Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Duu huyo kijana umempata wapi, maana mimi nina vijana wawili wangalau wanakula kilo moja ya unga kwa siku.

Nilikuwa na vijana sita, walikuwa wapiga kg 30 kwa wiki. Bahati nzuri nilibakisha chakula msimu uliopita
 
Ni kilimo cha umwagiliaji, dharama inategemeana na zao unalotaka kulima alafu pia inategemeana na shamba linatumia maji ya mifereji au ni la kutumia pump

Kama unalima vitunguu shamba kukodi ni shi ngapi?
Iwe kwa ku pump maji au mfereji.
Na je heka moja vitunguu unapata gunia ngapi?
 
Mkuu ni mazao gani ulilima na ulilimia wapi, mbona gharama za nguvu kazi saidizi ni nafuu?
Mkuu nililima Dodoma na nililima mahindi. Mwaka huu kwa sababu ya njaa nguvu kazi bei imepungua palizi ni elfu nane kwa ekari au elfu mbili kwa robo ekari.
 
Hapa naona kama tunaingizana mjini. Kwa kawaida gharama ya tractor kwa walio wengi kwa heka ni 40-60 elfu. Halafu ulipaswa kutuambia ulilima zao ghani maana mbali ya maelezo yako mazuri huonyeshi ni zao gani ulilima na aina ya mbegu ndio maana naona kama unatudanganya. Pia hizo gharama zako za kulima hasa hao vibarua ziko chini sana kulinganisha na sehemu nyingi, au wewe ni mwalimu mkuu wa shule fulani hivyo unawatumia wanafunzi kukufanyia kwa bei hiyo?
Mkuu kwa hapa Dodoma bei ya kulima kwa trekta ndo hiyo , na nilima mahindi,.Kama wewe uamini endelea kufanya theoretical research ,'wakati sisi tunafanya practical research. Ubarikiwe sana.
 
Kwenye suala la trekta 25 elf inawezekana.
Kwenye vibarua, bado ninaweza kumuamini japo kwa shida.
Kwenye mbegu hapo mpaka atuambie kwanza ni zao gani na alilimia wapi?
Mkuu nililima mahindi aina ya Stuka huku Dodoma na hizo zilikuwa gharama za mwaka jana, mwaka huu palizi ni sh elfu nane kwa ekari au elfu mbili kwa robo ekari kwa ajili ya njaa ni kubwa sana huku mwaka huu.
 
Mkuu unapoamua kuwa mkulima maana yake sehemu kubwa ya nguvu kazi unatoa wewe mwenyewe na usaidizi uupate pale tu unapozidiwa. Tatizo kubwa la ninyi vijana ni kufanya kazi ya kilimo kama wewe ni mwajiri vile. Kwa mfano mimi mwaka jana nililima ekari 12@ekari sh 25,000 kwa trekta jumla laki tatu. mbegu za kupandia kila ekari mifuko mitano yaani 10kg each ekari, kila mfuko elfu sita. kwa hiyo kila ekari elfu30x12= 360.000/. kupanda nilipanda mwenyewe ekari nne na ekari nane niliweka watu kila ekari elf tano =40,000/. Kupalilia kila ekari sh 12,000x12x2= 280,000/, Gharama za kuvuna na kusoma laki sita. .Mapato nilipata magunia 230 nikauza gunia 210@ sh 90,000/ nikapata 18900000. Niliacha gunia 20 ambazo nimetumia mwaka huu kuwalipa nguvu kazi na matumizi binafsi.
N.B sikuweka mbolea ya viwandani mimi shamba langu huwa naweka samadi mara moja kila baada ya miaka mitatu. Angalia mapato na matumizi majibu unayo mwenyewe.
Wewe unalimia mdomo.:p
Hulijui shamba.
 
Hivi unafahamu matajiri wakubwa wa nchi hii ni wakulima !!???
Duniani unafahamu wenye pesa ni wakulima!?
Usilolijua usilicrash hata hao viongoz wako wa serikali ni wakulima ,you cant see if you aint trained to see,jifunze sasa na tazama utapata majibu .
Sema kilimo unatakiwa uwe na mahesabu makali na usitegemee faida za siku mbili lazima ufanye kazi kweli ya kueleweka ,only msimu huu unaoishi moshi mile sita (rambo mferejini) somebody kalima 16 acres za nyanya kwa gharama ya million 50 na ushee ,kavuna more than million 700 ni investment kubwa but alitupa fedha nyingi na imerudi kwa faida ya ajabu huo mfano mdogo sana ,ukianza kilimo dont start with acre 10 nop anza na nusu eka au moja jifunze mazuri na changamoto than add more land utaona kilimo kilivyovyema ,wakulima ambao hawaendelei ni wale ambao wao wanafanya kilimo mazoea lazima ufahamu kilimo ni science utafanikiwa
Unasemea yule jamaa aliyelima nyanya pale nje ya sevia??
 
Nataka kulima hekari mbili za vitunguu mwaka huu,,wapi kwenye ardhi nzur washkaji nije niweke kambi hapo???
 
hivi kwanini nyie wakulima huwa mnapoleta mafanikio yenu mnapenda sana kuwataja kwa kebehi vijana wanaotafuta ajira...?

na kwa nini uamini sehemu pekee ya kupata faida ni kilimo pekee, na wala sio shughuli zingine,mfano uchimbaji wa madini, uvuvi, biashara n.k...

kingine jarbu kufikilia kila mwaka kuna waitumu zaidi ya laki moja hao ni graduate, bado kuna vijana wa diploma na form six leaver wale wanaoshindwa kuendelea na masomo, Wote hao waende kwenye kilimo kama unavyoelekeza...!wewe unadhani utapata hyo faida ya m3., au utamuuzia nani??
 
Mtanzania akifanikiwa huwa anakaa kimya ili aendelee kupiga hela mwenyewe na baadaye aonekane wa maana kuliko wengine. Ukimsikia m'bongo analeta ngonjera za hivi ujue anafanya utafiti, nia na madhumuni anataka asikie wengine wanasema nini kuhusu wazo lake.
 
Ni kweli usemayo mkuu, lakini mbona wakulima ndio jamii masikini kabisa humu nchini kama kweli inalipa kihivyo?
kua mkulima na kufanikiwa kupitia kilimo ni vitu viwili tofauti sana na usije kuvichanganya tena kiongozi
 
Kilimo??? Yaani ulinganishe na ajira? Hata kama napata laki 5 kwa mwezi wacha iwe hivyo. Kilimo hakitabiriki ingawa kweli ukkibahatisha unatoka, lakini pia ujiandae kutoka mrisi! Niliingiwa tamaa ya kulima matikiti maji, nikazamisha kama 2.5m (ikijumuisha na ununuzi wa shamba ekari 32). Nikakata kipande kama ekari moja nikalima hayo matikiti maji nikawa napiga hesabu ya kupiga hela si chini ya 5m, kwani niliambulia kitu? Kumbe timing yangu ilikuwa mbovu sokoni kukawa na matikiti kibao na pia timing ya kulima kumbe ilikuwa mbaya mengi yakabaki shambani maana hayakufikia mwisho wa kukomaa! Nashukuru tu nilibaki na shamba ndo faida yangu, sasa hivi ndo napanga nibadili kilimo nifanye ukulima wa samaki,, ha ha ha haaaa (nifuge samaki) maana liko karibu na mto usiokauka (Mto Ruchugi - Kasulu). Mtu hawezi tena kunidanganya eti niache kazi ya mshahara nikabobee kwenye kilimo. Na hiyo kazi ambayo mleta mada anaisema ya laki 5, hiyo si ni ya mtu wa diploma? Bora upige vyote (kilimo na ajira) hapo maisha yataenda!!
hahahahaha angalia usije fuga hao samaki nao wakadumaa
 
Wewe unalimia mdomo.:p
Hulijui shamba.
Ha ha haaaaaa, mkuu umenikumbusha jamaa yetu mmoja alikuwa analimia mdomo kwamba mwakani nitalima ekari 5 za mpunga kila ekari nitavuna magunia 30 hivyo nitakuwa na maguni 150 ya mpunga. Hapo nitakuwa nimetoka kimaisha!! mwaka ukafika hata nusu ekari hana msimu wa kilimo ukaisha tusione hata shina moja la mpunga jamaa akabaki anatutishia kutupiga tu kila tukimkumbusha!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom