Kilimanjaro marathon 2017, naomba updates

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,760
48,407
Mbio za mwaka huu za masafa marefu maarufu kama marathon zinafanyika Tanzania leo, nimetafuta updates na mapicha kote hamna ila blackout. Kuna Wakenya baadhi yao jamaa zangu wamesafiri kwenda kushiriki, nategemea ushindi wa kufunika...te te te

Haya mwenye mapicha aachie humu.
 
Watu bado wana 'hangover' ya Simba na Yanga.

Hehehe!! Lakini hao Simba uchawi ndio zao, wanapakatwa tu hamna kitu hapo. Halafu kumbuka Yanga bado wana mechi hivyo points wataongeza. Anyway hapa sio mahali pake, leta picha za hizo mbio za Kili, mlima tunaurudisha wamiliki stahiki leo....hehehehe
 
ot%2Bpic-7833.jpg


Mbio za Kili marathon zimefanyika leo manispaa ya Moshi mjini mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya chuo cha ushirika ambapo wakimbiaji zaidi ya 8000 wameshiriki mbio hizo.

Mbio hizo zimefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel majira ya saa kumi na mbili nusu asubuhi ambapo mbio za kilometa 42 zilianza, huku wale kilometa 21 wakianza mbio hizo majira ya saa moja kamili asubuh.

Mbio hizo ziligawanyika katika makundi tofauti totauti kuanzia wale waliokimbia umbali wa kilometa 42, umbali wa km 21 huku kwa upande wa walemavu wao walishindana katika mbio za umbali wa km 10 pamoja na zile za kilometa 5 ambazo hazina ushindani. kila kundi walipatikana washindi wa mbio hizo.

ot%2Bpic-7906.jpg


ot%2Bpic-8030.jpg


ot%2Bpic-8071.jpg


ot%2Bpic-8167.jpg

Washiriki wa mbio za kilometa 10 kwa upande walemavu wakichuana vikali

ot%2Bpic-8604.jpg

Mshindi wa kwanza km 42 wanaume, Moses Mongiki (Kenya)

ot%2Bpic-8759.jpg

Mshindi wa kwanza km 42 wanawake, Shelmith Nyawira Muriuki (Kenya)

ot%2Bpic-8274-2.jpg

Mshindi wa kwanza km 21 wanaume, Emmanuel Giniki (Tanzania)

ot%2Bpic-8387.jpg

Mshindi wa kwanza km 21 wanawake, Grace Kimanzi (Kenya)
 
Asante kilam kama kawaida Wakenya walichukua chao, halafu hawakuja wababe wa hayo mambo, wapo kule Tokyo na kwengineko.
 
Moshi ni mji mzuri

Moshi pasafi sana, halafu wana sheria za Kinairobi Nairobi, kwamba ukipatikana unatupa taka ovyo unakamatwa, halafu askari huwa wameahidiwa kulipwa kwa kila wanayemkamata akichafua mji.
Halafu kijijini wana nyumba nzuri nzuri sana, tatizo wengi hawaishi huko. Na ndio hawa Wachagga unaowaona Nairobi, na kwengineko, wanajenga nyumba nzuri vijijini kwao lakini wanaenda msimu wa Krisimasi tu basi. Kuna wale hulipa jamaa zao kuishi kwenye hizo nyumba.
 
Moshi pasafi sana, halafu wana sheria za Kinairobi Nairobi, kwamba ukipatikana unatupa taka ovyo unakamatwa, halafu askari huwa wameahidiwa kulipwa kwa kila wanayemkamata akichafua mji.
Halafu kijijini wana nyumba nzuri nzuri sana, tatizo wengi hawaishi huko. Na ndio hawa Wachagga unaowaona Nairobi, na kwengineko, wanajenga nyumba nzuri vijijini kwao lakini wanaenda msimu wa Krisimasi tu basi. Kuna wale hulipa jamaa zao kuishi kwenye hizo nyumba.

Sasa mbona Nairobi pachafu?
 
Sasa mbona Nairobi pachafu?

Ulikua Nairobi mwisho lini, hebu njoo mjini halafu ujisahau ufanye yale mazoea yenu ya Dar kutema mate ovyo, kuvuka barabara ukiongea kwa simu, kutupa taka kila mahali... Yaani Dar mjini pachafu sana mvua ikinyesha unaona kinyesi kinaelea kwenye mafuriko, mji unanuka balaa halafu ukiongeza na joto kali hadi unahisi kichefu chefu, omba yasikukute haya kama upo kwenye foleni.

Kuna hata Watanzania wanaofanya kazi mikoani kila wakitumwa Dar kwa shughuli ya siku chache huwa wanaona kama wanaadhibiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom