Mkuu Nina kitabu cha Kilimo cha matikiti maji PM me for details
Jamani habarini za wkend.., naomba kujua mche wa tikiti maji unaweza kuvunwa mara ngapi matunda yake?
Kwa mfano embe zinavunwa kila mwaka, ndizi unavuna mara moja tu na mche unakwisha kazi yake. Vipi kwa matikiti maji, unavunwa mara ngapi na kwa kipindi/interval gani?
Nataka kulima, yanalipa sana nisaidieni tafadhali.
natamani ningekua na mtaji maana gari likija kama kenta halikai siku nzima fasta tu kama ukitaka faida uza mwenyewe toa shamba leta sokoni bei ya jumla garini n elfu tatu mia5 had 2500 ukitaka haraka
watu wanapiga pesa kimya kimya ukitaka kujua utamu wa ngoma kunywa kiroba ingia ucheze
Mkuu wangu kilimo cha bustani ni changamoto! Faida ipo tena nzuri ya kuridhisha kabisa.
Binafsi nina uzoefu wa kutosha juu ya kilimo cha tikiti maji.
Mathalani unataka kulima ekari1 ya tikiti, huu ni mchanganuo mfupi kabisa;
kawaida ekari1=sqm4000
Kwa spacing ya 1m shimo hadi shimo na 2m mstari kwa mstari na kila shimo huwa naacha miche 2 na kuruhusu matunda3.
Na kama utapata mbegu ya hybrid itakuwa vizuri zaidi maana MATUNDA yake yanajiuza yenyewe, shambani ni sh1500.
So ukishusha hesabu hapo juu:
Jumla ya mashina ktk ekari1 ni
Sqm4000÷(1m×2m)×2=4000
Idadi ya MATUNDA =(4000×3)=12000
Mauzo shambani ni 12000×1500=Tshs18,000,000/=
Tatizo ni usimamizi, ila kilimo hiki kinalipa sana!
usome huu uzi toka mwanzo utaelewa nafikiri dawa zipo za majani ila tunda lenyewe halitaki ubichi hivyo ukiweza yawekee nyasi ili kuyazuia kukutana na ubichi na kupasuka sio ugonjwawakuu naomba mnisaidie dawa.nina tikiti zangu nimelima bagamoyo fukayosi zmestawi vema sema yanapasuka.nisaidieni wandugu yanazidi kupasuka.
Mkuu tikitiki hupasuka kutokana na maji kuzidi ama joto tizama kati ya hivyo viwili kimoja kitakuwa chanzo. Pole kwa hilo mkuu.
usome huu uzi toka mwanzo utaelewa nafikiri dawa zipo za majani ila tunda lenyewe halitaki ubichi hivyo ukiweza yawekee nyasi ili kuyazuia kukutana na ubichi na kupasuka sio ugonjwa
Hello wana JF
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliokuwa wanawapa watu moyo wa kufanya kilimo kwani hatimaye nami nimelima Tikiti na sasa nimevuna. Ingawa mavuno hayakwenda vizuri kutokana na mvua.
Sasa natafuta soko la matikiti yapatayo 900 yenye uzito wa kuanzia kilo 3 mpaka 7. Tafadhali naomba msaada wa kujua wapi naweza kupata soko kabla hayajaniharibika.
UKo mkoa gani mkuu?