Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Vipi mbuzi ulishapata mkuu?
Tuje kwenye nanasi, kama uko serious, nenda regional block Kibaha idara ya kilimo,pale watakupa kila kitu sawa na eneo ulilopata shamba kwa ukanda huu wa Dsm/Pwani. Kama hutajali nenda Kiwangwa bagamoyo ukajifunze kwa vitendo kwa wakulima, watakwambia faida ya mbegu za kisasa na faida ya mbegu za kienyeji kwa vitendo,naamu pia wakati na udongo gani unafaa.
Mbegu za nanasi ziko barabarani nyingi tu zinauzwa, ila kabla hujanunua fika Kibaha kwanza. Ukame unapunguza mavuno na kama unaweza nenda pale Mwenge njia ya Coca cola, kuna kituo cha serikali kwa ajili ya miche ya minazi/embe uliza kituo cha minazi. Pale kuna watalaamu kibao.
Mkuu kazi njema.
Wakuu naomba kujua wapi ninaweza kupata mbegu ya minanasi, nina kajieneo mahali sina plan nako kwa mwaka huu hadi mwishoni mwa mwaka kesho. sasa sitaki kukaacha kakae bure ni wapi ninaweza kupata kama miche 40,000 au zaidi na kwa bei nafuu?
Jone Mwalwisi
Mpigie huyu 0714-298116 mche mmoja ni kati ya shs25 na 30
Unapatikana sehemu gani ?.
Mkuu Mwalwisi.
Uko maeneo gani ?.Pwani,Dar na Tanga ni maeneo yanayostawi mananasi,yapo mananasi yanayostawi kanda ya ziwa Geita na eneo kubwa la kanda hiyo.
Kama unaishi maeneo ya mkoa wa Pwani,Tanga na Dar nakushauri tembelea Kiwangwa ni eneo mashuhuri kwa kilimo cha nanasi na upatikanaji wa miche ya nanasi ni rahisi sana mche mmoja unauzwa kati ya tsh 30 - 50.Eka moja ya nanasi inaingia miche 10,000 - 12,000.Ni vyema ukaandaa eneo lako mapema kwasababu minanasi inaweza kupandwa hata kipindi cha kiangazi.
Nimeku PM mkuuKama upo maeneo ya Mkuranga ni PM. Zipo nyingi hapa Dundani na Mwanambaya
Mpigie huyu 0714-298116 mche mmoja ni kati ya shs25 na 30
Mpigie huyu 0714-298116 mche mmoja ni kati ya shs25 na 30
Hivi nanasi tangu lipandwe hadi lizae linachukua muda gani?
Mkuu ebu check vizuri hizo number za simu uenda kuna number umekosea watu tuko kikazi zaidi.
Labda kama alitumia ya mtu. Mimi aliniuzia miche 280,000
mkuu unaweza kutupa dondoo kidogo ktk hiyo miche ulifanikiwa kuvuna mananasi mangapi na kwa kiwango kipi (ubora)? if you dont na mapato kwa kukadiria
Nimeipanda hii Januari. Ekari moja inatafuna miche 14,000 nami nimepanda ekari 20. Kuna suala la mbolea na upaliliaji pamoja na kushed jua wakati wa kiangazi. Hopefully ntavuna around July 2013. Nanasi moja kwa sasa ni TZS 300 likiwa shambani au unaweza kuuza eka moja 3,000,000