Kilimo: Miti aina ya mifudufudu

Kilimo: Miti aina ya mifudufudu

kanyagio

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2009
Posts
1,021
Reaction score
373
siku chache zilizopita nilienda pale Balton (njia ya Coca cola Dar) kufuatilia agricultural inputs mbalimbali, bahati nzuri nilikutana na mzee mmoja ambaye tuliongea mengi sana. Mojawapo ya kssue tuliyoongea ni upandaji wa miti kibiashara- yeye alinieleza kuwa anapanda miti aina ya mifudufudu kwa kitaalamu unaitwa Gmelina Arhobea (white teak). maelezo yake yapo hapa http://www.winrock.org/fnrm/factnet/factpub/FACTSH/Gmelina%20arborea1.pdf

yeye amesema ni miti mizuri na inakubali ukanda wa Pwani.. kama unataka kuiona fika Bagamoyo mjini maeneo ya petrol station , mkono wa kulia kuna kanisa la lutheran (KKKT) na hapo hapo kanisani kuna kitalu cha miti.. kwenye hicho kitalu kuna mifudufudu mikubwa ambayo ina diameter isiyopungua 1meter (ipo tayari kuvunwa).-- in fact nimeshaenda Bagamoyo kwa ajili ya kuona hiyo miti- nimeiona na inavutia sana!!

Alisema miti hii matumizi yake ni mbao na inakuwa tayari kuvuna baada ya miaka 10-12. miti hii inanyoooka vizuri sana kama utakuwa umefanya prunning vizuri na umepanda miche iliyonyooka vizuri.

nimewapigia wakala wa mbegu Morogoro wamenihakikishia kuwa kweli miti hiyo inalimwa kwa ajili ya mbao na kilimo mseto na bei ya kilo moja yenye mbegu zipatazo 1200 ni Tsh 7500. aidha wamesema, ukipanda mbegu hizi zinakuwa tayari kwenda shambani zikifia urefu wa sm 30-45. ila kumbuka mizizi isishike sana chini na ikishika chini lazima ukate mizizi kwa kisu kikali na uiache hapo kwenye kitalu ili ipone vidonda. ukishafanya hivyo miche mingi itapona ukiipeleka shambani. kumbuka kuipanda wakati wa mvua!!

Je kuna mtu ambaye amejishughulisha na upandaji wa miti hii ili tubadilishane taarifa, mawazo na uzoefu?
 
inaonyesha kama ni ishu nzuri hii ngoja niifanyie kazi mkuu
 
wazo zuri.Napenda sana kupanda miti hasa kwa ajili ya mbao ila ishu inakuja kwenye eneo
,kuotesha miti ya kutosha kunahitaji eneo la kutosha
 
Mkuu inaelekea umeshafanya kautafiti kadogo, unaweza kutujuza inahitajika care ya aina gani kwenye ukuzaji? Nami niko interested kujua ABC za hii kitu, ningependa pia kujua ni soft au hard wood?
 
wazo zuri.Napenda sana kupanda miti hasa kwa ajili ya mbao ila ishu inakuja kwenye eneo
,kuotesha miti ya kutosha kunahitaji eneo la kutosha

Mbona hujasema tukusaidie kujua sehemu za kupanda miti dada Ney? Kuna thread iko humu imesheheni mambo hayo.
 
Mafinga kuna maeneo ya kutosha wewe tuu na ela zako,nataka pata kama eka mia pale kwa kuanzia.
Ila kuna miti pale mafing wanapanda in 3 years time unavuna
 
Mafinga kuna maeneo ya kutosha wewe tuu na ela zako,nataka pata kama eka mia pale kwa kuanzia.
Ila kuna miti pale mafing wanapanda in 3 years time unavuna

njowepo, ni mafinga vijiji gani hivyo mkuu. na ni miti gani ya kuvuna ndani ya miaka 3 (inanitia wasiwasi) au unavuna milingoti?
 
njowepo, ni mafinga vijiji gani hivyo mkuu. na ni miti gani ya kuvuna ndani ya miaka 3 (inanitia wasiwasi) au unavuna milingoti?[/QUOTE]

Hapo pekundu,ungeuliza kama jamaa anavuna boriti/poles/fito za mlingoti. Hata mimi nina shaka juu ya umri huo, ila kwa fito za kujengea sehemu za starehe kama baa inawezekana kuvuna baada ya miaka 4, mara nyingi nimekutana na malori yakiwa yamepakia fito toka Iringa kuja Dar kwa ajili ya ujenzi wa viwanja vya starehe.

Ukienda Uchindile au Kilosa ya Mufindi unaweza kupata ardhi ya bure, ila ni namna gani uende huko, ni mziki mzito huo. Au ukienda Kimara Kilolo, kuna ardhi hadi basi,ila uendaji huko ni hatari. Ukienda Magome Kilolo, kuna misitu ya bure ya kununua ila kuna mteremko mmoja hivi ni hatari, ukiumaliza inabidi upumzike kidogo gari lipoe.

Ila msiogope, huo ndio utafutaji wa halali na haki kabisa.
 
Kanyagio inawezekana kwa miaka mitatu mfano kwa miti aina ya PINE inakua upesi sana hii hususani kwa kutengeneza karatasi na viberiti
 
Sijawahi kusikia jina la miti inayoitwa "mifudufudu" ila kutokana na jina lake kwa kiingereza, "white teak" inawezekana ikawa ni jamii ya mitiki, kwani mitiki huitwa "teak", ambayo nafikiri kiswahili kilitohoa jina na kuiita "mitiki". Hata hivyo, kwa lugwa ya kitaalamu mitiki huitwa "tectona grandis" kwa hiyo inawezekana nikawa siko sahihi kwani ni tofauti na "Gmelina Arhobea", ambayo inajadilikwa kwenye hii thread.

Nawasilisha.
 
Kanyagio inawezekana kwa miaka mitatu mfano kwa miti aina ya PINE inakua upesi sana hii hususani kwa kutengeneza karatasi na viberiti

Miti kwa ajili ya pulp ambayo data zake zinasemekana zipo,japokuwa vituoni hazipatikani ni miaka nane. Miche/mbegu ya miaka nane iko mingi huko Mbeya/njombe imepandwa, ila kwa miaka 3 bado,japokuwa huko duniani inawezekana. Tatizo ukiwa na miti hiyo soko lake kwa karatasi/viberiti lipo? kwa sababu pines za Mufindi hazina soko, nadhani SPM wameshafulia.

New forest wa UK walitaka kuanza project ya pine ya miaka 8 pale wilayani kilolo Iringa, lakini imeshindikana,japokuwa walishaomba hata eneo la kufanyia mradi.
 
jamani kuna yeyote ameshafanyia utafiti kilimo cha miti ya mifudufudu? yaweza stawi Kisarawe, Pwani?
 
Back
Top Bottom