Baraza la vijana wa CHADEMA mkoani Arusha wamedhamiria kupandisha bendera ya CHADEMA na M4C kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro kwenye safari itakayoanza siku ya jumamosi, tarehe 25/11/2012 mkoani Arusha. Lengo la shughuli hiyo ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba vijana wapo tayari kwa mabadiliko. Kutakuwa na viongozi wa dini mbalimbali watakaofanya swala baada ya bendera hizo kusimikwa rasmi kileleni humo. Safari itaanzia Arusha na inaratibiwa na Bavicha Arusha kwa gharama ya 50,000 ambayo ni gharama za chakula na viingilio. Shughuli hiyo ipo wazi kwa yeyote anayetaka kwenda na wanaotaka kuwagharamia wale walioshindwa kulipia gharama ila wangependa kwenda. Kwa yeyote anayetaka kwenda au kutoa sapoti au ushauri awasiliane na m/kiti wa Bavicha Arusha, mh. Nanyaro Ephata.
Nawasilisha.
Inapendeza sana,mwanga wa matumaini upo jirani kwa watanzania wote.ukombozi wa nchi hii upo karibu sana tusikate tamaa,tuwe pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kuondoa utawala dharimu madarakani.
Suala la msingi ni hili, hao watu wanaotaka kupandisha hiyo bendera ya M4C wanauzoefu wa kupanda mlima???? Wasije wakaishia njiani halafu ikawa aibu. Hilo ndilo angalizo kuu.
Suala la msingi ni hili, hao watu wanaotaka kupandisha hiyo bendera ya M4C wanauzoefu wa kupanda mlima???? Wasije wakaishia njiani halafu ikawa aibu. Hilo ndilo angalizo kuu.