Kilichomponza John Mnyika akafukuzwa bungeni ni kushindwa kujitetea kama Kafulila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kilichomponza John Mnyika akafukuzwa bungeni ni kushindwa kujitetea kama Kafulila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jun 22, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tumeshajadili na sitaki kurudia kauli ya John Mnyika kutolewa nje bungeni aliposema kuwa Rais Kikwete ni kiongozi dhaifu.

  Mwaka jana David Kafulila ilikuwa hivihivi alitakiwa kufuta kauli yake aliposema serikali ya legelege haikusanyi kodi. Kafulila kama Mnyika alikataa katakata kufuta kauli yake. Lakini Kafulila alienda mbali kwa kusema kuwa hafuti kauli kwa sababu ame-quote hotuba ya Julius Nyerere iliyosema:...Serikali Corrupt haikusanyi kodi...Kesi ikaisha maana ni kweli wengi tunaijua hii kauli.

  John Mnyika naye angeweza kusema kuwa kusema Rais wa nchi ni kiongozi dhaifu si kumdhalilisha kwani yeyote angeweza kum-quote Julius Nyerere pia.

  Je, Mnyika angemnukuu Julius Nyerere wapi? Soma kitabu cha Nyerere kiitwacho UONGOZI WAKE NA HATIMA YA TANZANIA. Sentensi ya mwisho kwenye ukurasa wa 50 inasema hivi:

  {..Rais Mwinyi ni mtu mwema na mpole, lakini ni kiongozi dhaifu; au upole wake na udhaifu wake unatumiwa na watu ambao wala si wema wala wapole kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu..}.

  Hapa Mnyika angekuwa amemaliza kesi kama mwenzake Kafulila kirahisi kabisa.

  Na wala tusingefikia hatua ya kulifanya neno DHAIFU kupata umaarufu ulioanza masaaa kadhaa baada ya kutimuliwa Mnyika hadi kufanya T-SHIRT zenye neno hilo (DHAIFU) kupanda gharama kama kiatu kilichomponda George Bush kilivyopanda bei baada ya yule mwandishi Muntadhar al-Zaidi kumtupia hicho kiatu.
   
 2. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  t shirt hizi kwani zipo tayari? zinapatikana wapi?
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  there is no need to neither justify nor qualify any statement ya mnyika, the statement was 100% sufficient na kumtoa nje imeboresha tu uzito wa kauli, wanngei-ignore ingepita kama upepoz tu
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Haikuwa na haja ya kujitetea kwani Mnyika ametoa neno hilo ndani ya nafsi yake.

  Na kama hilo limewauma sana mafisadi na watoe kauli yao na tuwasikie maana Mi mpaka sasa nasema jk & wabunge wake wote ni WADHAIFU kupindukia!

  Ila kweli Baba wa Taifa alikuwa anaona mbali,alijua tu ya kwmb watu anaowaachia madaraka ni Wadhaifu.

  MUNGU AILAZE ROHO YA J K NYERERE MAHALA PEMA PEPONI.
   
 6. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
Loading...