Kilimo cha Mihogo (Cassava): Mbinu, Ushauri, Changamoto na Masoko yake

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,021

Wakuu,

Kutokana na uhitaji wa kuwepo mjadala endelevu na wa tija kwa wajasiriamali, tumeona ni vema tukaweka hii thread kwa maslahi ya wengi.

Tunashauri Mjadala huu ujikitae kwenye maeneo yafuatayo:

1. Aina za mihogo na maeneo inakostawi vizuri
2. Misimu ambayo mihogo inapandwa ni miezi ipi? Inaweza kupandwa misimu yote ya mwaka?
3. Mihogo inashambuliwa na magonjwa yapi? Zipi mbinu za kukabiliana na maradhi hayo?
4. Mihogo inachukua muda gani tangu kupandwa hadi kuvunwa?
5. Hekari moja inaweza kutoa magunia mangapi ya mihogo?
6. Masoko ya mihogo na bidhaa zake ndani na nje ya nchi yapoje?
Asante


MICHANGO YA WADAU MBALIMBALI KUHUSU KILIMO CHA MIHOGO
 
Mzee umechungulia deal nasikia kilimo cha mihogo kinalipa vibaya mno na soko lake ni kubwa pia.

Mfano mzuri ulio hai nenda pale mbezi stendi mwisho utakuta wamama kibao wanapigania ikija fuso ya mihogo nusu saa nyingi inakua imekwisha,na unakuta wengine wanasubiria mpaka saa tano ya usiku.

Ngoja wataalamu wenye uzoefu nayo watupe data.
 
<br />
<br />
kweli mkuu nimeona hata naofisini wengi wanapiga mihogo badala ya chapat
 
Nadhani mtu yeyote aliye makini asingependa kuwekeza kwenye kilimo cha mhogo na kuuza bila kuongeza thamani, hasa kusindika. Ninajua very recently kuna watafiti wamegundua matumizi mengi zaidi ya unga wa mhongo mbali na chakula. Kama unaweza kutembelea ofisi za IITA unaweza kupata taarifa nzuri. Very recently pia kuna ka-mtandao ka mashirikia yanayopromote mhogo kameanzishwa nadhani naweza kukutautia details at some point
 
Mkuu nazisubiria hzo more details, ubarikiwe sana.
 
Wanajf naomba mwenye ujuz/utaalam wa kilimo cha mihogo, nampango wakulima huko kisarawe kama heka 5,
Soko lake likoje, na garama za kilimo zkoje?

Mkuu naanza ujenzi wa kiwanda cha kusindika Rufiji kuanzia Sept na by Jan 2012 nitaanza kununua tani 20 kila siku mihogo aina zote so kama utakuwa na uwezo wa kufikisha tutanunua yote. Michungu na mitamu yote tutachukua kutengezea starch tuna masoko ya nje makubwa na tutanunua bei nzuri tu mkuu.

Maelezo mengi zaidi yapo hapa mkuu

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources-10.html#post2118391
 
Wanajf naomba mwenye ujuz/utaalam wa kilimo cha mihogo, nampango wakulima huko kisarawe kama heka 5

Soko lake likoje, na garama za kilimo zkoje?
 
Nimekupata kiongozi tupo pamoja!
 
Wataalam pia tuombe mtusaidie kujua aina gan ya mbegu ni bomba!, tayar niko kazini. Kuna watalaam weng hapa lakn naona msimu unakaribia wako shamban, akina malila, ngoshwe n.k! Hawasikk
 
nami nimefaidika mkuu! Asante, hv maeneo ya huko mbegu zinauzwa bei gan kwa fungu? Maana nimeambia kule maeneo ya kisarawe, fungu la mashina 7 urefu wa mita moja ni buku6.
Mkuu check na magereza ndo walipewa jukumu la kuandaa mbegu bora zinazohimili ukame na magonjwa na zenye amount kubwa ya starch. Pia check pale Kibaha kuna shamba la mbegu ambalo hata sisi tumeshauriwa na wizara ya Kilimo kuna wataalamu pal wanafanya utafiti na kubreed mbegu bora na nimesikia zipo za kutosha.
 
Asante sana, wk hii nitafika kibaha, ni pale taasisi ya elimu? Au kwa afisa ugani wa wilaya? Nipe raman mkuu ili niende pale.
 
hivi mihogo inachukua muda gani tokea kulima hadi kuvuna,katika maeneo ya rufiji?

Inategemea aina ya mbegu. Kuna mbegu za muda mfupi (miezi 6) na za muda mrefu (mpaka mwaka mmoja). Halafu unataka mihogo kwa madhumuni gani - starch nyingi au chakula? Jaribu kuangalia aina ya mbegu ambayo itakufaa kwa aina ya matumizi yako.

Wengine huwa tunakula inapofika mwezi wa ramadhani.
 
Thanks much mkuu, nimekupata vema vp maeneo ya mlandizi kibaha yamafaa kwa kilimo?
 
Mkuu hii ni kibqha sehemu gani, ningependa kuwatembelea hawa na kuchukua mbegu.
 
<br />
<br />

Mkuu hii ni kibqha sehemu gani, ningependa kuwatembelea hawa na kuchukua mbegu.

Cassava research takes place in various research institutes that are based on the research zones. These include Agricultural Research Institute (ARI) Naliendele based in Mtwara (Southern zone), ARI Kibaha based in Kibaha (Eastern zone), ARI Ukiriguru based in Mwanza (Lake zone), ARI Maruku based in Kagera (Lake zone). Others are ARI Uyole based in Mbeya (Southern highlands zone), ARI Hombolo based in Dodoma (Central zone), ARI Tumbi based in Tabora (Western zone), ARI Tengeru based in Arusha (Northern zone) and ARI Kizimbani based in Unguja.

Sehemu zote hizi mkuu ndo nimeambiwa na wataalamu wa wizara mbegu zinapatikana na pia baada ya hawa jamaa kufanya utafiti wanatoa kwa Magereza kwa ajili ya kuzalisha ili wakulima wanunue kwa wingi sasa. So ukifika kwao japo sina address zao kamili utapata mbegu au maelekezo mazuri.

Mbegu ambazo zimethibitika kuwa na viwango kwa saa zinaitwa Kibaha, Mzungu na Kiroba ambazo ukilima kwa hali ya nchi yetu unweza kupata kati ya tani 10 hadi 20 kwa Hekta.

Nafikiri hii itatoa mwanga kidogo.
 
thanks much mkuu, nimekupata vema vp maeneo ya mlandizi kibaha yamafaa kwa kilimo??

Mkuu mikoa yote ya Pwani muhogo unakubali vizuri tu ila kama utapenda kuwa mdau kwa eneo letu au ungependa kuzalisha ili tununue ningeshauri ili kupunguza ghrama za usafirishaji ni nzuri kama utaelekea barabara ya Kilwa maeneo ya kuanzia Mkuranga kuelekea njia ya Mtwara hadi karibu na Mbuga ya Selous maeneo yapo wazi sana mkuu na yanakubali muhogo ile mbaya. Tutahitaji muhogo uingie kwenye mashine kabla ya kuzidi umri wa siku 3 tangu kuvunwa ambayo najua hiyo ni feasible kabisa kwa sehemu kubwa ya Tanzania kufikisha kiwandani.

So Mlandizi pia sio mbali nimeongelea kupanua profit margin kwa kupunguza transportation costs tu hapo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…