Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Kilichomponza Tido Mhando ni uzalendo wake

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,149
Reaction score
56,431
Akiwa BBC Nairobi miaka hiyo aliingia matatizoni na serikali ya Rais Moi kwa kufichua mauaji ya Robarth Auko. Wakenya wengi na serikali walikuwa wakidhani Tido ni Mkenya lkn kumbe alikuwa ni Mtanzania.

Alikuwa akiwindwa sana na kwa sababu hizo BBC ikamuondoa Kenya na kumpeleka London. Akiwa London alifanya kazi ya utangazaji kwa mafanikio makubwa sana na inaelezwa historia yake haijavunjwa na mtangazaji yeyote kwa kuwahoji viongozi wengi hususan marais tena kwa ujasiri mkubwa. Ikumbukwe aliwahi kumhoji Marehemu Laurent Kabila juu ya uongozi wake usalama wake na usalama wa nchi kwa ujumla na baada ya mahojiano yale haikupita wiki kabila akauwawa.

Kwa wakati huo miaka takriban 50 ya BBC haijawahi kuongozwa na mtu mweusi katika nafasi ya ukurugenzi.

Lkn Tido mhando alifanikiwa kuwa mkurugenzi wa BBC wa kwanza mweusi tena tena mtanzania baada ya yule mama wa kizungu aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kuhamishwa kwenda kuwa mkurugenzi wa BBC katika bara Asia.

Nikutokana na uchapakazi wake uliomletea sifa na heshima dunia nzima katika fani ya utangazaji ndipo Rais kikwete alipomuomba arudi Tanzania kuja kuboresha kama siyo kukifufua chombo cha habari cha Taifa.

Wakati huo kulikuwa na Radio Tanzania na television ya Taifa TVT zilizounda kitu kilichoitwa taasisi ya utangazaji Tanzania TUT. Ilikuwa ni vigumu sana kumshawishi Tido akubali kazi yake aliyokuwa akilipwa ma pound ya Uingereza lkn hatimae kwa uzalendo wake alikubali kuacha kazi yake na kuja Tanzania.

Alipofika kitu cha kwanza aliomba apewe mamlaka kamili ya kukisuka upya chombo cha Taifa huku akifafanua kwamba ni aibu kwa nchi kama Tanzania kutokuwa na shirika la utangazaji akitolea mfano kama BBC, KBC, UBC, CNN nk.

Ndipo alipopewa mamlaka ya kuisuka na ndio akaanzisha shirika la utangazaji la Taifa TBC. Akafanikiwa kulifanya kuwa shirika pendwa na lenye wapenzi wengi kuliko chombo chochote Tanzania.

Kilichokuja kumponza ni kipindi cha uchaguzi kilipofika alipoanzisha kipindi cha mchakato majimboni.

Kipindi kilikuwa kikiongozwa na yeye mwenyewe na alikuwa akikutanisha wagombea wa CCM na wa upinzani kujinadi pamoja na kuelezea sera zao. Na kisha kuruhusu maswali kwa watazamaji.

Ngoma ilielekea kuwa ngumu sana kwa CCM kutokana na kushambuliwa kila kona na wananchi kwenye maswali ndipo CCM walipogoma kuendelea na kipindi cha mchakato majimboni na wakamwambia Tido akiondoe kipindi kisiendelee.

Tido alikataa akasema ameshasaini mkataba na hakielimu kama wadhamini wakuu wa kipindi hivyo kuuvunja mkataba ni gharama akashauri kama CCM wameamua kujitoa basi yeye ataendelea na ambao wako tayari

Kweli kipindi kiliendelea na kilisaidia wapinzani kupata wabunge wengi na kushuhudia anguko la wabunge wengi maarufu wa CCM kwenye uchaguzi ule. Hivyo kitendo kile hakikuwafurahisha mabwana wakubwa wakamuondoa Tido TBC

Walipomuondoa alichukuliwa na Mwananchi Comunication kama mkurugenzi mkuu ambapo pia alifanya kwa mafanikio makubwa kabla ya kumaliza mkataba wake na kuchukuliwa na Azam Tv. Ambapo kama kawaida yake amefanikiwa kukufanya king'amuzi cha Azam kuwa kinga'amuzi kinachoongoza kwa mauzo mengi kuliko king'amuzi chochote Tanzania.

Sasa pichani hapo chini ni Tido Mhando akiwa amefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya ofisi akiwa TBC. Binafsi nimeumia roho sana maana nimjuavyo Tido ni jembe na CV zake zinamruhusu Kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari duniani kwa nafasi ya ukurugenzi.

Ila kwakuwa mahakama ni chombo cha haki ngoja tuiachie itende haki ila kwakweli inasikitisha sana. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

FB_IMG_1516978060258.jpg
 
Namkumbuka tido,ndio aliyekuja kulifanya gazeti la mwananchi liwe bora kuliko magaxeti yote,kwa sababu ya misingi aliyoiweka kwenye gazeti la mwananch,mwanaspot na the citizen, mpaka Leo ni magazeti bora.amefanya mageuz makubwa sana kwenye tasnia ya habari Tanzania.
 
Huo ufusadi ndo wanauona Leo auditors walikua likizo? Ukurupukaji. com. Watashindwa except Kama no maagizo kutoka juu.
 
Back
Top Bottom