mwakijembe
JF-Expert Member
- Mar 20, 2017
- 1,638
- 2,293
Yaani watu wanapotishana kwenye mitandao humu,toa mchanganuo ulilima wapi,kilimo cha kutegemea mvua au kumwagilia,ulipata jumla ya gunia au tani ngapi na uliuza kwa bei gani??,mimi pia ni mkulima wa mahindi nzuri tu ila kwa hekali 2 ukapata mil3 ,mmmhhhh?!???
Nakuambia wewe acha tu huku mitandaoni. Nilijaribu kuingia kwenye kilimo nikawekeza vya kutosha. Kila siku nikawa nawaaga wafanyakazi wenzangu kwamba huu ni mwaka wa mwisho kuwa ofisini. Nilichokipata huko kwenye kilimo ni Mungu tu anajua. Asikudanganye mtu, ni bora ubaki kwenye ajira hata kama unatukanwa kuliko kujichanganya kwenye kilimo kwa hizi hadithi za mitandaoni. Kilimo ni wito sio kitu cha mchezo.