Kilimo kinaenda wapi?

Jodeo

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
1,286
1,328
Habari ndugu?

Kwa muda mrefu Nimekuwa nikijiuliza kwa nini shule zinazofundisha somo la kilimo zimepungua sana na ni kwa nini? Sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu inategemea kilimo, na ndiyo sector inayoajiri watu wengi zaidi ( more than 80% directly wanategemea kilimo).

Nikakumbuka: Shule Karibu zote zilizofundisha kilimo (za serikali, yule mkenya alizitowesha kabisa kwa kufuta somo hilo)

Awali sector ya kilimo huwa kubwa sana kabla ya viwanda kukua , na baadae sector hii uwezesha sector ya viwanda kukua.

Sasa ninajiuliza wataalamu wa kilimo wenye basics za kilimo watatoka wapi kwa hali ya sasa tuliyonayo? Na hivyo viwanda tunaviendeaje kwa kilimo hiki goigoi?!

Huu uti wa mgongo wa taifa unaenda kombo! Serikali fungua macho yako rudisha somo la kilimo kwa kasi ikupasayo, tena ikibidi liwekwe na shule binafsi.
Hatuwezi kusema eti "uti wa mgongo" ...ilihali uti huo umeachwa ujipindie wenyewe!

Kama tusipoupa fimbo ya kusimamai hakika huo uti wa mgongo utaangunga na kufika chini kabisa, nasi hatutakuwa salama. KWAHERI
 
Naamini sana katika kilimo.

Dunia inakwenda kwenye thrd stage ya agricultural revolution.
Agritech, hata yakirudi hayo masomo lzm mitaala iwe reviewed,
Iwe ni mitaala inayomuwezesha mwanafuzi ht akitoka shule na sufuri awe na uwezo Wa kulima ngogwe kitaalamu na kujikomboa.
 
Nafikiri hapa tulipo, kilimo kiunganishwe tu na viwanda basi.Sema viwanda vinategemea pia miundo mbinu kama reli, bandari pamoja na nishati ya umeme. Lakini kwa kuanzia serikali iruhusu kilimo hasa kilimo cha chakula kuwa biashara.
 
kufuta hii kitu lilikuwa kosa kubwa. watu weusi inabidi tutawaliwe tena.
 
Back
Top Bottom