Kilimanjaro: CHADEMA Arusha kupandisha bendera ya CHADEMA na M4C.

Filipo

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
9,343
5,536
Baraza la vijana wa CHADEMA mkoani Arusha wamedhamiria kupandisha bendera ya CHADEMA na M4C kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro kwenye safari itakayoanza siku ya jumamosi, tarehe 25/11/2012 mkoani Arusha. Lengo la shughuli hiyo ni kuudhihirishia ulimwengu kwamba vijana wapo tayari kwa mabadiliko. Kutakuwa na viongozi wa dini mbalimbali watakaofanya swala baada ya bendera hizo kusimikwa rasmi kileleni humo. Safari itaanzia Arusha na inaratibiwa na Bavicha Arusha kwa gharama ya 50,000 ambayo ni gharama za chakula na viingilio. Shughuli hiyo ipo wazi kwa yeyote anayetaka kwenda na wanaotaka kuwagharamia wale walioshindwa kulipia gharama ila wangependa kwenda. Kwa yeyote anayetaka kwenda au kutoa sapoti au ushauri awasiliane na m/kiti wa Bavicha Arusha, mh. Nanyaro Ephata.
Nawasilisha.
 
Ahsante sana Bavicha Arusha, Lazima bendera ya chama ipandishwe katika kilele cha mlima Mrefu Barani Africa...

Mkuu hizi ni habari nje sana! Najua sintaweza kwenda ila nimelipa gharama za kufaninisha kamanda mmoja kwenda.
 

Mimi nitabeba rocket nikifika juu nyie mlioko chini nitafutieni target ya
jangili la pembe za ndovu wetu!!
 
Safi sana ni mpango mzuri sana!naona mambo ya ubunifu wa hari ya juu!
 
Kiukweli CDM Arusha ni wabunifu na hivi ndivyo inatakiwa kuwa, hongereni sana, wengine tutawasupport kwa maombi ili mpande na mrudi salama.
 
Inapendeza sana,mwanga wa matumaini upo jirani kwa watanzania wote.ukombozi wa nchi hii upo karibu sana tusikate tamaa,tuwe pamoja katika kipindi hiki kigumu cha kuondoa utawala dharimu madarakani.
 
filip suala lako nimelinote.

Suala la msingi ni hili, hao watu wanaotaka kupandisha hiyo bendera ya M4C wanauzoefu wa kupanda mlima???? Wasije wakaishia njiani halafu ikawa aibu. Hilo ndilo angalizo kuu.

Mengine itifaki itazingatiwa.
 
Last edited by a moderator:
Filipo

Tunashukuru sana kwa hili!
Na bila shaka ni wakati wa mabadiliko!

Viva CDM!
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jambo jema sana!!
Mimi ntamchangia kamanda mmoja ili aweze kutekeleza yaliyokusudiwa na Vijana!
Filipo ntakupatia mchango wangu Jumanne!!
 
Last edited by a moderator:
Hili ni jambo jema sana!!
Mimi ntamchangia kamanda mmoja ili aweze kutekeleza yaliyokusudiwa na Vijana!
Filipo ntakupatia mchango wangu Jumanne!!

nimekupata my dia. J4 nitafuatilia na nitawakilisha!
 
Last edited by a moderator:
filip suala lako nimelinote.

Suala la msingi ni hili, hao watu wanaotaka kupandisha hiyo bendera ya M4C wanauzoefu wa kupanda mlima???? Wasije wakaishia njiani halafu ikawa aibu. Hilo ndilo angalizo kuu.

Mengine itifaki itazingatiwa.

usihofu Mkuu! Vigezo na masharti kuzingatiwa!
 
Last edited by a moderator:
all the best makamanda chini ya Nanyaro,tunataka dunia ijue na mafisadi wote wajisalimishe kabla ya 2014
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom