Kilichoiponza Simba mechi dhidi ya Yanga kuwania Ngao ya Hisani

MANJANGO

Member
Jun 16, 2022
54
156
Mechi imekwisha, Simba imekufa 1-2 dhidi ya Yanga,

Kiukweli inàuma mechi tano mfululizo za derby Simba hajashinda hata moja, huku akipokea vipigo vitatu na droo mbili(tena zilizokua na faida kwa Yanga)

Turudi kwenye mada.
Simba ilikosa Wachezaji wa kuamua mechi. Kiukweli mechi ya jana ndio mechi ambayo Simba alitengeneza nafasi nyingi hasa kipindi cha pili., Tatizo lilikuwa nani afanye nini wakati gani walipokuwa kwenye eneo la goli la Yanga. Clatous Chama, Sakho na Kibu walifika sana lakini hawakujua kumaliza mechi mapema. Yanga hii mechi alishakubali mapema lakini hatujua tufanye nini baada ya goli moja, walivurugika mno wakati waliposhambuliwa.

Outara beki mzuri lakini mzito hana kasi na sio mtu wa kujitoa, huyu ni Pascal Wawa mwenye kimo kirefu. hii mechi angeanza Onyango na Henock pengine hii dhahama isingetukuta. Huyu bwana Outarra hakua na la kufanya pale alipopitwa japo hatua moja, hajuai hata kuvuta mtu shati kama ameshindwa Kuslide?

Mkude kama kiungo mkabaji, huyu jana hakua na msaada kwenye eneo la ulinzi. Jonas Mkude ni overrated player, hua anatekeleza nusu tu ya majukumu yake huku akikwepa moment za lawama, hana kasi. Hapa Simba warudi sokoni kutafuta kiungo mkabaji wa viwango vya CAF, to me Kanoute is far better.

ISRAEL MWENDA. Huyu ni kama viatu vya kucheza kama fullback wa SIMBA SC vinampwaya, hana uwezo wa kumudu haya majukumu tunamuonea tu, David Kameta 'Duchu' was better than him.

Mohammed Husein ni beki mwenye nidhamu za kuzamani. Unakubalije tobo na mpiga tobo wote wanapita huku ukiwa nje ya box? Hii si mara ya kwanza kukubali kupitwa kirahisi bila kucheza japo faulo kuokoa timu. Poor team captain!😔

Kocha. Kikosi alichoanzisha Coach Zoran ni dhaifu. Watu kama Kakolanya, Israel Mwenda, Kyombo hawakupaswa kuanza. Sub ya kuwaingiza Okra, Okwa, Mzungu nadhani ilikua na lengo la kuwachanganya Yanga lakini waliishia kujichanganya wenyewe.

Mwisho. Mashabiki wa Simba nao wajifunze kucheza game nje ya uwanja kama wanavyofanya waYanga. Mashabiki wa Yanga walianza propaganda za mara refa ni Simba mara Tff cjui hivi cjui vile. Hizi siasa hua zinaathiri sana saikolojia ya refa na mda wote anawaza kuprove kwamba yeye sio Simba mwishoe tunaumia hasa kwenye maamuzi ya 50/50. Hii si mara ya kwanza wanatumia hii mbinu na imekua ikiwafaidisha sana. Mwanza pia ilikua hivyo kwa Arajiga. Utaona hii siasa itarudi watakapoona msala wao wa kumtumia Manara kwenye Yanga day unaenda kutolewa hukumu na sio ajabu TFF wataufyata.
 
Tatzo mnaaminishwa ujinga na mnakubali,hamna kikosi cha maana OVER
 
Back
Top Bottom