifuatilia vizuri nimesema kwa vile mahitaji ni mengi sana kuliko mapato au makusanyo ya kodi hata kama utazidisha mara 2 au 3 ya makusanyo ya 2015/2016 ya serikali bado hazitatua matatizo yote muhimu kwa wakati mmoja.

Sasa unatakiwa kuweka vipaumbele vya kuigawa hiyo pesa uliyokusanya ili mambo mengi muhimu yatatuliwe. Na sio machache muhimu uyatatue kwa 100% lakini ukayaacha mengine mengi yenye umuhimu kama uliyotatua au yenye umuhimu zaidi.

Swali: Hapa unafanyeje sasa?
Jibu: Unapunguza kidogo kwenye bajeti ya kuajiri wafanyakazi wapya au unasitisha au unachelewesha kwa muda maboresho au nyongeza ya stahiki za wafanyakazi waliopo kazini kwa sasa na kuzichukua hizo pesa unaziongezea kidogo pesa za makusanyo yaliongezeka na kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba ambavyo vilikuwa vichache na duni miaka iliyopita ya awamu ya 4.

Serikali ilitakiwa ipunguze umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria na kurudisha miaka 55 kama zamani au kuishusha hadi miaka 50.
Hii ni ktk kutoa fursa ya ajira kwa vijana wapya wanaohitimu taaluma mbalimbali vyuoni.

Nahisi hapo katikati wazee wetu (huko CCM) walikuwa wabinafsi kujiongezea umri wa kustaafu. Wao walitakiwa wabaki kuwa washauri au expert fulani wenye mikataba ya mwaka mmoja mmoja ambao nafasi zao hakuna vijana wenye sifa za kuziba nafasi zao.

Wazee wameshapata uzoefu na mitaji ya kujiajiri na kuajiri vijana kwenye miradi/biashara zao. Wasaidie kuongeza nafasi za ajira na pato la taifa.
Hii pia itasaidia kumaliza hii mentality ya kutegemea kuajiriwa na serikali maisha yetu yote hadi uzeeni.


Hicho kitu cha kawaida sana duniani, sio kwamba unafanya austerity measures kamili lakini unachukua baadhi ya hizo hatua.

Ilikuwa serikali ina ajiri daktari kibao na waalimu wote wanaohitimu lakini wanafunzi wanakaa chini, wagonjwa wanakosa dawa hospitali za serikali. Au wagonjwa wanalala chini ktk mazingira hatarishi kwa kukosa vitanda.
Waalimu wengi lakini hakuna maabara n.k.

Tulikuwa tunakosa maji ya uhakika na masafi hata hapa jiji la Dar es Salaam, tukishambuliwa na kipindupindu mara kwa mara.

Angalia hapo chini jinsi bajeti ya madawa ilivyo ongezeka;
KUIMARIKA upatikanaji wa dawa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma nchini, kumeligusa shirika lisilo la kiserikali la Sikika na kubainisha kuwa limeridhishwa na hali ya sasa ya upatikanaji wa dawa nchini.

Aidha, limeishauri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuimarisha usimamizi na matumizi ya dawa. Katika mazungumzo ya watendaji wa Sikika wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Irene Kiria na wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari nchini, kwenye ofisini za shirika hilo Kinondoni, Dar es Salaam jana, kwa mujibu wa ufuatiliaji wa Sikika, upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutoa huduma umeongezeka.

Sikika kwa mujibu wa takwimu zao ilisema upatikanaji huo umeongezeka kutoka asilimia 56 mwaka jana hadi kufikia asilimia 81 mwaka huu. “Hiki ni kitu kikubwa ambacho hakijawahi kutokea kwa miaka mingi, kwamba kuna dawa kwa wingi na wananchi wanazipata kwa bei ileile, na kwa urahisi, hili ni jambo kubwa kwake (mwananchi),” alieleza Kiria katika mazungumzo hayo.

Kutokana na hilo, Sikika limeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua ilizochukua kuhusu hali ya upatikanaji wa dawa, na pia kufurahishwa na uamuzi wa serikali wa kupanga bajeti ya dawa na kuitekeleza kikamilifu kinyume cha miaka ya nyuma. “Tulilalamikia hilo kwa muda na tunafurahi kusema kwamba fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya dawa kwa mwaka wa fedha 2016/17 zilitolewa kwa kiasi kikubwa kulinganisha na miaka ya nyuma.

Hii imeiongezea MSD uwezo wa kuagiza na kununua dawa, na hivyo kuongeza upatikanaji wa baadhi ya dawa vituoni,” alieleza Kiria katika mazungumzo hayo ambayo wahariri pia walichangia mjadala huo.

Katika mwaka wa fedha wa 2016/17 serikali ilitenga bajeti ya dawa ya Sh bilioni 251 kutoka Sh bilioni 89 za mwaka 2015/16. Katika mwaka huu wa fedha ulioanza Julai Mosi, serikali imetenga fedha nyingi zaidi kwenye ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi ambapo Sh bilioni 236 zimetengwa kwa ajili hiyo.

Aidha, kwa mujibu wa Bohari ya Dawa (MSD), uanzishaji wa utaratibu wa kuagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji viwandani umepunguza gharama za dawa kati ya asilimia 15 hadi 80, hivyo kuongeza upatikanaji wa dawa vituoni kwa gharama nafuu.

Sikika pia ilipongeza uamuzi wa serikali wa kupunguza ukiritimba wa MSD, kwa kuwa sehemu pekee ambapo vituo vilitakiwa kununua dawa, baada ya sasa vituo vya huduma kuruhusiwa kununua dawa kutoka kwa wauzaji binafsi pindi zinapokosekana MSD. Kwa upande wao, wahariri katika mazungumzo hayo walieleza kuwa ni muhimu dawa zinazopelekwa vituoni zikawa ni zile zenye uhitaji kwa maeneo husika na kuwapo na udhibiti wa bei za dawa.
 
Back
Top Bottom