Kilio cha Madaktari wanaomaliza internship Awamu ya Tano

Kilio cha Madaktari wanaomaliza internship Awamu ya Tano

KAWETELE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2015
Posts
738
Reaction score
1,787
Anaandika Daktari Mpya mtaani aliyemaliza mafunzo ya utaraji (internship).

"Jina kubwa" kuliko wallet. Unakutana na classmate wako wa o level anakuita kiongozi, mkuu, kamanda na anaenda maili moja mbele anakuita " Daktari".

Meanwhile hauna kitu mfukoni zaidi ya nauli na maisha yako yamekuwa ya kuungaunga.
Hapo ndo unatamani kumziba mdomo. Unaanza kukumbuka jinsi ulivyokomaa miaka mingi sana shuleni ukijidanganya ukipata jina kubwa la "Daktari" pengine na pesa zingekuwa nyingi.

Ndipo unakumbuka hauna kitu zaidi ya ujuzi wa udaktari kichwani na mikononi na hauna sehemu ya angalau kuutumia huo ujuzi maana Serikali haiutambui uwepo wako. Unakumbuka jinsi wazee wa Muhimbili walivyokusotesha miaka 5+ kwa kile wanachokiita 'to satify the examiners' pamoja na kukuita 'The cream of The nation' huku wengine wakikuita 'mbuzi', 'mhuni' n.k

Unakumbuka ulivyovumilia matusi yote ukiamini ipo siku yatasahaulika.Naam sasa unaona matusi yale ya wazee wa MUHAS yalikuwa nafuu pale unapotafta angalau kijisehemu cha kujishikisha halafu mtu anakuambia atakuajiri na atakulipa bei sawa na mlinzi wa hospitali yake.

Unachukia sana ila hauna jinsi maana unakumbuka utokapo kwamba pengine usipofanya kitu kabisa wadogo na wazazi wako mambo hayaendi kabisa. Unaamua kutafuta kijiwe kingine na kingine ili angalau pamoja na kulipwa hela ya mlinzi majumlisho kwa hivyo vijiwe vitatu yaweze angalau kukidhi baadhi ya mahitaji yako ya msingi.

Masaa 24 daily uko kazini except siku ya ibada. Sehemu ya kulala ni kwenye daladala ukiwa unahama kijiwe kimoja kwenda kingine. Unakumbuka wimbo wa Kibaha School wa 'Struggle for success' unaamua kukomaa hadi itakavyothibitika vingine.

Pamoja na hayo...

Ndipo unakumbuka wenzio hawana vyeti na ni wakuu serikalini achilia mbali wenye vyeti feki. Tena wanapiga pesa na masaa yao ya kazi ni mawili kwa siku wanapata na muda wa kwenda gym. Wanalala kwenye mahekalu tena wakilindwa huku wewe unaegesha kwenye nyumba ya kupanga. Unaambiwa wanaishi hivyo maana ni waunga mkono juhudi za mamlaka toka juu!

Ndipo unaposema kwa ujasiri kama alivyosema mtu wa Mungu Musa "Ni heri kuteseka na watu wa Mungu/ Watanzania walio wengi kuliko kuitwa Mwana wa Binti Farao"

Eee Mwenyezi tusaidie.
 
Chuoni mlifundishwa ENTERPRENEURSHIP, kwahiyo usilalamike hapa.....SERIKALI Inapunguza Wage-Bill na sio kila Muhitimu lazima aajiriwe na serikali....OVa
Ungefikiria kidogo mkuu huyu ni daktari moja kati ya sekta zenye upungufu wa watalamu na kule kijijini bibi yako na wangu wanakosa hawa watu, na Dada zetu wanapoteza uhai wakati wa kujifungua kwa sababu zahanati haini daktari!
 
Kuna AMO, CO ni ma cheap labors......serikali inapunguza Wage-Bill...Mshahara wa kumlipa Daktari wa Degree Serikali haina, kwahiyo Mvumilie tu.
 
Ningelikua nimesomea udaktari wala nisingehangaika na kazi za serikalini, ninge base private sector au international posting tu botswana, namibia, zambia, canada kote huko lakini sababu akili za Watanzania ni ndogo hua hawapendi kutafuta maisha nje ya Tanzania basi wanalia lia kama huyu daktari uchwara
 
Kuna AMO, CO ni ma cheap labors......serikali inapunguza Wage-Bill...Mshahara wa kumlipa Daktari wa Degree Serikali haina, kwahiyo Mvumilie tu.
Hivi haujui kuwa AMO utawakuta wana mshahara mkubwa kuliko daktari anayeanza! Kama hujui, habari ndo hiyo!!! Uzoefu wa AMO unalipa
 
Tanzania kada za muhimu kama madaktari n.k zinadharaulika sana na umuhimu wake ni kama tissue paper unaithamini wakati una uhitaji nayo tu, ukimaliza shida zako unaiacha na hauikumbuki
 
Ningelikua nimesomea udaktari wala nisingehangaika na kazi za serikalini, ninge base private sector au international posting tu botswana, namibia, zambia, canada kote huko lakini sababu akili za Watanzania ni ndogo hua hawapendi kutafuta maisha nje ya Tanzania basi wanalia lia kama huyu daktari uchwara
Unajua condition za kwenda huko Botswana lazima uwe umefanya kazi serikalini na upewe kibali toka wizarani na tangu 2015 hivyo vibali havijatoka.
Na huyo si amesema yuko private sector au kaajiriwa na serikali huyo?
 
Hivi haujui kuwa AMO utawakuta wana mshahara mkubwa kuliko daktari anayeanza! Kama hujui, habari ndo hiyo!!! Uzoefu wa AMO unalipa
Hao ni waliopo kazini kitambo.....lakini kuajiri AMO na CO ni nafuu kuliko hawa wa Degree
 
Fungua duka la dawa baridi utapinga mpunga tu, kwani lazima uajiriwe
 
Back
Top Bottom