Ntemi Kazwile
JF-Expert Member
- May 14, 2010
- 2,182
- 307
Vipi mbuzi ulishapata mkuu?
Tuje kwenye nanasi, kama uko serious, nenda regional block Kibaha idara ya kilimo,pale watakupa kila kitu sawa na eneo ulilopata shamba kwa ukanda huu wa Dsm/Pwani. Kama hutajali nenda Kiwangwa bagamoyo ukajifunze kwa vitendo kwa wakulima, watakwambia faida ya mbegu za kisasa na faida ya mbegu za kienyeji kwa vitendo,naamu pia wakati na udongo gani unafaa.
Mbegu za nanasi ziko barabarani nyingi tu zinauzwa, ila kabla hujanunua fika Kibaha kwanza. Ukame unapunguza mavuno na kama unaweza nenda pale Mwenge njia ya Coca cola, kuna kituo cha serikali kwa ajili ya miche ya minazi/embe uliza kituo cha minazi. Pale kuna watalaamu kibao.
Mkuu kazi njema.
Nashukuru sana mkuu