Kilichomkuta mchungaji huyu kiwe funzo

tatizo ni kuwa wachungaji wengi wanaamini dini ya kweli ni miujiza pekee

Pili wana ni Mungufy kiasi cha kuhisi wao ndiyo wenye mamlaka na kusahau kuwa wao ni daraja tuu
Hili ndio tatizo kubwa sana.

Umesema kweli mzee.
 
Wa kulaumiwa ni hao wanaoamini kwamba kuna mtu anaweza kumrejeshea maiti uhai wake na wala siyo huyo mchungaji kwa sababu yeye anatafuta riziki yake kupitia wasiotumia vizuri akili zao.
 
Wa kulaumiwa ni hao wanaoamini kwamba kuna mtu anaweza kumrejeshea maiti uhai wake na wala siyo huyo mchungaji kwa sababu yeye anatafuta riziki yake kupitia wasiotumia vizuri akili zao.
sasa kwanini walaumiwe ilhali AKILI hawana
 
Nakumbuka kisa cha Mwinjilisti Enoch Mwanyonga, dah.... Akaenda msibani, akawaambia wafiwa, acheni kulia, marehemu hajafa, amelala tuuu.... Hebu fukieni kaburi, jamaaa wakamwambia usitutanie, mfufue Kwanza ndipo tufukie kaburi.
Jamaa akapiga dua za kufa mtu, aliyelala hakuamka. Kidogo achezee mikwaju
Hahahaha hatari sana
 
hawa wachungaji kdg wamponze jamaa yangu, alitokea mgonjwa mtaani kwake kuwa ilikuwa alfajiri akaitwa amcheki mgonjwa. baada ya kumcheki akaiambia familia amekwisha fariki familia ikawasiliana na mchungaji kwa ajili ya mazishi.

wacha mchungaji aseme mtoto ajafa,niko na jamaa chimbo akapokea simu toka kwa mkewe kuwa katangaza dogo kafa kumbe mzima.

jamaa kijasho kikamtoka ila ananiambia yule dogo alihakikisha kafariki sasa inakuwaje,huku nyumba mchungaji piga maombi kumfufua wapiiiii ilikaa siku nzima wakazika.

hadi leo jamaa yuko moto sana na yule mchungaji
 
Haya mambo haya....

Kule Uganda kuna waliochomwa moto kanisa zima na mtume na nabii Kibwetere kwa kuwaambia waumini wake ni mwisho wa dunia halafu yeye akachomokea kwenye tundu jembamba (narrow escape) aka escape na fedha dhahabu na silva alizowavua waumini

Naskia alikimbilia marekani anakula bata hadi kesho, huku mamia ya waumini wake wakiwa tayari wameshauona mwisho wa dunia
 
duh! Ahsante bwana nilikua sijawahi kusikia hii inshu
 
hawa wachungaji kdg wamponze jamaa yangu, alitokea mgonjwa mtaani kwake kuwa ilikuwa alfajiri akaitwa amcheki mgonjwa. baada ya kumcheki akaiambia familia amekwisha fariki familia ikawasiliana na mchungaji kwa ajili ya mazishi.

wacha mchungaji aseme mtoto ajafa,niko na jamaa chimbo akapokea simu toka kwa mkewe kuwa katangaza dogo kafa kumbe mzima.

jamaa kijasho kikamtoka ila ananiambia yule dogo alihakikisha kafariki sasa inakuwaje,huku nyumba mchungaji piga maombi kumfufua wapiiiii ilikaa siku nzima wakazika.

hadi leo jamaa yuko moto sana na yule mchungaji
ahaha mchungaji alijivika Umussa alafu fimbo haikugeuka nyoka
 
Nimekaa jirani na kanisa fulani wale wagonjwa na walemavu waliokuwa wanapita njia hapo kwangu miaka Saba yote niliwaona vile vile hakuna aliyebadilika na wengine walifariki bila kupona RIP Bupe
 
Nimekaa jirani na kanisa fulani wale wagonjwa na walemavu waliokuwa wanapita njia hapo kwangu miaka Saba yote niliwaona vile vile hakuna aliyebadilika na wengine walifariki bila kupona RIP Bupe
ahaha haya mambo NI kukubaliana tu na hali halisi
 
Kama ilivyo hulka ya binadamu wengi wa kileo kuendeshwa na mihemko inayo wafanya kuwa wepesi kuamini na kusadiki pia na kupelekea kupoteza muda kufanya mambo yaliyo na umuhimu kwa wakati. Imekuwa kasumba siku hizi kila bango lihusulo mikutano ya injili linaambatana na maneno yenye ushawishi ambayo kwa lugha nyingine naweza Sema ni maneno ya kitapeli.

Unakuta tangazo limeandikwa /kutangazwa kuwa:

VIPOFU WATAONA
VIZIWI WATASIKIA
VIWETE WATATEMBEA
UTAOMBEWA KUWA TAJIRI

Na kuna mtumishi mwaka jana hapa Mbeya alitangaza kuwa maiti zitafufuliwa. Basi, kama Waswahili walivyowahi kusema kuwa Mungu hadhihakiwi.

Wakati mchungaji yule yupo akiendelea na mkutano, nyumba kama ya tano toka pale yalipo makutano kuna mgonjwa akafariki, basi wale wanafamilia wakakimbia kumueleza mchungaji kilicho tokea na kwa kuwa katika matangazo waliona habari za KUFUFUA WAFU.

Basi mchungaji akautangazia mkutano kuwa kuna dharura nyumba ya jirani hivyo wakaungane kufanya maombi Mungu akadhihirike. Basi Wabongo zilipigwa simu kila kona kupena habari kuwa leo kuna mtu atafufuliwa doh!

Watu walikodi bajaji na bodaboda wakafika eneo la tukio, maiti ikatolewa na mchungaji akawasihi watu waimbe tenzi ili kukaribisha Roho Mtakatifu. Watu wakaimba si mchezo, watu wakabubujikwa kweli kweli, basi maombi yakaanza, ilikuwa SAA 9 alasiri, maombi yakapigwa mpaka kufika saa 2 kasoro usiku marehemu katulia tulii.

Watu wakaanza minong'ono kwamba mbona mmchungaji anachelewesha au mambo yamebuma. Baridi iliingia kusema ukweli kila mtu alijikunyata lakini wakati huo mchungaji jasho linamtiririka huku akionekana dhahiri kuwa amepaniki.

basi wazee watu wazima wakaona wajiongeze wamsitiri mtu mzima mwenzao na aibu ile, ndipo wakamtuma mtoto wa miaka kama 12 hivi ajifanye amepandisha mapepo na kuzua tafrani mahala pale na kisha kubebwa kuingizwa ndani kisha ikatangazwa kuwa mtoto alikuwa na hali mbaya, hivyo wanaomba mchungaji akaongeze nguvu kwa yule aliye hai , kisha warejee kwa marehemu.

Baada ya kutoka hapo. Wazungu wanasema, ''the rest is history''

Sijui ni watu wasio julikana
Ongeza bidii mkuu unaweza kuwa mtunzi mzuri wa riwaya
 
Kuna wahubiri wakubwa dsm walikuwa wakidanganya wanaponya kumbe wanaleta watu kutoka kimanzichana wakijifanya viwete kisha wanafanya usanii wanapona wanapewa elfu 30,000/= wanarudi zao kimanzichana!
Wote walikuwa matapeli watupu, mara misukele imeanguka ubungo kanisani! utapeli mtupu!
 
Back
Top Bottom