Kilimo cha Bamia: Fahamu kuhusu mbegu bora, mazingira sahihi ya kulima, magonjwa na namna ya kuyakabili

Mkuu hongera kwa aidia nzuri sana,

ninavyo fahamu kuhusu bamia kwa sasa soko lake ni kuuza kwenye masoko yandani kama kariakoo na kwingineko.

Ila kama utaweza kupaki freshi unaweza kju export kwenye soko la ulaya kuna demand ila kumeet standardzao c kitu cha mchezo.

toa ufafanuzi kidogo
 
Habari wadau, natamani sana kulima Bamia ila sijui hali yake kisoko. Naomba ushauri wenu ndugu zangu.

Na ikiwa unalo wazo mbadala la zao zuri la kilimo linalokomaa na kuuzika kwa mda mfupi usisite kunishauri.
 
Bamia ni kama zao jingine lolote la mboga mboga au mazao yatokanayo na kilimo. Nitachangia kuhusu bei.Popote ulipo soma ni kipindi gani wazalishaji huwa wachache kwa zao hilo,zalisha kipindi hicho.

Bamia ni zao rahisi kwa kanuni na gharama,ukilizalisha wakati sahihi utafurahia mno mapato yake ukikosea msimuwa kuzalisha utakichukia kilimo.

Kuhusu magonjwa yaliyotajwa maafisa kilimo au wauzaji wa pembejeo wenye taaluma ya kilimo watakupa maelezo kamili ila dawa zote zinazozuwia na kutibu ubwili unga zinazuwia na kutibu magonjwa hayo ukichanganya na viatilifu vinavyozuwia wadudu.

Kilimo ni biashara kuna maswali hayawezi kujibiwa hapa ,uliyedhamiria tafuta habari kuhusu zao husika na masoko yake. Zikitajwaa humu habari za masoko na mtindo wa wetu wa kuigana biashara itaharibika kwa mazao kufurika.
 
wiki mbili zilizopita sokoni Tandika, kiroba cha ndoo sita kilikua kati ya 55000-80000 Tsh inategemea na wingi wa bidhaa husika sokoni,
mbegu kopo kubwa kwa kariakoo ni 16000,
baada ya kumaliza kupanda nitarejea na mrejesho wa kiasi gani kinafaa kwa heka moja.
 
Faizafoxy huko mkuranga yanapatikana Mashamba ya kukodi? Na kukodi ni shilling ngapi kwa heka moja?
 
Faizafoxy huko mkuranga yanapatikana Mashamba ya kukodi? Na kukodi ni shilling ngapi kwa heka moja?
Kwa mwaka 2014 nakumbuka ekari 1 ilikuwa 50,000 hadi 70,000 kijiji kinaitwa malela.

kabla hujafika mkuranga kunakijiji kinaitwa vikindu hapo unaenda kushoto utakutana na kijiji cha vianzi, mbele yake ndio kunahicho kijiji cha malela

Ardhi yake inarutuba nzuri na maji yapo mwaka mzima, hivyo kunafaa Kwa kilimo cha umwagiliaji

Wanalima sana tikiti, mbogamboga, matango na mpunga
 
mimi ninalo shamba la kuuza kabisa lifaa kwa bamia Ufuta na Mihogo ni mkuranga pia Kijiji Hoyoyo nitafute 0655841348 na ukitaka kwa ajili ya ufugaji wa SAMAKI pia ninalo KISEMVELE siitaji Darali
 
Mimi nalima kama mboga za nyumbani,inanaisaidia kweli najipanga kulima kama zao la biashara
 
Habarini Wakuu,

Baada ya kuona nina kila sababu ya kuongeza kipato changu, nimefikiri na kugundua nahitaji kuwekeza katika kilimo cha bamia kwa sasa.

Na kwa kuwa JF ina watu makini na hodari katika nyanja mbalimbali basi mtanisaidia kimbinu,ushauri na maarifa ili kufanikisha hii plan yangu.

Kwa kuanzia nina eneo la ekari 2 na visima viwili vyenye maji ya kutosha nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.

Kimsingi nimekamilisha maandalizi mengi ya awali kwa ajili ya kuanza kilimo cha umwagiliaji,kwani pamoja na kuwa na maji ya kutosha lakini pia nimenunua pump na nina mbolea ya samadi tayari.

Yote kwa yote naomba mnijuze,

~ni aina gani ya mbegu inafaa zaidi na inayotumia muda mfupi toka kupanda hadi mavuno na yenye soko zuri.

~changamoto zipi nijiandae kukabiliana nazo katika kilimo hiki.

~dawa zipi zinahitajika magonjwa na wadudu wakianza kushambulia mimea.

Ni hayo tu,natumai kupata mawazo yenu wakuu ili nijue kipi napaswa kufanya.
 
Hongera ndugu kwa hatua kubwa uliopiga, mambo ya kuzingatia katika kilimo:-
1. Fanya uchunguzi juu ya soko la zao lolote kabla ya kulilima, hii itakusaidia kuangalia matazamio ya faida. Wengi huwa tunakosea tunaanza kulima then tunakuja kutafuta soko usifanye kosa hilo.

2. Andaa pembeje za kilimo unachotaka kukifanya (mbegu, madawa) na pesa ya dharula. Mimi ningekushauri ununue mbegu za kampuni hizi mbili PV Holland na Royal na ulime nusu heka kampuni moja na nusu nyingine kampuni nyingine. Sababu kubwa ya kukwambia hivi hii itakusaidia na kukupa uhakika ni aina gani ni nzuri na bora kuliko nyingine, ninamaana hapa wewe mwenyewe utajua mbegu gani inawahi kuzaa mapema, mbegu gani haishambuliwi na magonjwa na nimbegu gani utaichuma kwa muda mrefu wakati wa kuvuna, hii muhimu sana kuweka kumbukumbu ya kuandika siku ulipopanda.

3. Ingia kwenye kilimo sasa sana uwe unachunguz a mazao yako mara kwa mara maranyingi dawa hupuliziwa kila baada ya wiki 2, inategemea na geographia ya eneo husika.

4. Naamini ukizingatia hayo utafanya vizuri utakapo lima awamu yapili kwasababu utakuwa umepata uzoefu wa kilimo na changamoto ulizopitia. Bamia kupanda hadi kuanza mavuno ni siku 45 mpaka 60.

Nisikuchoshe na maelezo marefu mimi pia najifunza naamini wapo wengine wajuzi zaidi watajazia au kurekebisha pale nilipokosea.

Nakutakia kila lakheri na mafanikio.

Sent from my LG-H635 using JamiiForums mobile app
 
wiki mbili zilizopita sokoni Tandika, kiroba cha ndoo sita kilikua kati ya 55000-80000 Tsh inategemea na wingi wa bidhaa husika sokoni,
mbegu kopo kubwa kwa kariakoo ni 16000,
baada ya kumaliza kupanda nitarejea na mrejesho wa kiasi gani kinafaa kwa heka moja.
Mkuu Hornet hali vipi? Mrejesho please. Mambo yaliendaje...!
 
Back
Top Bottom