MJADALA: Maswali, majibu na ushauri kuhusu Kilimo cha Mpunga cha kitaalam pamoja na masoko yake

kuhusu kulima mpunga Ndiyo kwanza naanza sijawahi lima sehemu nyingine , na maeneo ni kijiji cha namawala, sitakuwa full time shamba lakini naplan kuwa na visit mara mbili kwa mwezi

Kama usimamizi ni wa remote control kama unavyoonyesha basi inatakiwa uwe na mtu / meneja ambaye atakuwepo muda wote shambani. Kitu kingine kwenye labour ume understimate sana kwani uvunaji unahitaji watu wengi. Angalizo muhimu, kama unapanga kulima sehemu za Mtimbila au Malinyi wakati wa kuvuna watu wa kuvuna ni wachache sana unaweza ukahitaji kutafuta watu kutoka Shinyanga au Kigoma. Mbona hakuna gharama za kuhifadhi (storage)?
 
kuhusu kulima mpunga Ndiyo kwanza naanza sijawahi lima sehemu nyingine , na maeneo ni kijiji cha namawala, sitakuwa full time shamba lakini naplan kuwa na visit mara mbili kwa mwezi

Kwanza nakupongeza kwa kuchagua eneo zuri maana kata ya idete ni nzuri kwa utoaji wa mpunga!

Tahadhari:
1.Inaonekana huna uzoefu nakilimo cha mpunga,ningekushaur upate msimamiz ambaye anauzoefu na ambaye unamwamini vya kutosha

2. Ekari 50 ni project kubwa sana kwa mtu anayeanza,ningekushaur uanze na 25 ekari ili ujifunze vya kutosha ili mwakani unaweza kulima 50 au mia kabisa. Maana uzoefu unaonyesha ni wachache sana wanaofanikisha safari ya kwanza ivo ni bora uanze kidogokidogo

Ukitaka maelezo zaid ni pm nikupe mwenyeji wa namawala ambaye yuko dar anaweza kukushaur zaidim

Nakutakia kila la kheri
 
Kama usimamizi ni wa remote control kama unavyoonyesha basi inatakiwa uwe na mtu / meneja ambaye atakuwepo muda wote shambani. Kitu kingine kwenye labour ume understimate sana kwani uvunaji unahitaji watu wengi. Angalizo muhimu, kama unapanga kulima sehemu za Mtimbila au Malinyi wakati wa kuvuna watu wa kuvuna ni wachache sana unaweza ukahitaji kutafuta watu kutoka Shinyanga au Kigoma. Mbona hakuna gharama za kuhifadhi (storage)?

Asante kwa ushauri wako, ghalama za kuhifadhi kwa miezi sita ni km sh 2,000 kwa gunia ongeza kwenye ghalama
 
Ila inabidi ujitahidi sana kwenye timing ama upate eneo ambalo lipo karibu na mto so that maji yasiwe changamoto sana maana kama wenyeji wakikupeleka mbali na vyanzo vya maji na mvua zenyewe zikawa za kusua sua itakula kwako so be carefully with areas selection, all da best.
 
chodoo,
Kuna rafiki yangu alikwenda huko ifakara somewhere called Mkula kwa minajili ya kujishuhulisha na kilimo cha mpunga na miwa kama unavyojielezea wewe hapa....lakini kilichofuatia ni kuzama kwenye mapenzi na ngono zembe na akajikuta anajaza vibinti mimba ingali huku Dar ameacha mke na mtoto mmoja. Alihishi hapo Mkula zaidi ya miaka 7 na amerudi Dar.

kwa usafiri wa Fuso tena kwa msaada. So i wish u all the best,ila usisahau kinachokupeleka huko! vinginevyo yatakupata.

ya Abubakary Masolwa....watch out
 
Pongezi sana, ila nakushauri manager wako wa shamba awe mtu wa eneo hilo, yeye ndo anajua vijana wanaojituma, hata wakipewa hela wakapotea anajua sehemu ya kuwapata, usalama wa shamba na mali zake n.k
 
Chodoo,

Kwenye hayo mahesabu kuna contingency? what if mvua haikunyesha? what if mvua ikapitiliza ikanyesha kipindi haitakiwi?

Tuwekee what ifs halafu utupe projections ambazo ni pessimisstic ili tuelewe hali halisi
 
Kuna rafiki yangu alikwenda huko ifakara somewhere called Mkula kwa minajili ya kujishuhulisha na kilimo cha mpunga na
miwa kama unavyojielezea wewe hapa....lakini kilichofuatia ni kuzama kwenye mapenzi na ngono zembe na akajikuta ana
jaza vibinti mimba ingali huku Dar ameacha mke na mtoto mmoja. Alihishi hapo Mkula zaidi ya miaka 7 na amerudi Dar
kwa usafiri wa Fuso tena kwa msaada. So i wish u all the best,ila usisahau kinachokupeleka huko! vinginevyo yatakupata
ya Abubakary Masolwa....watch out

LOL

You made my day bro
 
Kama usimamizi ni wa remote control kama unavyoonyesha basi inatakiwa uwe na mtu / meneja ambaye atakuwepo muda wote shambani. Kitu kingine kwenye labour ume understimate sana kwani uvunaji unahitaji watu wengi. Angalizo muhimu, kama unapanga kulima sehemu za Mtimbila au Malinyi wakati wa kuvuna watu wa kuvuna ni wachache sana unaweza ukahitaji kutafuta watu kutoka Shinyanga au Kigoma. Mbona hakuna gharama za kuhifadhi (storage)?

Labda uwe karibu na mto ili umwagilie. Nimelima eka 20 za mpunga, ulipoanza kuchanua mvua ikakoma, ni hasara 100%. Kama ni wa maji ya mito, kila la heri
 
Ila inabidi ujitahidi sana kwenye timing ama upate eneo ambalo lipo karibu na mto so that maji yasiwe changamoto sana maana kama wenyeji wakikupeleka mbali na vyanzo vya maji na mvua zenyewe zikawa za kusua sua itakula kwako so be carefully with areas selection, all da best.
Najaribu kulifanyia kazi wazo lako ingawaje likikosekana itabidi tu ni take risk, kuna mtaalamu wa mpunga ambaye tutaenda naye kuangalia maeneo ambayo yanafaa
 
Chodoo,

Kwenye hayo mahesabu kuna contingency? what if mvua haikunyesha? what if mvua ikapitiliza ikanyesha kipindi haitakiwi?

Tuwekee what ifs halafu utupe projections ambazo ni pessimisstic ili tuelewe hali halisi
kweli tutategemea sana mvua na tunarisk kwa sehemu so hizo what if we can't answer them, tunajitahidi kufanya Yale tuyawezayo tu
 
pongezi sana, ila nakushauri manager wako wa shamba awe mtu wa eneo hilo, yeye ndo anajua vijana wanaojituma, hata wakipewa hela wakapotea anajua sehemu ya kuwapata, usalama wa shamba na mali zake n.k
mwenyeji atakuwepo na mtu mwingine ambaye watasaidiana
 
jipange jipange tena sana kwa maana ninavyoujua mpunga si mchezo...na usisahau wa kupandikiza ndio safi na nakushauri usiuze mpunga unachotakiwa ukishavuna unutoa mzigo wako shamba unauleta ifakara mjini kunu magodauni unahifadhi mpunga wako baada ya hiyo miezi sita unakoboa hapo hapo godaun kuna mashine. Unauza mchele...au kama unajua soko zuri unasafirisha mwenyewe....
 
kwa kweli najaribu sana kujipanga vizuri ili niweze kufanya vizuri, kuhusu kuuza mpunga au mchele itategemea kipi nitakiona kina tija kwa wakati husika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom