Kilichofutikwa ni uvundo

Kilichofutikwa ni uvundo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,341
Reaction score
829,493
1473068771000.jpg
sikutaka tuwe na post leo..ilikuwa tupumzike..mishemishe za kilingeni jana zilikuwa si haba
Lakini hebu tujadili kidogo hili la maiti(sio marehemu)
Maiti ni mzoga pumzi ikishatoka imetoka kinachofuata ni mchakato wa kuanza kuoza/kuvunda, kuharibika na baadae kuwa mabaki ya mwili na vile utakavyozikwa navyo kama ukibahatika kuzikwa (si kila mmoja anajaaliwa mazishi)
Pamoja na mazishi ya gharama sana pamoja na majeneza ya thamani kubwa pamoja na kuzikwa na Vito na vitu vingine vya thamani..kilichofutikwa humo ni uvundo mtupu......
Ukishafukiwa kifuatacho ni uvundo tuu hadi nyama zote zitakapoliwa na funza na bakteria chini ya ardhi
1473069389090.jpg

Upuuzi wa wengi ni pale marehemu kabla ya kifo chake Kuteseka na kuugua sana bila misaada ya ndugu na marafiki...ama la kwa wale wanaojiweza kufanya mazishi ya kufuru kwenye mwili unaooza
Dhima ya kufanya yote haya ninini?
Sifa?
Upendo?
Kujali?
Kumbukumbu?
Kuiga?
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na jibu lake lakini vyovyote iwavyo tukubali tukatae kufuru kwenye mzoga wakati kuna watu bado wana uhitaji ni laana
 
Sasa kama ni hivi mbona kama alisema azikwe nyuma ya nyumba msipo fanya hivyo inakuwa mtafutano, ni kweli matendo yoyote kwenye maiti hayana faida wala hasara kwa maiti?????
 
Sasa kama ni hivi mbona kama alisema azikwe nyuma ya nyumba msipo fanya hivyo inakuwa mtafutano, ni kweli matendo yoyote kwenye maiti hayana faida wala hasara kwa maiti?????
Yana faida au hasara kama kuna kauli/wosia wake
 
Bora kuchomwa moto Mungu kosa baniani kosa Aridhi kosa

Moto faidi jivu tupa bahirini

Baniani nux saana
 
Akiwa mgonjwa hata wakumpa dawa hakuna aikfa tu ndugu watatokea na wengine utakuta walikwepo ulaya huko jmn ebu tubadilike duuh
Na huo ndo ushahidi tosha kwamba binadamu hatupendani kabisa! Mtu akiwa mzima hakuna wa kumletea mayai / juice ili aendelee kuwa mzima. Ikitokea akaugua na kulazwa hospital,, ndo watu wanaandamana na vyakula vya kila aina huku wakijua kuwa hawezi kula hivyo vyakula .. akifariki tu, hapo ndo balaa, ufahari wa kila mtu utaonekana hapo siku ya msiba!
TUPENDANE TUKIWA HAI JAMANI
 
Back
Top Bottom