Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,749
Kwa hali yeyote ni lazima utawala wa Sheni uondoke madarakani,kilichotokea Zanzibar ni Mapinduzi,kwa lugha nyepesi upinduaji umechelewa kiasi ya kutumia watu waliovalia UNIFORM za JWTZ na kumteka makamo mwenyekiti wa Tume alipokuwa anaendelea kutangaza baada ya Mwenyekiti kutoonekana.
ushindi wa Magufuli umewahi na hakuna data zinazothibitisha kuwa alishindwa kama ilivyo Zanzibar ambako data za uchaguzi zilibandikwa ukutani kama haitoshi hata washindi wa Uwakilishi walikabidhiwa hati za ushindi pia kuhalalishwa kwa wabunge ambao nao walishinda kupitia uchaguzi huohuo alieufuta mtu mmoja tu na wao kuhalalishwa na wasimamizi walewale kuwa wameshinda uchaguzi na kukabidhiwa hati za ushindi.
Kama watu watanyamaza iwe kutoka chama chochote kile cha siasa ,kilichotokea na kufanywa Zanzibar kinaweza kuwakuta na kwa kutumia hila na njia zilizofanywa na akina Sheni na kundi au tuseme genge lake.
Kuendelea kuwachwa kwa genge hilo kuiminya demokrasia ni kuiweka matatani serikali ya Muungano ,hilo halina mjadala ni suala la muda tu ,na athari zake ni kubwa kuliko wanavyofikiria kuwa kodi inayokusanywa itamaliza kero na kuiweka sawa nchi ,huko ni kujidanganya ni lazima uchaguzi wa Zanzibar uendelee kutangazwa na mshindi ambao ni CUF wapewe ushindi wao kwani ikisemwa kuna maisha baada ya uchaguzi genge la Sheni ni lazima wayakubali hayo.