Kilichomkuta mchungaji huyu kiwe funzo

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Kama ilivyo hulka ya binadamu wengi wa kileo kuendeshwa na mihemko inayo wafanya kuwa wepesi kuamini na kusadiki pia na kupelekea kupoteza muda kufanya mambo yaliyo na umuhimu kwa wakati. Imekuwa kasumba siku hizi kila bango lihusulo mikutano ya injili linaambatana na maneno yenye ushawishi ambayo kwa lugha nyingine naweza Sema ni maneno ya kitapeli.

Unakuta tangazo limeandikwa /kutangazwa kuwa:

➡ VIPOFU WATAONA
➡VIZIWI WATASIKIA
➡VIWETE WATATEMBEA
➡UTAOMBEWA KUWA TAJIRI

Na kuna mtumishi mwaka jana hapa Mbeya alitangaza kuwa maiti zitafufuliwa. Basi, kama Waswahili walivyowahi kusema kuwa Mungu hadhihakiwi.

Wakati mchungaji yule yupo akiendelea na mkutano, nyumba kama ya tano toka pale yalipo makutano kuna mgonjwa akafariki, basi wale wanafamilia wakakimbia kumueleza mchungaji kilicho tokea na kwa kuwa katika matangazo waliona habari za KUFUFUA WAFU.

Basi mchungaji akautangazia mkutano kuwa kuna dharura nyumba ya jirani hivyo wakaungane kufanya maombi Mungu akadhihirike. Basi Wabongo zilipigwa simu kila kona kupena habari kuwa leo kuna mtu atafufuliwa doh!

Watu walikodi bajaji na bodaboda wakafika eneo la tukio, maiti ikatolewa na mchungaji akawasihi watu waimbe tenzi ili kukaribisha Roho Mtakatifu. Watu wakaimba si mchezo, watu wakabubujikwa kweli kweli, basi maombi yakaanza, ilikuwa SAA 9 alasiri, maombi yakapigwa mpaka kufika saa 2 kasoro usiku marehemu katulia tulii.

Watu wakaanza minong'ono kwamba mbona mmchungaji anachelewesha au mambo yamebuma. Baridi iliingia kusema ukweli kila mtu alijikunyata lakini wakati huo mchungaji jasho linamtiririka huku akionekana dhahiri kuwa amepaniki.

basi wazee watu wazima wakaona wajiongeze wamsitiri mtu mzima mwenzao na aibu ile, ndipo wakamtuma mtoto wa miaka kama 12 hivi ajifanye amepandisha mapepo na kuzua tafrani mahala pale na kisha kubebwa kuingizwa ndani kisha ikatangazwa kuwa mtoto alikuwa na hali mbaya, hivyo wanaomba mchungaji akaongeze nguvu kwa yule aliye hai , kisha warejee kwa marehemu.

Baada ya kutoka hapo. Wazungu wanasema, ''the rest is history''

Sijui ni watu wasio julikana
 
Baathi ya wachungaji wa siku hizi wengi wao sio wakweli wanatumia njia mbalimbali il wawe na waumini wengi
 
Nakumbuka kisa cha Mwinjilisti Enoch Mwanyonga, dah.... Akaenda msibani, akawaambia wafiwa, acheni kulia, marehemu hajafa, amelala tuuu.... Hebu fukieni kaburi, jamaaa wakamwambia usitutanie, mfufue Kwanza ndipo tufukie kaburi.
Jamaa akapiga dua za kufa mtu, aliyelala hakuamka. Kidogo achezee mikwaju
 
Ha ha ha
 
Shida ni kwamba watu hawasomi biblia, sio kila maiti inafufuliwa ila mpaka upate kibali cha roho mtakatifu, na ukipewa kibali kutoka juu jua wazi kuwa kuna watu Mungu anawatafuta watubu dhambi zao na kumkiri kuwa Yesu ni Bwana zaidi ya mabwana
 
Nakumbuka kisa cha Mwinjilisti Enoch Mwanyonga, dah.... Akaenda msibani, akawaambia wafiwa, acheni kulia, marehemu hajafa, amelala tuuu.... Hebu fukieni kaburi, jamaaa wakamwambia usitutanie, mfufue Kwanza ndipo tufukie kaburi.
Jamaa akapiga dua za kufa mtu, aliyelala hakuamka. Kidogo achezee mikwaju
Watu wanaumia wameondokewa na ndugu wao wanaleta usanii? Watakuchoma moto walai.
 
Back
Top Bottom