Future Billionaire
Member
- Feb 3, 2015
- 45
- 9
As ante sana mkuu
Nashukuru mama porojo, umenifungua macho hapa
Hata mimi nilishawahi sikia tetesi juu ya uyaongeleayo mkuu,ngoja waje wadau kama kina Malila watatoa elimu ya uhakika hapa
Mkuu nimepata wito wako,
Mitiki inahitaji uangalifu sana, ni lazima kufanya utafiti wa kutosha kwenye udongo na hali ya hewa ya eneo husika kabla ya kuotesha miti. Fanya utafiti kwenye soko la ndani kama lipo ili usije ukaanza kulalamika huko mbeleni, pia angalia scale ya shamba unayotaka kuwa nayo. Nina mzee wangu mmoja anataka kuuza mitiki kwa bei ya soko la Dunia wakati ana eka mbili kule Kilombero ndani, nani atanunua? Nilimshauri auze kibongo bongo.
Fuata maelezo ya Watalaam vizuri na usiwe mvivu wa kutembelea mashamba ya serikali au hata ya watu Binafsi kule Kilombero/Mtibwa/Longuza/Lindi. Mimi nilifika Kilombero Teak co, na nikafikia uamuzi sawa na nilivyoona. Ninayo mawasiliano ya wauza mbegu wa serikali.
Hakuna mavuno bora chini ya miaka 20, hata kama ni nguzo za umeme, ila unaweza kupata boriti kwa kazi za kawaida kabisa kwa muda wa chini ya miaka 15 hivi. Hapa tunazungumzia uhalisia sio nadharia, twendeni shambani tukapate taarifa sahihi.
Habari za Benki kukopesha wakulima wa Mitiki nazisikia sana, changamoto iko kwenye document na ukubwa wa shamba sio mitiki yenyewe.
Kisima
Unapatikana wapi naomba nitumie ktk pm namba yako tuwasiliane. Mm nipo dar es salaam
Nipo Moro mkuu na upandaji wa miti ni moja ya shughuri nifanyazo.
Nitakupa abc za namna gani hii miti inapandwa.
Nimekutumia mawasiliano yangu tayari.
Je miti ya MITIKI inaweza kulimwa Mwanza? Naombeeni msaada
Wadau habari zenu.
Nimenunua eneo lenye ukubwa wa ekari 10 huko Tanga, lengo ni kupanda michungwa. Lakini kuna wazo la kupanda miti aina ya Mitiki badala ya Michungwa.
Mwenye uzoefu wa miti hii tafadhari nipe ushauri, yaani tathmini kipi kinalipa kati ya michungwa na mitiki. Najua mitiki kuvuna hadi ipite zaidi ya miaka 15. Mwenye uzoefu anipe tathmini kati ya mazao haya mawili.