Kilimo cha vitunguu maji

Kilimo cha vitunguu maji

Mnaweka nini kwenye vitunguu maji..... Vitunguu maji tukiwa tunapika jikoni havina harufu, havitoi machozi..... Havina ladha kabisa Au ni GMO pia??
Mmmh ww unanunua wapi hvo vitunguu mkuu...
 
Hii mada nzuri sana. Hakika nitaweka kambi hapa. Ila nilichogundua baada ya kusoma threads nyingi za wakulima tofauti tofauti ni kuwa mtu hasemi kilichomfelisha shambani, anakimbilia kukukatisha tamaa tu kuwa zao fulani ni gumu sana . Ninachoomba wadau tuseme ni chanagamoto gani ulikutana nazo mpaka ukafeli shambani? Kwasababu kwa mfano watu wengi wanasema kitunguu ni kigumu sana kulima. Ugumu wake uko wapi? Changamoto zake zipoje? Tusaidiane wadau tuondokane na hili dimbwi la umasikini kupitia kilimo na inawezakana kabisa.
Kitunguu maji ni zao ambalo watu wengi wanalikimbilia ila si zao rahisi kama wanavyofikifikiria...ni zao gumu na linahitaji usimamizi makini kuanzia vitalu mpaka kuvuna.

Kama huna muda wa kukaa shambani nakushauri usililime hiki zao maana litakufelisha vibaya sana.

Changamoto kubwa za shambani ni hali ya hewa na udongo.

Kitunguu ni zao linaloathiriwa sana na mabadiliko ya hali ya hewa, jua likiwa kali sana ni tatizo na baridi likizidi sana pia ni tatizo....kifupi kitahitaji hali ya hewa ya wastani kuweza kustawi na kukuva mavuno.

Kitunguu kinapenda hali ya ukame hivyo mvua nyingi au maji yanayotuama pia ni tatizo.

Kitunguu kinastawi vizuri ktk udongo ambao una mchanganyiko wa tifutifu na kichanga....Udongo mgumu wa mfinyanzi haufai kwa kitunguu kwani unatuamisha maji kwa muda mrefu na kichanga kabisa pia hakifai kwani hakishiki maji na wakati wa jua kali kinachoma vitunguu na pia upotevu wa virutubisho huwa mkubwa.

Changamoto nyingine ni kuwa kitunguu maji kinapenda maji...yaani unyevu wa kutosha katika ukuaji wake wote hivyo hakikisha eneo unalotaka kulima lina maji ya kutosha.

Changamoto nyingine ni ya magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu.
-Kitunguu kinaathiriwa na magonjwa mengi ya fangasi kama Downy mildew, Purple blotch, stemphillium blight, (soft,pink and neck rot), tip burn,botrytis leaf blight,damping off n.k)..hivyo unatakiwa uwe na elimu ya kutosha kuyajua magonjwa na vipi utakabiliana nayo.

Pia wadudu wasumbufu kama vithiripi (thrips) , Red and black spider mites (utitiri mwekundu na mweusi), leaf hoppers (mbilizi) pamoja na leaf miners... unatakiwa ujue unakabiliana nao vp.

Changamoto nyingine ni mtaji...kitunguu kinataka pesa iwe mfuko wa shati ili ulihudumie shamba kwa wakati, dawa upige kwa wakati, mbolea uweke kwa wakati na maji umwagilie kwa wakati.

Mwisho changamoto nyingine ipo kwenye masoko....bei hubadilika badilika kutegemeana na uzalishaji wa mwaka husika na pia kipindi gani umelima...Kiangazi changamoto za magonjwa ya ukungu hupungua, wadudu huwa wengi ila mavuno nayo huwa ni makubwa tofauti na kipindi cha mvua....Bei za chini hushuka mpk sh 70000 kwa gunia ya kilo 100 na huweza kupanda kufika hadi 400,000.
 
Hivi vitunguu soko lake ni uhakika?
 
Hivi vitunguu soko lake ni uhakika?
soko lake linabadilika badilika....hupanda ghafla na kushuka ghafla kutegemeana na wingi wa bidhaa masokoni. Leo inaweza kuwa laki baada ya wiki mbili bei ikalipuka kufika hata laki 2 kwa gunia..na pia unaweza kuona bei ni laki 2 baada ya wiki mbili ukasikia bei ni elfu themanini...
 
Namaanisha kwamba mtu anaweza kuja kuchukua mzigo wote au ndio mambo ya gunia mojamoja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom